Ratiba ya PlayOff ya ligi kuu Tanzania bara, unatabiri yapi kutokea ?

gearbox

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2024
Posts
563
Reaction score
1,768
kati ya jkt na tabora atakae shinda nje ndani anarudi ligi kuu, alieshindwa anapewa nafasi nyingine kujipima kwa biashara united, kati yao ataeshinda anapanda ligi kuu, anaeshindwa anashuka Ligi Daraja la Kwanza.

ROUND 1

🕳️Tabora United vs Jkt Tanzania - 04/06/2024

🕳️JKT Tanzania vs Tabora United - 08/06/2024

ROUND 2

🕳️Biashara vs alieshindwa round 1 - 12/06/2024

🕳️Alieshindwa round 1 vs Biashara - 16/06/2024
 
BIASHARA UNITED WILL RECORVER TO THE NEXT LEVEL IN PREMIER LEAGUE 👀👀
Na mimi napenda Biashara warudi ila ni ngumu sana.

Tabora na Jkt wana advantage ya kuwa fiti kucheza, hao biashara mara ya mwisho wamecheza mwezi uliopita.

Timu za ligi kuu zinapewa milioni 50 kila mwezi, wana advantage ya maandalizi pia wanaweza tumia nguvu ya pesa kuzihujumu timu za ligi za chini.

Timu za ligi kuu zina wachezaji bora zaidi, pesa za mishahara zipo.
 
Utabiri wangu/

Jkt na Tabora wanaenda matuta.. Jkt anatolewa

Jkt anaifunga Biashara, Napenda sana Biashara united irudi ligi kuu lakini ni ngumu kuwafunga Jkt wakiongozwa na Shiza Kichuya
Unaweza ukawa sawa kabisa ila wasiwasi wangu mimi siko mbali sana na utabiri wako ila kama tabora U angeanzia ugenini naamini angetoboa hao jamaa tangu championship msimu ule wanagombania kupanda game zao zilikuwa ngumu mno na zina mengi ndani yake.
 
Hii ni point, lakini nao biashara imekuwa kawaida yao huwa wanaanza vizuri sana ligi ya championship lakini mwishono wanajikwaa wanaishia nafasi za kucheza playoff
 
Na mimi napenda Biashara warudi ila ni ngumu sana.

Timu za ligi kuu zinapewa milioni 50 kila mwezi, wana advantage ya maandalizi pia wanaweza tumia nguvu ya pesa kuzihujumu timu za ligi za chini...
BIASHARA UNITED WAPAMBANE WAPATE USHINDI KURUDI LIGI KUU 👀👀
 
Tabora anatolewa, afu anafanya comeback tena?
Kuna nafasi mbili kwa timu za ligi kuu kwenye playoff

kati ya jkt na tabora atakae shinda nje ndani anarudi ligi kuu, alieshindwa anapewa nafasi nyingine kujipima kwa biashara united, kati yao ataeshinda anapanda ligi kuu, anaeshindwa anashuka Ligi Daraja la Kwanza.
 
Kuna nafasi mbili kwa timu za ligi kuu kwenye playoff

kati ya jkt na tabora atakae shinda nje ndani anarudi ligi kuu, alieshindwa anapewa nafasi nyingine kujipima kwa biashara united, kati yao ataeshinda anapanda ligi kuu, anaeshindwa anashuka Ligi Daraja la Kwanza.
Nimekuelewa mkuu, ila nahisi huko mbele waje wafanye tu timu za daraja la chini zipande Moja kwa moja
 
Timu 2 za daraja la chini zimepanda moja kwa moja - Kengold ya Mbeya na Pamba ya Mwanza.

Timu 2 za Ligi kuu zimeshuka moja kwa moja - Mtibwa ya Morogoro na Geita Gold ya Geita

Hizi playoffs zina lengo la kuongeza ushindani ligi kuu, timu 2 za ligi kuu na moja ya ligi ya chini zinashindana kuwania nafasi mbili za kurudi / kupanda ligi kuu, timu dhaifu inashuka / kurudi ligi ya chini.
 
Timu za ligi daraja la kwanza kuwatoa timu za ligi kuu huwa ni nadra sana. Timu za ligi kuu zina zaidi ya 70% kurudi. Hivyo nawapa Tabora Utd na JKT nafasi za kuruadi.

Ilitokea mara moja tu kwa mashujaa kuiondoa Mbeya City.
 
Mashujaa kuiondoa mbeya city na pia Ihefu kuiondoa mbao fc
 
kati ya jkt na tabora atakae shinda nje ndani anarudi ligi kuu, alieshindwa anapewa nafasi nyingine kujipima kwa biashara united, kati yao ataeshinda anapanda ligi kuu, anaeshindwa anashuka Ligi Daraja la Kwanza.

ROUND 1

[emoji2734]Tabora United vs Jkt Tanzania - 04/06/2024

[emoji2734]JKT Tanzania vs Tabora United - 08/06/2024

ROUND 2

[emoji2734]Biashara vs alieshindwa round 1 - 12/06/2024

[emoji2734]Alieshindwa round 1 vs Biashara - 16/06/2024
tff kisanga,
mbona mwaka jana zilikua timu 4 ?(2 za ligi kuu na 2 za daraja la 1)
 
Timu 2 za daraja la chini zimepanda moja kwa moja - Kengold ya Mbeya na Pamba ya Mwanza.

Timu 2 za Ligi kuu zimeshuka moja kwa moja - Mtibwa ya Morogoro na Geita Gold ya Geita

Hizi playoffs zina lengo la kuongeza ushindani ligi kuu, timu 2 za ligi kuu na moja ya ligi ya chini zinashindana kuwania nafasi mbili za kurudi / kupanda ligi kuu, timu dhaifu inashuka / kurudi ligi ya chini.
mwaka jana hawakufanya hivi,
usikute secretary wa tff anataka timu ya kwao (tabora utd) ibaki ndio mana kapindua sheria
 
JKT wakicheza kwa mzuka ule wa juzi na Simba,watatoboa asubuhi tu.

Hao united wawili wakikutana,haitabiriki!
 
Tabora anamfunga JKT nje ndani halafu JKT ataenda kumtoa Biashara United.
Tabora na JKT watarudi ligi kuu
 
Natamani Biashara United Mara warejee ligi kuu kwa mfunga yoyote hapa awe JKT au Tabora United.
 
Back
Top Bottom