Ray C kutikisa tena anga la Bongo

Ray C kutikisa tena anga la Bongo

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906
Msanii wa kike aliyewahi kutikisa kupitia muziki wake kwa ufundi wa kukata viuno akiwa stejini mwanadada Ray C yuko mbioni kurudi tena kwenye game na tayari ameshafanya ngoma tano na zinatarajiwa kuachiwa hivi karibuni.
RAY%20CCCCCC_0.jpg

Ray C

eNewz imezungumza na msemaji wa Wanene Entertainment Gentriez ambapo kwa sasa ndiyo sehemu ambayo Ray C anatengenezea ngoma zake na amefunguka kuhusu maendeleo ya Ray C kimuziki na kusema kuwa kwa sasa maendeleo yake ni mazuri sana na tayari wameweza kutengeneza nyimbo tano za msanii huyo.

“Maendeleo ni mazuri na sasa hivi Ray C tayari ameshatengeneza ngoma nne kama siyo tano ambazo tayari zimekamilika tunasubiri tu ziingie sokoni , baada ya Songa atafata Damian Soul halafu ndio atafuata Ray C”

Wanene Entertainment wameweza kumsaini Damian Soul na wamesema kuwa bado kuna wasanii wengine watafuata akiwemo msanii kutoka Kenya ambapo wamedai kuwa bado wako kwenye mazungumzo.

Chanzo: EATV
 
Ataishia kujitikisa mwenyewe kama kawaida yake.
 


Msanii Ray C anatarajia kuingia tena kwa kishindo kwenye muziki na sasa amesharekodi nyimbo 5, nyimbo hizo zitafanyiwa video kisha kuwa released, kwa sasa anasimamiwa na Wanene Ent.
 
Karibu!
Muziki umebadirika sana,changamoto ni kubwa mno-Muziki wa sasa umebaki full shangwe, Kaya,Pombe +Ngono elimu ni kiduchu sana.

Ulifanya/Mlifanya Makubwa sana dada yangu katika nyakati zenu.

"Mahaba ya dhati yamenishukia"
 
Back
Top Bottom