Rav4 Inapunguza Mwendo ghafla nikiachia Accelerator

Rav4 Inapunguza Mwendo ghafla nikiachia Accelerator

Swali la mwisho, Je Mfano ukiwa hiyo speed 100 ikianza kujipunguza mwendo huwa mpaka inasimama kabisa au huwa inajipunguza tu na kuanza kwenda mdogo mdogo?
Hapa mimi nakushauri mtafute fundi akufanyie adjustment kwenye brakes zako,isikijekuwa zinakamata sana hivyo ni lazima utumie nguvu ku accelerate au inasimama ghafla unapoachia accelerator ukiwa kwenye high speed.Unajua nimegundua kwanini watanzania wengi tunajua ABC za ufundi magari,hii inatokana na tabia yetu ya kununua magari used kitu,kinachotufanya tuwe watumwa wa mafundi garage,huwezi kukuta mtu amenunua gari imetembea km 500 kafungua bonnet ya gari yuko garage,labda kama imepata ajali,na mleta mada hapa na RAV 4 yake tayari naona naye ameshaanza kujifunza ufundi wa magari taratibu....
 
Poa... Karibu
... nitakuwa mkosefu wa fadhila nisiposhukuru wadau wote walionipa maoni yao humu! Asanteni sana. In short wakati najiandaa kukuona kama nilivyokuwa nimeahdi kuna jamaa yangu mmoja alinipa wazo kwamba nicheki fuel system inaweza ikawa na matatizo hasa kama gari limekaa muda mrefu ikishindikana ndio suala la control box lifuate.

Ni kweli, kwanza, petrol pump haikuwa nzima sana; petrol filter ilikuwa chafu sana; nozel 3 hazikuwa na uhai wa kutosha. Kilichofanyika ni kubadili pump, kusafisha filter, na kubadili nozel. Gari imetulia ajabu na kasi yake sio ya kitoto.

Asanteni wadau.
 
Back
Top Bottom