Ray C ametumbukia upya kwenye janga la matumizi ya dawa za kulevya


Methadone yenyewe ni dawa ya kulevya, kinachofanyika ni kwamba yenyewe ina effect ndogo kulinganisha na zile zinazotumika kama vile cocaine au heroin, pia watumiaji ni rahisi kupunguziwa dozi taratibu bila kupata madhara makubwa ambayo ni hatari kwa maisha yao.

Hivyo wanakwenda kwa utaratibu huu mpaka wanaacha kabisa. Hivyo methadone huwapa watumiaji utamu uleule kama wanaoupata kwenye heroin au cocaine ili kuwafanya wasahau heroin au cocaine, baada ya hapo wanapunguziwa dozi kwa urahisi zaidi bila madhara makubwa.

Fahamu kwamba mtumiaji 'chronic'/ sugu wa dawa za kulevya akiacha ghafla anakufa, hivyo methadone ndio mojawapo ya suluhisho la kuziacha dawa hizi taratibu.

Wanachofanikiwa watumiaji ni kuacha kutumia heroin au cocaine bila kupata madhara ambayo ni hatari kwa maisha yao, lakini huwa bado wanakuwa na hamu ya kuendelea kutumia ingawa si kubwa kama ile ya mwanzo kwa kuwa bado wana 'traces'/ mabaki za dawa kwenye damu zao, hapa ndipo nidhamu inapohitajika.
 
Haya matatizo yangepungua sana kama wange ruhusu bange. nimesikiliza vijihotuba vya hao wanasiasa wenu sioni hata mmoja anaezungumzia mmea mtakatifu.....

Mkuu,ni watu wachache sana wanaojua ukweli kuhusu mmea huu,watu wengi wanaishi kama ng'ombe kwa kufuata kila wanachoambiwa bila kuhoji kama vile;

-Kuruhusu bangi katika baadhi ya maeneo na kukataza kwa maeneo mengine lakini wakati huohuo wanasema bangi ni haramu.

-Kuruhusu sigara/tumbaku na kukataza bangi lakini wakati huohuo wanatangaza kwamba matumizi sigara/tumbaku ni hatari kwa maisha.(taarifa za mpaka sasa zinaonesha bangi haijawahi kusababisha kifo hata kimoja,tumbaku husababisha vifo vingi sana kwa mwaka),lakini watu hawajui hili.

-Wanakataza watu wasilime bangi lakini wakati huohuo wanajua kwamba bangi ina uwezo wa kutibu cancer.

-Wanakataza bangi lakini wakati huohuo wanajua kwamba kenye heka moja ya bangi unapata zaidi ya lita 3500 za diesel ya kuendeshea mitambo ya viwandani,magari na mashine nyingine.

-Wanakataza bangi lakini wakati huohuo wanajua kwamba kwa kutumia bangi tunaweza kutengeneza karatasi zenye ubora mkubwa zaidi ya hizi za sasa.

Wanajua kwamba kuna matumizi zaidi ya 100 muhimu yanayotokana na bangi.Bangi ni hatari kwa biashara za wakubwa hasa mafuta na viwanda vya madawa.Watu wasiojua wanaishi kama mazuzu kwa kufuata sheria zilizowekwa na walafi wakubwa,watu hawana uwezo wa kuhoji wanakubali kila kitu kinachosemwa na wakubwa hawa.

Wakubwa hawa wanatunga sheria chafu na kuzipeleka/enforce UNO ili zitumike kwa mataifa mengine kama vile Tanzania nk.Na sisi tunapokea na kuzimeza kama kinda la ndege linavyokinga chakula kutoka kwa mdomo wa mama yake bila kujali kama anapewa sumu au la.

