MSAGA SUMU
JF-Expert Member
- May 25, 2015
- 6,661
- 21,656
Heshima mbele wakuu,baadhi ya ratiba ya mh Magufuli kwa miaka 2018 mpaka 2025,mabadiliko yanaweza kutokea kidogo (lkn tegemea baadhi ya vitu kuongezeka ila sio kupungua)
- September 2018 rais Magufuli atakuwa anazindua daraja la magari la kupita juu (kwa lugha ya kitaalam linaitwa MANY LANES EXTRAORDINARY FLYOVER)
- October 2018 rais Magufuli atakuwa anazindua mradi mkubwa wa maji wa mto wa Malagalasi ,mradi huo utagharimu mabilioni ya shilingi na utahudumia maelfu ya mamia ya wananchi.
- November 2018 rais Magufuli atakuwa anapokea ndege mbili nyingine mbili aina ya Bomberdier C-series ikiwa ni mwendelezo wa serikali ya Tanzania kununua ndege na mandege ya maana.
- Desemba 2018 Magufuli kuweka jiwe la ujenzi kuashiria kuanza rasmi mradi wa aina yake ya ujenzi wa Hydropower kubwa barani Afrika nyuma kidogo ya Ethiopia.Stiglers itakuwa na uwezo wa kuzalisha 2100MW.Tusisahau kuwa Kenya kwa sasa pamoja na kelele zake zote umeme wanaozalisha ni 1337MW (KenGen owns thirty one (31) power generating plants with a combined installed capacity of 1,337MW )
- Januari 2019 Magufuli atakuwa anaweka jiwe la ujenzi kuashiria kuanza mradi wa BRT phase 2. Mradi huu utashuhudia serikali ya Tanzania ikichoma pesa za kimerakani zaidi ya milioni 160. Tusisahau Kenya inahitaji dola milioni 70 kumaliza kabisa tatizo la njaa.
- Februari 2019 rais Magufuli akiwa anatoka mapumzikoni kijijini kwake Chato atapita jijini Mwanza kufungua uwanja wa kisasa jijini Mwanza baada ya kukamilika kwa ukarabati. Ukarabati huo uliogharimu kiasi cha Sh bilioni 105 zilizotumika kujenga jengo la mizigo, mnara wa kuongozea ndege, kuhamisha mto na kuongeza urefu wa mita 500 eneo la kurukia ndege.
- Machi 2019 rais atakuwa anaweka jiwe la msingi kuashiria kuanza ujenzi wa reli kwa kiwango cha kimaifa kutoka Dodoma kuelekea Isaka.Reli kufika Isaka kwa lugha ya kijiografia inamaana ni kuwa tuko Kigali na Bujumbura kiroho,kinachosubiriwa ni kufika kimwili tu.