RC Albert Chalamila: Dar kila mtu anataka kumiliki ardhi. Hayo ni mawazo ya kishamba, uzieni watu nyumba sio ardhi!

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Watu wa Dar mko wapi?

Akizungumza hivi karibuni, Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam, Albert Chalamila amezungumzia namna ambavyo watu wengi wa Dar wanapenda na kutaka kumiliki ardhi.

Chalamila amesema kuwa kiuhalisia sio kila mtu anaweza kumiliki ardhi na badala yake kuwe na utaratibu wa watu kumiliki nyumba ambazo zimejengwa na mashirika ya umma.

Chalamila ametolea mfano kuwa kuna watu ambao wanafanya kazi Ilala lakini wanaishi Mlandizi. Amesema kuwa hayo ni mateso na kwamba ufike muda kuwe na utaratibu wa watu kuuziwa nyumba na mamlaka husika na sio viwanja.

======

Hivi Chalamila anajua bei ya nyumba za National Housing au anaongea tu kisa yeye anaishi nyumba ya bure Mikocheni, so anahisi kila mtu anaweza ku-afford?

Kama kungekuwa na nyumba za bei rahisi huko Ilala nani angeenda kukaa Bunju huko?

===============================================================

Hivi Chalamila anajua bei ya nyumba za National Housing au anaongea tu kisa yeye anaishi nyumba ya bure Mikocheni, so anahisi kila mtu anaweza ku-afford?

Kama kungekuwa na nyumba za bei rahisi huko Ilala nani angeenda kukaa Bunju huko?

View attachment 3187602
yeye ameshindwa kujaijiri anakula uchawa kwa samia halafu analeta kiherehere
 
Ana point ya msingi mashirika yajenge nyumba na yauze kwa mfumo wa MORTGAGE hii inasaidia kupata mji uliopangika vizuri na kupunguza slams na kero nyingine, Wazungu hawanunui viwanja wananunua nyumba ukiona mzungu, muhindi au mwarabu kanunua kiwanja ujue ni commercial sio residential
 
Wazo zuri. Japo mswahili nyumbani kwake ndiyo ofisini kwake, kuishi ghorofani hataweza.
 
Chalamila amesema kuwa kiuhalisia sio kila mtu anaweza kumiliki ardhi na badala yake kuwe na utaratibu wa watu kumiliki nyumba ambazo zimejengwa na mashirika ya umma.

Hizi habari akaongee kwenye vikao vyao vya chama, zinahusu zaidi sera za chama na serikali
 
Back
Top Bottom