Ray Kigosi awatolea povu watanzania, kisa unafiki wao

[emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Kweli house girls wanawajuwa sana hawa supastaa wa Bongo movies. Kigosi asifananishe supastaa wa Bongo flavor na wao. The latter wapo juu. Kweli nachukia bongo movies. Too cheap and out of stds. Ukitaka kupandisha hasira, angalia bongo movie.
 
Siku zote ukwel unapigwa pingu ili uongo uzid enea
Binadam hawana mana
 
Kitu ambacho Ray kashindwa kukijua ni kwamba mwenzao alikuwa na mafanikio yalopelekea kuhisiwa hivyo sababu ya kutoa kazi nzuri. Yeye na wenzake wanatoa kazi mbaya ndiyo maana hawapati mafanikio hivyo kushindwa kuhusishwa hata na ndumba za Babu wa Bagamoyo achilia.mbali Freemason
 
Ray unakumbuka bifu yako na Kanumba? Hadi wazazi wakahusishwa? hadi uchawi ukahusishwa? Kama ni unafiki na wewe umo. Sasa umetolea mifano ya Kanumba na Diamond! Kanumba aliitwa freemason kwa vile movies zake zilinoga, Diamond pia muziki wake unapendwa ndio maana...Nyie bongo movies si mjitahidi basi muwe Freemasons movies zenu zipendwe na wabongo? Toeni kazi nzuri mtauza tu sio mlete kazi mbovu halafu uje ulielie eti usisemwe. Usisemwe we nani? Hata Mwanamziki Mr Ebbo(RIP) tulimsema vibaya kwa kusimamisha basi kuulizia saa ngapi, japo tulikasirika lakini tukanunua kazi yake.
 
Achana na makala. Bongo movie chenga. Limebaki jina. Hakuna anayeangalia uchafu huo sasa.
Kaangalie mwenyewe kazi zako
 
To be honesty sijawahi kuwa na wivu wa kijinga kupinga madai ya mtu yeyote yule maana ni haki ya kila mtu kikatiba na anao uhuru wa kuandamana kudai haki yake anayoamini anastahili kuipata.
LAKINI SASA kwa mara ya kwanza najitokeza kupinga HAKI YA WANA BONGO MUVI KUDAI HAKI YAO YA KUZUILIWA MOVIE ZA KIGENI KUINGIZWA NCHINI ILI TUU WATANZANIA WOOOOTE TUANGALIE MUVI WANAZOTENGENEZA WAO ..
madai yao ni ya kijuha na hayamithiliki hata kumwadithia mtoto mdogo maana anaweza kukushangaa na kukudharau milele daima.
Nathamini jitihada za bongo movie ila bado ni kiduchu sana kufikia hatua ya kutaka WATANZANIA WOOOTE MIL 50 TUKOSE UHONDO WA MUVI ZA KIGENI TURUDI KWENYE UJIMA NA KUANGALIA MUVI ZAO ZINAZOANZA KUTAMBAA ILIHALI ZA KIGENI ZINAKIMBIA KWA SPEED HE USAIN BOLT.

MIZIZI YA MUVI ZA KIGENI IMEMEA MIOYONI NA KATIKA MAISHA YETU YA KILA SIKU KIASI KWAMBA ITAKUWA NGUMU KWENDA DUKANI KWA MPEMBA AU MANGI KUMWAMBIA NIGEE MFUKO WA RAY KIGOSI WE MIA 5 NA SIO TENA MFUKO WE RAMBO.
.....Tanzania tuna mifuko ya RAMBO na sio mifuko ya RAY KIGOSI.....na haikuitwa hivyo kwa bahati mbaya.

Jipangeni bongo muvi acheni ujuha na utoto usio na tija .
 
Upumbavu wa Insta ni vizuri ukabaki hkohko.....
Hah hahaha huu ndio unafiki tunaousema, Akitokea mange kaandikia kutokea insta muna mquote na kuifanya hoja ya msingi, wengine wakileta munaita ujinga duh!
 
Anzisha uzi badala ya kutumia uzi wa bongo movie kutoa yanayokubana moyoni.
 
ray alikupiga kibuti nini naona unaongea kwa chuki sana
 
Wanachokifanya bongo movie hivi sasa siungi mkono ila alichokisema Ray kuhusu unafki wa watu kwa Kanumba ni kweli,Binafsi naona bongo movie ndiyo ileile Kanumba hakuwa na chochote tofauti na wenzie ni unafki wetu.
 
Aliyosema ni kweli lakini bongo movie mh mh hamna haifai. Kwa upande mwingine wasanii wanaofanya vizuri wanapitia mengi mpaka kufikia mafanikio.Wanapita pengi na vitendo vyao vinaashiria mengi ndio maana wanafikiwa kuhisiwa wako freemason.Unakuta msanii anakuwa na urafiki na mwanachama anaehusika na Freemason huku wote wakionyesha ishara zilizo ktk alama zinazotumika Freemason pengine kwa kujua Ama kutokujua.Lady JD na mafanikio yake hajawahi kuhusishwa na watu hao kwa kuwa hana Uhusiano na wanachama hao.Juzi sijui msanii nani,harmorapa alijiita mwanamke shupavu kwa kingereza bila kujua sasa akipondwa Hajui lugha hiyo ni uwongo?.Kanumba alijizolea umaarufu kwenye maigizo kiasi kwamba hata alipoanza filamu alibaki na umaarufu japo baadhi ya filamu zake zilikuwa na makosa na makosa hayo na vile alivyokuwa anaenda yangeisha
 
1. Ray angenyamaza tu hata yeye alikua hampendi Kanumba ilo linajulikana wazi.

2. Naona kamtolea mfano Mondi ili mashabiki wa mondi tumsupport aongeacho...kwa hili kafeli

3. Ray sio muigizaji mzuri ni bora awe director..ila sababu anapenda kuuza sura ndiyo maana anataka aigize aonekane.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…