Ratiba za masomo kuongezewa muda wa masaa mawili kutakuwepo na malipo ya ziada kwa walimu?

Ratiba za masomo kuongezewa muda wa masaa mawili kutakuwepo na malipo ya ziada kwa walimu?

Njaa kwa watoto na Usafiri mida hiyo unaanza kuwa shida ...
 
Kwa sie ambao muda wa kutoka kazini ni saa 10:30 hakuna kilichobadilika. Na bahati nzuri watoto hupata uji na lunch shuleni.

Taabu ni kwa zile shule ambazo hazina utaratibu wa chakula, hapo ndipo ninapowawazia hawa watoto!!!
 
Hata Kama magu ni boko jamani muwe na shukrani miezi mitatu kawalipa huku mnaendesha miradi yenu khaaa
Hakuna kipengele cha CORONA kwenye mkataba....umenitoa kwangu Mwanza umenileta Tandahimba kwa mkataba wa kudumu..nikae kituoni nifanye kazi...kulipwa ilikua na lazma ndo maana alishajibia hilo kuwa hata Corona ingekaa kwa miaka 10 angetulipa...Mbona nikiugua hata miez 6 huwa nalipwa kwani ugonjwa nimejipa Mimi??
 
Zamu yenu kuisoma namba,

Km mlikuwa mnaona raha kula vya Bure, Sasa mtavilipa, wale mlioenda kulima mtajiju, hakuna mapumziko babaaa, ngoma hd 12
 
Hahahah watu wanawaponda walimu hapa nyie hamjui aisee hio ratiba itachingia utoro mashuleni [emoji3][emoji3][emoji3]

Saa 8 tu Kuna wanafunzi wanapaona mbali sana sauze as 10 halafu unakuta home hapewi hata shilingi kumi

Kuna wanafunzi wako standby na saa na kengele[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Daah walimu watakoma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Walimu bwana; miezi mitatu mmelipwa bila kufanya kazi hata lisaa limoja leo mnahoji kuongezewa masaa mawili?

Kwa kukufanunuliwa masaa ya kufanya kazi kisheria ni 40 - 45 kwa wiki. Kama unaingia kazini saa 1.30 mpaka Mpaka saa 10-30 jioni ukiondoa lisaa limoja la mapumziko ya chakula utakuwa umefanya kazi masaa 8 hivyo kwa wiki masaa 40 ambayo yako kisheria.
Kama unafikiria kwa umakini hiyo miezi mitatu imefidiwa na itafidiwa kwenye likizo zijazo ,mantiki ya kua tulipokea mshahara wa bure haipo ,pia kwenye halmashauri yangu tulikua tukitoa mazoezi na kuyasahihisha
 
Hata Kama magu ni boko jamani muwe na shukrani miezi mitatu kawalipa huku mnaendesha miradi yenu khaaa
Kua muelewa usiwasikilize wanasiasa muda huo utakatwa likizo ,mwezi wa nne kunakuaga na likizo ya wiki mbili ,wa sita mwezi mmoja ,wa 9 wiki mbili halafu desemba shule zitamaliza muhula desemba 18
 
Walipwe overtime ya nini, mbona wamelipwa miezi mitatu bila kufanya kazi, na mwezi wa tatu walifanya nusu mwezi wakalipwa full[emoji848]
Ukiwa likizo hulipwi mshahara ? Muda uliopotea utafidiwa kwenye likizo kama ulimsikiliza vzuri mwalimu
 
Waziri wa Elimu katia waraka na ratiba mpya za mihula ya shule jana.

Ndani ya waraka huo kaongeza muda wa masaa mawili kwenye RATIBA za shule yaani zianze SAA 2:00 asubuhi hadi SAA 10:00 jioni badala ya SAA 8:00 mchana.

Katika kuongeza huku hakuzungumzia malipo ya ZIADA (overtime) kwa walimu ambao no watekelezaji na wasimamizi wa RATIBA hiyo.

Nauliza je, amesahau kuwa muda wa kazi kwa mwajiriwa wa umma unaishia SAA 9:30 alasiri? Kama kaongeza muda wa kazi haoni kuwa Kuna haja ya kumlipa ZIADA huyu mwalimu kwani naye muda wake wa kazi hautofautiani na wafanyakazi wa kada nyinginezo?

CWT na hata serikali watoa majibu ya kama KUTAKUWEPO na malipo ya ziada na kinyume chake kutaleta mgogoro wa kikazi kati ya mwajiriwa na mwajiri.
Wakati wa likizo ya Corona mbona hamkusema msilipwe? Pigeni kazi
 
...but wakati shule zimefungwa si wamelipwa mishahara kama kawaida? Kumbuka kada nyingine za ajira ziliendelea na kazi wakati walimu wakipumzika katika kipindi chote cha corona.

Mawazo yangu tu.....najaribu kuwa fair

But overtime zinategemea mkataba wa ajira...kama ipo, ipo tu.
Huo muda utafidiwa kwenye likizo ,kwa iyo ukisema walimu walipokea mishahara ya bure sio sahihi
 
Masaa mawili machache wangeongeza 3.
mimi nitapiga kazi hadi saa tatu usiku.
 
Mimi ni mwalimu. Wakat watoto wapo nyumbani nilikuwa natoa kazi watoto wafanye na nasahihisha madaftar karibua elfu moja kwa wiki. Hilo lilikuwa agizo la katibu tawala wa mkoa niliopo.

Sasa hayo masaa mawili ya ziada yapo kisheria na posho inatakiwa iwepo. Vinginevyo naona kama wanapigia mbuzi gitaa. Sina mpango wa kukaa mpaka muda huo. Mm ikifika saa 7 mchana nachora nipo geto.

Tafuta njia nyingine ya kuelezea matatizo yako na namna ya kuyatatua ama sivyo " Mpiga ngumi ukuta huumiza mkonowe" binafsi nilishaona Mwalimu kijana sana ametoka chuo akataaka kuweka ujinga kwenye kazi za serikali kwa kudharau maazimio ya kamati ya Afya ya Kijiji mwisho wake alipata miezi yake sita safi gerezani na alipotoka aliishia kwao huko Musoma na dunia haikusimama
 
Nipo nafanyia utafiti Nadharia ya UALIMU NI WITO na hivi karibuni nitakuja na andiko,.. linalothibitisha kua kweli Kada hii ni Wito....
Mwl WA Chemistry na Biology .
 
Back
Top Bottom