Ray Kigosi awatolea povu watanzania, kisa unafiki wao

Ray Kigosi awatolea povu watanzania, kisa unafiki wao

halafu wewe ray mambo yakujiita the greatest uache!!
we ujiite the greatest kwa muvi gani hasa? au huko kusema neno pumbaaavuu kila movi.
kama wewe the greatest sasa akina denzel au kiefer sutherland a.k.a jack buer wajiitaje? maana hawa muvi zao zapendwa dunia nzima wakati ww hata hapo Uganda Hawakutambui
[emoji3] [emoji3] [emoji3]
 
Kweli house girls wanawajuwa sana hawa supastaa wa Bongo movies. Kigosi asifananishe supastaa wa Bongo flavor na wao. The latter wapo juu. Kweli nachukia bongo movies. Too cheap and out of stds. Ukitaka kupandisha hasira, angalia bongo movie.
 
Siku zote ukwel unapigwa pingu ili uongo uzid enea
Binadam hawana mana
 
Kitu ambacho Ray kashindwa kukijua ni kwamba mwenzao alikuwa na mafanikio yalopelekea kuhisiwa hivyo sababu ya kutoa kazi nzuri. Yeye na wenzake wanatoa kazi mbaya ndiyo maana hawapati mafanikio hivyo kushindwa kuhusishwa hata na ndumba za Babu wa Bagamoyo achilia.mbali Freemason
 
Ray unakumbuka bifu yako na Kanumba? Hadi wazazi wakahusishwa? hadi uchawi ukahusishwa? Kama ni unafiki na wewe umo. Sasa umetolea mifano ya Kanumba na Diamond! Kanumba aliitwa freemason kwa vile movies zake zilinoga, Diamond pia muziki wake unapendwa ndio maana...Nyie bongo movies si mjitahidi basi muwe Freemasons movies zenu zipendwe na wabongo? Toeni kazi nzuri mtauza tu sio mlete kazi mbovu halafu uje ulielie eti usisemwe. Usisemwe we nani? Hata Mwanamziki Mr Ebbo(RIP) tulimsema vibaya kwa kusimamisha basi kuulizia saa ngapi, japo tulikasirika lakini tukanunua kazi yake.
 
Kupitia ukurasa wake wa Instagram Ray ametoa
ujumbe ambao unalenga kutoa uelewa kwa
mashabiki hasa wa filamu na muziki nchini
ambao wamekuwa wakiponda juhudi za mastaa wa Kitanzania
Huku akitolea mfano wa Kanumba na Diamond platnumz

Ray Kigosi ameandika…
1. Kanumba alipoanza kuona mwanga wa
kufanikiwa bila kujali juhudi zake kuna watu
walimuita Freemanson, Mara anatumia nguvu za
Giza. that is to say films zake hazikuwa nzuri
but ziliuza sababu ya nguvu za Freemanson na
nguvu za giza!!
2. Kanumba alipoenda Big Brother alipondwa
Sana na kuitwa bogus kwa Madai hajui
kiingereza, Ni watanzania Hawa Hawa
walibebea bango hili huku baadhi ya waandishi
uchwara wakieneza ujinga huu bila kujali juhudi
zake. But Leo wanamsifia hakuna Kama
Kanumba!
3. Kuna wakati Kanumba alionekana wazi
kuvunjwa moyo na kukatishwa tamaa kwa
kuonekana juhudi zake si kitu. But Alisema
maneno machache Kuwa mtanikumbuka kama si
Leo basi Ni Kesho.
And alichosema kimetimia, wale wale
waliokuwa wakisema Ni Freemanson bila hata
kujali juhudi zake kwenye game Leo ndio kwa
unafiki wanasema hakuna Kama Kanumba !…..
HAO NDIO BINADAMU NA TABIA ZAO
Je Kanumba kaondoka na Bongo Movie yake ya
Freemanson ? Kama wengine mnavyodhani
industry Ni Mtu sio system !
4. Diamond Platnumz nae baada ya kuona Njia
ya mafanikio kuna watanzania, wasanii
wenzake na hata baadhi ya wanahabari
wanasema Ni Freemanson, wengine
wanaonyesha chuki ya wazi kwake. Wanasema
Hana muziki mzuri, Mara Ni Kiki tu ambazo
hata Kanumba alikuwa akiripotiwa magazetini
na kina Wema.
Hawaoni juhudi na thamani ya Diamond sasa !
Hatuombi baya limpate Diamond ili kudhibitisha
tabia na unafiki wa binadamu. But HAO NDIO
BINADAMU siku zote hawana Jema unafiki ni
sehemu ya Maisha.
5. kila siku Ni kuzua hii na kile, Mara ooh
Diamond Ni mchawi, kasema mleteni huyo
mganga wangu mkashindwa kumleta,
akajitokeza mganga fake sijui na Madai juu
Kuwa Diamond atashuka kimuziki kwa sababu
ananipuuza niliyempa nyota, Diamond akasema
sawa namtegemea Mungu. Miaka 4 sasa tangu
yaliyoitwa ya mganga Diamond hashuki ndio
anazidi kupaa. HAO NDIO BINADAMU kusema
lolote Ni haki Yao.
Kazi za Kanumba sasa zinapewa thamani na
ubora uliovuka mipaka na viwango ambao
hakupewa kipindi yupo hai ! HAO NDIO
BINADAMU na tabia zao. Ni tabia tu ya baadhi
ya watu kubebea mabango mabaya ya Mtu au
uzushi na kuacha mazuri yake then baadaye
wakishikwa Uchawi wanageuza walichoamini Ni
nyeusi kiwe nye.
View attachment 501515
View attachment 501518
Achana na makala. Bongo movie chenga. Limebaki jina. Hakuna anayeangalia uchafu huo sasa.
Kaangalie mwenyewe kazi zako
 