Kwa kweli inauma sana kuona karibu kila jambo muhimu kwenye dunia hii ni feki.Vita karibu zote ni feki,magonjwa mengi ni feki,kilimo kina mbegu feki,matumizi ya pesa nayo ni feki,vyakula ni feki,serikali ni feki,sheria ni feki,madawa ya hospitali ni feki,tafiti nyingi ni feki,Demokrasia ni feki,habari zinazotangazwa nazo ni feki,UNO ni feki,AU ni feki,UAE ni feki,uharamu wa bangi ni feki.Tuna kazi kubwa ya kubadilisha dunia hii.
 
Mkuu deception, inaonekana kwako wewe 90% ya mambo yanayofanyika/ kutokea duniani kwako ni illusion maana una feki nyingi sana naogopa usije ukasema hata binadamu nae ni feki hahaaa!!!
 
Kwa macho yangu ya nyama nimeshuhudia Ray c akinyimwa dawa pale mwananyamala naye akiwa analalamika anaumia kwanini anyimwe dawa.hii ndiyo tz hata amri ya rais inapuuzwa.
 
mi nafikiri badala ya kuhangaika na ray c tuhangaike na tatizo hilo kwa ujumla kwani kuna waathirika wengi sana ambao wameleta madhara kwenye jamii ray c ni tone tu haina maana tukahangaika naye kwa nguvu kubwa huku tukiacha wengine wakiangamia

Ni kweli mkuu hebu tuliangalie tatizo generally.
 
Madawa ni tatizo kubwa inafaa asaidiwe nina Mtoto katumbukia kwenye hiyo kitu, alikua anasoma Mlimani mwaka wa 3 sheria akatumbukia huko dadake ni Hakimu lakini tumeshindwa hili ni Janga tusaidiane

Mkuu, pole sana kwa janga lililokuta nyumba yako. Jaribu kuwa naye karibu sana, kama inawezekana na kumueleza madhara ya hii kitu. Pia kumsaidia kupitia watumishi wa Mungu. Jaribu kutafuta watu walioacha kabisa umkutanishe nao aone kuwa inawezekana kuacha. Hata kama ni walio nje ya nchi unaweza kupata taarifa zao kwenye internet.

Nadhani inabidi tuanze kuongea na watoto tangu wakiwa wadogo juu ya madhara ya haya madawa. Sio kusubiri mpaka mtoto ameathirika maana akianza hautajua. Hili tatizo hata uwe na elimu au pesa kiasi gani, ukiwa teja unakuwa useless kabisa.

Hii thread inasikitisha kweli. Na hali ya jamii yetu ni mbaya.
 
Kuna lodge flan mwananyamala inaitwa kifaru hua anachukua chumba na kujidunga na kupumzika hapo

Na Hapo Mwananyamala Si Ndiyo Makao Makuu Ya Hiyo Kitu Kwa Hapa Nchini Tanzania?
 
Na Hapo Mwananyamala Si Ndiyo Makao Makuu Ya Hiyo Kitu Kwa Hapa Nchini Tanzania?

Pale kino mkuu ndo headquarter aisee alaf nje nje tu nashangaa nyie watu wa kitengo hamfuatilii au ndo bangusilo ionekane serikali kimeo
 
Pale kino mkuu ndo headquarter aisee alaf nje nje tu nashangaa nyie watu wa kitengo hamfuatilii au ndo bangusilo ionekane serikali kimeo

Wenye Hicho Kitengo Chao Uliowataja Wamekusikia Mkuu Kwani Mimi Ni MJASIRIAMALI Tu Nisiye Na Mbele Wala Nyuma Na Isitoshe Sipo Huko Kwenu Tanzania Sasa Ni Mwaka Wa 7 Na Nipo Kwetu Huku Rwanda Ila Nakumbuka Tu Baadhi Ya Sehemu Na Maeneo.
 
