Rav 4 old model 1990

Rav 4 old model 1990

KINGSLEE

JF-Expert Member
Joined
Aug 30, 2013
Posts
830
Reaction score
1,046
Habar wadau
Naomba kujua mambo ya kitaalam kuhusu hili gari.
lina injin aina ya 3S 1990 cc, 4WD
Naskia ni Imara sana na liko vizuri kwenye Rough road
PLz kwa mwenye Ujuzi nalo; Naomba kujua gari hili naweza nikafunga Injini ya Aina gan Automatic ambayo inaweka ikafiti na ambayo itakuwa ni kuanzia 1300cc mpaka 1500cc..
 
sawa mkuu
je gari hiiunaweza ukafunga injini gani ambayo ni ndogo kuliko hiyo
Samahani mkuu, kwanini unataka kubadilisha uweke ndogo zaidi? Kwamba hiyo 3s iliyomo ni kubwa sana ukilinganisha na mahitaji yako?
 
Habar wadau
Naomba kujua mambo ya kitaalam kuhusu hili gari.
lina injin aina ya 3S 1990 cc, 4WD
Naskia ni Imara sana na liko vizuri kwenye Rough road
PLz kwa mwenye Ujuzi nalo; Naomba kujua gari hili naweza nikafunga Injini ya Aina gan Automatic ambayo inaweka ikafiti na ambayo itakuwa ni kuanzia 1300cc mpaka 1500cc..
Rav4 karibu zote ni ngumu aise. Suala la kubadilisha engine sahau kabisa. Utakuwa teja wa garage. Kwanza engine ya cc1300 sidhani kama inaweza kumudu uzito wa hilo gari.

Pia hiyo model ya kwanza Rav4 ni too old aise. Watu wanaisifia kuwa ni ngumu, lakini kwa upande wa technology na comfortability it is too outdated. Hivi kweli, kwa nini ununue gari la model ya miaka 25 iliyopita? Hilo gari limetoka Mzee Mwinyi akiwa rais, ndani ukiingia halina tofauti saana Kirikuu. Any way, ni mtazamo wangu.
 
Sawa mkuu nimekuelewa vizuri.
Naomba utambuwe Lengo langu sio kumiliki gari linalokwenda na wakati!
Nimejaribu kutafuta gari yenye cc ndogo kuanzia 1300cc mpaka 1500cc ambayo itakuwa na 4WD na imara nikakuta nyingi ni kuanzia 1990cc kuendelea.
Nakubaliana na baadhi ya Wadau wakishauri Toyota Cami au Suzki Jimmy ila sasa cha ajabu hizo gari sina mzuka nazo kabisa kwasababu siti zake zimejibana sana na mwonekano wake haunivutii.

Alternative;
Ni Rav 4 Model gani ambayo kwa upande wa technology na comfortability nikiweka injini ya 1500cc itaweza kumudu uzito wa gari?

Kama unaweza kuifaham Plz weka na Picha itapendeza zaidi..

Nahitaj gari ya kazi kwamba nikienda shamba nafika mpaka sait na sitak gari ya kula bata kwenye Lami tuu.

Au gari yeyote ile from different types (Siyo Rav 4 tuu) yenye CC hizo na yenye 4WD ambayo itanifaa kwenye mishe zangu za kwenda shamba na kurud twn...
 
Tafuta Suzuki Grand Vitara 2nd Gen zile zinaanzia mwaka 1998 mpaka 2005. Kuna yenye cc1600, japo ni chache saana zenye cc1600. Ila zipo. Zina top speed ya 150kph au 160kph nadhani. Ila ni very capable off road maana zile ni proper 4WD kabisa, zina low range gearbox, sio AWD kama kina Rav4.
1097462
1097463
 
View attachment 1097462View attachment 1097463
Hizi suzuki Grand Vitara bei yake ikoje?.. Nimependa speed ya 150 maana mimi sinaga haraka kabiea barabarani
 
Ni kati ya Tsh 13m mpaka 20m. Sio zote zina speed ndogo, ni hizo za cc1600 pekee. Zipo zenye 220kph pia.
 
Mkuu hizi suzuki 4wd yake ni powerful kuliko subaru forester au nissan xtrail?
 
Ndio mkuu. Grand Vitara ni proper 4-Wheel-Drive. Hao wengine wana kitu wanaita AWD, ila Subaru ana technologia nzuri saana ya hii kitu wanaita Symmetrical AWD, hii tairi zote nne zinazunguka kwa wakati mmoja. So kwa matumizi ya on road conditions, Forester itafanya vizuri kuliko Grand Vitara. Xtrail pia wako vizuri, japo na wao ni AWD, ila ina modes tofauti. Yao unaweza kuchagua kati ya 2WD, AWD (ambapo unguvu inazungukuka kwenye tairi zote nne, ila nguvu zaidi inapelekwa kenye tairi lenye grip zaidi) na mwisho kuna option ya ku lock diff ya kati, so nguvu inagawanywa sawa kati ya tairi za mbele na za nyuma na zinazunguka pamoja.

Hitimisho: Grand Vitara ni nzuri zaidi offroad, Forester ni nzuri zaidi on road,ila ina uwezo mzuri pia offroad, Xtrail ipo katikati. Maana ina the best of both worlds.
Ila Grand Vitara inakosa kitu wanaita diff lock. Ingekuwa na hiyo kitu, ilikuwa inakwenda njia moja na kina Jeep na Land Cruiser.
 
Ni kati ya Tsh 13m mpaka 20m. Sio zote zina speed ndogo, ni hizo za cc1600 pekee. Zipo zenye 220kph pia.
Mkuu inaonekana unaijua vizuri hii gari... Vipi fuel consuption yake ikoje?.. Lita moja inakwenda km ngapi?
 
Mkuu hiyo kitu consumption yake ni kati ya 7-8 mjini na 10-11 highway. Kama ni automatic gearbox. Kwa manual gearbox inakuwa better kidogo, japo ni kama km 1 au 2.
 
Habar wadau
Naomba kujua mambo ya kitaalam kuhusu hili gari.
lina injin aina ya 3S 1990 cc, 4WD
Naskia ni Imara sana na liko vizuri kwenye Rough road
PLz kwa mwenye Ujuzi nalo; Naomba kujua gari hili naweza nikafunga Injini ya Aina gan Automatic ambayo inaweka ikafiti na ambayo itakuwa ni kuanzia 1300cc mpaka 1500cc..

Usithubutu badili engine, bora ununue ya kiwango cc hizo kama ist
 
Back
Top Bottom