Serikali pia inabidi ilegeze masharti ya kutoa passport vijana wetu waweze kutoka nje kirahisi na kwenda kutafuta maisha huko. Kuwarundika tu hapa ndani wakati ajira hakuna kuna faida gani? Kuna fursa huko nje Watanzania zinatupita kwa sababu ya ukiritimba tu na mambo ya ajabu ajabu yasiyo na maana. Hakuna sababu ni kwa nini kijana wa Kitanzania aliyesomea Kiswahili, kwa mfano, aendeshe bodaboda wakati Kiswahili sasa hivi ni hotcake dunia nzima na Wakenya ndiyo wanatamba huko nje sisi tupo tu pamoja na kwamba ndiyo tunaongea Kiswahili fasaha kabisa!
Wafungue mipaka. Vijana watoke nje wakapate exposure kuhusu dunia inavyokwenda. Waibe na teknolojia huko wakiweza. Waende wakapige boksi huko na maisha yaende. Rwanda, kama sikosei, diaspora wanatambuliwa kama mkoa wa sita kiutawala na wanachangia asilimia ya kueleweka katika pato la taifa kupitia home remittances. Hakuna sababu Tanzania iwe ya mwisho kwa kuwa na diaspora katika nchi za ukanda huu wa Afrika.
Yaani sisi karibu kila kitu kigumu sijui kwa nini 😬😬😬