Rasmi: Yanga na Simba kukutana Septemba 16 katika mechi ya Ngao ya Jamii

Rasmi: Yanga na Simba kukutana Septemba 16 katika mechi ya Ngao ya Jamii

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Ngao ya Jamii Kuzindua Rasmi Msimu Mpya wa Mashindano ya TFF

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linapenda kuwataarifu wadau na mashabiki wa soka kuwa mechi ya Ngao ya Jamii (Community Shield) itakayozindua msimu mpya wa mashindano itachezwa tarehe 16 Septemba 2025 jijini Dar es Salaam, ikiwakutanisha klabu ya Young Africans SC na Simba SC.

Kwa mujibu wa marekebisho ya kanuni yaliyopitishwa na Kamati ya Utendaji ya TFF katika kikao chake cha hivi karibuni, mfumo wa mashindano ya Ngao ya Jamii umebadilika. Endapo ratiba za mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) zitaingiliana na ratiba za ndani, Ngao ya Jamii itachezwa kwa mchezo mmoja tu wa fainali, badala ya mfumo wa awali uliokuwa na mechi tatu (nusu fainali mbili na fainali).

Mabadiliko haya yamezingatia ukweli kwamba Tanzania ni mwenyeji wa Fainali za CHAN 2025, zinazochezwa kuanzia tarehe 2 Agosti hadi 30 Agosti 2025. Aidha, mwanzoni mwa Septemba, timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) itashiriki michezo miwili ya mchujo wa Kombe la Dunia. Baada ya Ngao ya Jamii, klabu zetu zitakuwa na majukumu ya kushiriki mechi za raundi ya awali ya mashindano ya CAF.

TFF inawaomba wadau na mashabiki kuendelea kuunga mkono juhudi hizi katika kukuza na kuendeleza mchezo wa soka nchini.

=====

Imetolewa na:
Cliford Mario Ndimbo
Ofisa Habari na Mawasiliano, TFF
20 Agosti 2025
Taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)@taifastars_ @caf_online @ligikuu @b...jpg
 
Kila mwaka itakua ni kuchezesha kanuni tu ...lazima Simba vs Yanga wakutane? 😂🙌
 
Karia na TFF yake wanatapatapa mpaka basi! All in all, dakika 90 za mchezo zitaamua matokeo.
 
Back
Top Bottom