Mafyangula
JF-Expert Member
- Jan 16, 2025
- 557
- 1,039
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima, amewahakikishia wananchi wa mkoa huo kuwa hali ya ulinzi na usalama imeimarishwa kikamilifu kuelekea Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika kesho, Oktoba 29, 2025.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Oktoba 28, 2025, Malima amesema kuwa hakuna taarifa zozote za vitendo vya uvunjifu wa amani katika mkoa huo, na kusisitiza kuwa vyombo vya dola viko tayari kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa utulivu na usalama wa hali ya juu.