Alikua anapenda sana wanaume masela! Kuanzia Majani, Mwisho hadi yule mla unga wa arusha!! Mwenyewe aliona sifa... hilo ni tatizo lake, haiwezekani mtu mmoja asaidiwe na kila mtu hadi rais wa nchi na bado tu habadiliki???...tuachane nae sikio la kufa hilo
 
Kama MTU anaambiwa hasikii were utamsaidia mini mwache kwani hawaoni witney na mwanae au yanaitaji
 
Source of information? Au unaeneza majungu tu. Ulimkuta wapi?
 
Mkuu deception inaonekana kwako wewe 90% ya mambo yanayofanyika/kutokea duniani kwako ni illusion maana una feki nyingi sana naogopa usije ukasema hata binadamu nae ni feki hahaaa!!!

Ha ha haaa,ni kwamba 'common denominator' ya mambo haya yote ni pesa/money.Pesa yenyewe ni dhana feki kwa kuwa imeanzishwa kwa misingi feki na matumizi yake pia ukichunguza vizuri utagundua kuwa ni feki.Hakuna mantiki/'logic' yoyote inayofanya pesa ishuke au ipande thamani,mambo haya tuliyofundishwa mashuleni kwamba ndio yanafanya pesa ipande au ishuke thamani ni feki tu,wakubwa wa dunia hii wamekaa chini na kuweka kanuni za hisabati ili pesa ifuate kanuni hizo kwa malengo yao binafsi.Tunachokiona sisi ni kiini macho/'illusion' tu.

Sasa kwa kuwa pesa ndio mhimili wa kila kitu katika dunia yetu,ndio maana leo hii kila kitu hakiendi sawa kwa kuwa kila kitu kinategemea pesa kama 'common denominator';

-Madaktari wanaharibu misingi ya afya
-Wanasheria wanaharibu misingi ya haki
-Vyuo vikuu vinaharibu elimu
-Serikali zinaharibu misingi ya haki na usawa
-Vyombo vya habari vinaharibu taarifa
-Dini zinaharibu misingi ya kiroho

na mengine mengi.

Maisha tunayoishi sasa sio halisi,ni 'pre defined' na sheria ambazo misingi yake ni pesa.Chunguza sana utaona kwamba jinsi unavyoishi si vile ungependa wewe uishi.

Chukulia kama tutaweza kuindoa pesa kwenye 'loop' ya maisha yetu na kuweka rasilimali kama mbadala wake.'We don't need money,we need resources(food,water,education,good healthy,shelter,clothes etc),and we can get all these without money'.
 
Deception

Nimekusoma mkuu ila sijui unazungumzia wakuu wa duniawa kipindi gani au karne ipi...kwa mtazamo wangu ni kweli uwepo wa pesa umefanya maisha yasiwe halisi na siku zinavyozidi kwenda uhalisia wa maisha ndio unapopotea lakini kwa nionavyo mimi ni kama dhana hii ya pesa imetokea mbali sana kihistoria kulingana na mafundisho ya dini (christian ninayoijua mimi) kiasi kwamba kinachotokea sasa hivi ni muendelezo tu na hakuna dalili yoyote ya kupotea au kupata mbadala wake...

Huoni kama kuna namna nyingine ya kufikiria ili kuchukulia mambo kwa mtazamo mwengine!? Kwa maana tukisema tukomae na dhana feki ya pesa (ambayo hatuwezi kuizuia kuendelea ku dominate milele yote) kua chanzo cha mambo mengi ambayo ni illusion ni kupoteza muda badala yake tugeuke na tufikirie ni JINSI GANI ya kuondoka katika huu ujinga wa kuendeshwa na hizi illusions..mkuu Deception sijui kama umenielewa....

Kuwaambia watu kitu flani ni illusion bila kumuelewesha "atatokaje" katika hilo giza ni kumpa mzigo ambao hatoweza kuubeba, kama mtu amekaa na dhana zaidi ya miaka 40 then wewe siku moja tu umwambie hiyo dhana ni kiini macho bila kumwonyesha upande wa pili ya shilingi ni kumuonea tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…