To be honesty sijawahi kuwa na wivu wa kijinga kupinga madai ya mtu yeyote yule maana ni haki ya kila mtu kikatiba na anao uhuru wa kuandamana kudai haki yake anayoamini anastahili kuipata.
LAKINI SASA kwa mara ya kwanza najitokeza kupinga HAKI YA WANA BONGO MUVI KUDAI HAKI YAO YA KUZUILIWA MOVIE ZA KIGENI KUINGIZWA NCHINI ILI TUU WATANZANIA WOOOOTE TUANGALIE MUVI WANAZOTENGENEZA WAO ..
madai yao ni ya kijuha na hayamithiliki hata kumwadithia mtoto mdogo maana anaweza kukushangaa na kukudharau milele daima.
Nathamini jitihada za bongo movie ila bado ni kiduchu sana kufikia hatua ya kutaka WATANZANIA WOOOTE MIL 50 TUKOSE UHONDO WA MUVI ZA KIGENI TURUDI KWENYE UJIMA NA KUANGALIA MUVI ZAO ZINAZOANZA KUTAMBAA ILIHALI ZA KIGENI ZINAKIMBIA KWA SPEED HE USAIN BOLT.

MIZIZI YA MUVI ZA KIGENI IMEMEA MIOYONI NA KATIKA MAISHA YETU YA KILA SIKU KIASI KWAMBA ITAKUWA NGUMU KWENDA DUKANI KWA MPEMBA AU MANGI KUMWAMBIA NIGEE MFUKO WA RAY KIGOSI WE MIA 5 NA SIO TENA MFUKO WE RAMBO.
.....Tanzania tuna mifuko ya RAMBO na sio mifuko ya RAY KIGOSI.....na haikuitwa hivyo kwa bahati mbaya.

Jipangeni bongo muvi acheni ujuha na utoto usio na tija .
 
Upumbavu wa Insta ni vizuri ukabaki hkohko.....
Hah hahaha huu ndio unafiki tunaousema, Akitokea mange kaandikia kutokea insta muna mquote na kuifanya hoja ya msingi, wengine wakileta munaita ujinga duh!
 
Huhitaji kumfahamu ni nani bali ujumbe wa kweli umefika japo simfahamu na siangalii movie zake lakini alichokisema ni cha kweli. Mimi nitaenda mbali hata Lowasa tulimuita FISADI lakini baadhi yetu wanamuona LOWASA yuleyule ambaye hajafanya lolote lile la kujisafisha na huo uliosemwa UFISADI leo tunasema ni rais wa mioyo....Na hata Magufuli tunayemsema hajui kiingereza akimaliza muda wake tutamshangilia pia hapo ndipo ubaya wa TAIFA lilojaa wanafiki kila kona utakapoliona...........
Anzisha uzi badala ya kutumia uzi wa bongo movie kutoa yanayokubana moyoni.
 
halafu wewe ray mambo yakujiita the greatest uache!!
we ujiite the greatest kwa muvi gani hasa? au huko kusema neno pumbaaavuu kila movi.
kama wewe the greatest sasa akina denzel au kiefer sutherland a.k.a jack buer wajiitaje? maana hawa muvi zao zapendwa dunia nzima wakati ww hata hapo Uganda Hawakutambui
ray alikupiga kibuti nini naona unaongea kwa chuki sana
 
Wanachokifanya bongo movie hivi sasa siungi mkono ila alichokisema Ray kuhusu unafki wa watu kwa Kanumba ni kweli,Binafsi naona bongo movie ndiyo ileile Kanumba hakuwa na chochote tofauti na wenzie ni unafki wetu.
 
Kweli kabisa ley, hata juzi tuliona baadhi ya wabunge waliokuwa wakimponda kikwete wakimshangilia bungeni na kutamka tumekumiss, lkn ndo waliosema serikari ya jk legelege,dhaifu,wa nataka rais wakuinyoosha nchi, Nikweli binadam mmoja ana roho saba. Bongo move simamieni na kudai haki yenu kwani haki haiombwi ila hudaiwa.
Aliyosema ni kweli lakini bongo movie mh mh hamna haifai. Kwa upande mwingine wasanii wanaofanya vizuri wanapitia mengi mpaka kufikia mafanikio.Wanapita pengi na vitendo vyao vinaashiria mengi ndio maana wanafikiwa kuhisiwa wako freemason.Unakuta msanii anakuwa na urafiki na mwanachama anaehusika na Freemason huku wote wakionyesha ishara zilizo ktk alama zinazotumika Freemason pengine kwa kujua Ama kutokujua.Lady JD na mafanikio yake hajawahi kuhusishwa na watu hao kwa kuwa hana Uhusiano na wanachama hao.Juzi sijui msanii nani,harmorapa alijiita mwanamke shupavu kwa kingereza bila kujua sasa akipondwa Hajui lugha hiyo ni uwongo?.Kanumba alijizolea umaarufu kwenye maigizo kiasi kwamba hata alipoanza filamu alibaki na umaarufu japo baadhi ya filamu zake zilikuwa na makosa na makosa hayo na vile alivyokuwa anaenda yangeisha
 
1. Ray angenyamaza tu hata yeye alikua hampendi Kanumba ilo linajulikana wazi.

2. Naona kamtolea mfano Mondi ili mashabiki wa mondi tumsupport aongeacho...kwa hili kafeli

3. Ray sio muigizaji mzuri ni bora awe director..ila sababu anapenda kuuza sura ndiyo maana anataka aigize aonekane.
 
Back
Top Bottom