RASMI - UEFA yaondoa sheria ya goli la ugenini

RASMI - UEFA yaondoa sheria ya goli la ugenini

Uamuzi muafaka kabisa huo sheria nyingine ambayo inabidi kuangaliwa ni hii ya kuzidi (Offside).
 
Yule Refa alikuwa ni shabiki wa man u na alishawekaga wazi enzi zake kuwa Chelsea ni timu iliyozaliwa 2004( imagine pale ilikuwa 2009) hivyo mechi yeyote ikichezwa vs Chelsea basi Kuna uwezekano Chelsea ikapoteza iyo mechi. Aliitwa Howard Web[emoji4] huyu jamaa mashabiki wa Chelsea hatutomsahau aise.
Kwani uongo mkuu chelsea si imezaliwa 2004, au ulitaka aseme ilizaliwa 1900?.
 
labda alimaanisha kuzaliwa kama elite club mkuu, maana kuanzia 2004 chelsea imekuwa club kubwa na imefanya vizuri tofauti na miaka ya nyuma ya 2004
Ni kweli kabisa mkuu ..lakini kabla ya hapo Chelsea tulifanya makubwa tu sema 2004 kuendelea ndo mafanikio yaliongezeka zaidi.
 
na Mlleta Mada denooJ utuwekee hiyo Link wengine hatuamini mpaka tupapase wenyewe ipo siku mtayaondoa na hayo ma miligoti kkuwsiwe na magoli hata ya ugenini. Mm naona bora yaendelee Vilabu km vya Misri ni wababe sana mkienda malizia kwao.
juzi kaizer chief kashinda moroco, hakuna cha ubabe ni kujipanga tu
 
na Mlleta Mada denooJ utuwekee hiyo Link
wengine hatuamini mpaka tupapase wenyewe
ipo siku mtayaondoa na hayo ma miligoti kkuwsiwe na magoli hata ya ugenini
Mm naona bora yaendelee Vilabu km vya Misri ni wababe sana mkienda malizia kwao
Habari iko BBC, Skysports google utaiona.
 
Hii mimi naunga mkono hoja.

Sikubaliani kabisa na hii sheria ..eti ya kuotea.

Waache hata kama mtu ataamua kupumzika kwa kipa pinzani.

Watu wacheze mpira.
Hahah tena sheria inategemea na refa anavyoitafsiri akishindwa mmeliwa ndo maana sasa kuna refa wa pili ambaye ni VAR
 
Nakumbuka Yanga (ya akina Tenga) walikuwa wahanga wa hii sheria mwaka 1975 wakati walipotolewa kwenye hatua ya pili katika michuano ya klabu bingwa Afrika ambapo walitolewa na Enugu Rangers International ya Nigeria baada ya kutoka sare ya 0-0 Lagos na 1-1 Dar es Salaam.
 
Yani unataka kuuwa mpira
Yaan sheria hata marefa hawawezi kuitafsiri mpaka wameletewa VAR. Isitoshe kuna off side trick yaan mpaka unakosa ladha ya mpira.
Kila siku utata tuu mbona huyo ya goli la ugeniji halikua na utata kama off side trick?
 
Mpira wa miguu siyo rede chief. Ungekua unaangalia mpira ungejua kwanini offside ilikua introduced.
Mpira ukiingia golini kidogo letsay ⅓sio goli ila mchezaji ukizidi hata ukucha tu sio mpaka mwili mzima off side. Isitoshe hata refarees zinawachanganya ndo maana wakaleta VAR
 
Hii mimi naunga mkono hoja.

Sikubaliani kabisa na hii sheria ..eti ya kuotea.

Waache hata kama mtu ataamua kupumzika kwa kipa pinzani.

Watu wacheze mpira.
Sheria ya kijinga et mpita mpaka uingie wote golini ndo goli ila ukizidi ukucha tuu umeotea,
 
Mpira ukiingia golini kidogo letsay ⅓sio goli ila mchezaji ukizidi hata ukucha tu sio mpaka mwili mzima off side. Isitoshe hata refarees zinawachanganya ndo maana wakaleta VAR
Refarii haziwachanganyi.

VAR haiangalii offside peke yake.

Ndiyo maana yanaletwa maboresho kwa mambo ya kuzidi ukucha au jezi.
 
Back
Top Bottom