Baada ya kufatilia hili sakata linaloendelea kati ya Harmonize (KondeGang) na Rayvany (Wasafi) maoni yangu ni kwamba Wasafi wameshinda hii battle ingawa kwa jicho la kawaida unaweza usigundue.
Nachoona hapa Wasafi lengo lao Kubwa ni kuihamisha hii bifu ya Harmonize dhidi ya Diamond, na kuipeleka kwa Harmonize dhidi ya Rayvany kwakuwa waliona Diamond hanufaiki na bifu hilo, ila kwa Rayvanny itamsaidia kukua zaidi huku Harmonize akibaki palepale au kushuka.
Kitendo cha Harmonize kushindanishwa na wasanii wakubwa kama Diamond au hata Kiba kilikuwa kinamuweka pazuri zaidi kuliko hivi ambavyo anashindana na Rayvanny mtu ambaye hata yeye anaamini anamzidi 'ukubwa'.
Nimeona kwenye interview Rayvanny anazungumzia kuhusu kumzidi Harmonize subscription, views na online sales; hakika hivyo hajavisema kwa bahati mbaya, hii ishu iko planned kabisa na management, na Diamond kajikausha kama hausiki ila usikute ndio masterplan wa mchezo mzima.
Inshort walijua kile kitendo cha Ray kurelease video yake na Paula ni lazima konde atajichanganya tu, na kweli ikawa hivyo. Sasa usishangae kutoona mashabiki wakimlinganisha Harmonize na Diamond, utaona wanamlinganisha na Rayvanny huku Diamond yuko bts anakula popcorn tu[emoji16]