Ratiba ya kutoa heshima ya mwisho kwa askari Polisi waliofariki kwa ajali ya gari

Ratiba ya kutoa heshima ya mwisho kwa askari Polisi waliofariki kwa ajali ya gari

Mungu wetu anazidi kutukumbusha: Hakuna ajuaye siku wala saa. Tuitafute hekima ya Mungu ili tujue kuwa hakuna anayemiliki au aliye na mamlaka kamili ya kifo. Mwanadamu usithubutu kuifanya njia ya wote ya kuondoka Duniani kama ndiyo namna ya kuwatishia au kuwaadhibu binadamu wenzako au ukajisahau ukaona wewe una mamlaka ya kuamua nani aishi na nani afe wakati gani.

Wanadamu tumrudie Mungu wetu, hasa wale watekaji na wauaji waliokifanya kifo kama ni mali yao na hivyo kuwaua wanadamu wenzao, huku wakiwa wamevikwa na uwendawazimu, hata wasijue kuwa hakuna mwanadamu mwenye mamlaka juu ya kifo.

Unaweza kupumbazika kwa sababu una bunduki, una bomu, au madaraka ya kuamuru kuua, hata ukaamini kuwa kwa kuwa wewe unaua wenzako wakati upendao, ukadhani una mamlaka pia ya kukizuia kifo dhidi yako.

Mungu wetu ana njia nyingi za kuwaonya wanadamu:

Aonapo wenye bunduki wamejitwalia mamlaka ya Mungu, na kuwaua wanadamu wengine, Yeye huwaondoa bia hata ya mshale, ili wajue kuwa bunduki haizuii kifo.
Aonapo wenye mamlaka wakitoa amri ya watu wengine wauawe, wakiamini wana uwezo wa kuamuru nani aishi na nani aondoke, huweza kuwachukua kwa namna nyingine, bila ya amri ya yeyote, ili wajue kuwa mamlaka yao hayawapi umiliki wa uhai wao au wanafamu wenzao.

Matajiri wanapojisahau na kuamini kuwa utajiri unaweza kuzuia kifo, Muumba huweza kumchukua tajiri, tena wakati mwingine bila ya kunywa hata aspirini ya buku 1, huku akiwa ameacha mabilioni bank.

UJUMBE WA MUNGU:

Wanadamu tupendane, tuvumiliane, tusameheane , huku tukijua kuwa hata tuwe na mamlaka makubwa kiasi gani, juu yetu kuna nguvu tusiyo na mamlaka nayo, nayo ni MUNGU MWENYEWE.
Tuwakumbuke ndugu zetu waliouawa 29 Oct kama nzi, tumwombe Mungu awajalie pumziko jema la milele. Lakiniwale wauaji na waliotoa amri, geuzeni njia zenu, fanyeni toba kamili mkijutia mliyoyafanya. Si bunduki wala madaraka yenu kitakachozuia ukuu wa Mungu juu yenu.

Hao waliokufa wamemaliza safari yao ya hapa Duniani, funzo na ujumbe ni kwetu ambao bado tupo katika Ulimwengu huu.

Mungu wa huruma na rehema awape faraja wanafamilia wa marehemu wote. Pamoja na masikitiko yote, lakini angalao ninyi mtailaza miili ya wapendwa wenu kwa namna mpendayo, lakini tuna maelfu ya familia ambazo ndugu zao baada ya kuuawa, walitupwa baharini, ziwani na maporini, na kuanywa kuwa chakula cha wanyama na wadudu. Hawa majonzi yao, huzuni zao, hazielezeki, Mungu Mkuu awape faraja ile ambao mwanadamu hawezi kuitoa.
 
View attachment 3675615taarifa ya kutoa heshima ya mwiaho
Ratiba yangu nikula Raha hizi siku mbili na kumpongeza dereva wa roli aisee
downloadfile-49.jpg
 
Back
Top Bottom