RC Albert Chalamila: Gari lililobeba mitambo maalum liko njiani kwa ajili ya Uokoaji Kariakoo

Yaani chalamila aliwahi kufika kabla hata Greda halijafika,........sasa sijui alikuwa anawahi kufanya nini wakati vifaa havipo, yaani kwa dunia ya sasa tunashindwa kupata simple machine kwaajili ya rescue tunaanza kuchimba na chepe na mikono? Halafu mambo ya kijinga ndiyo tuna entertain,sijui goli la mama........kuna upuuzi mwingi sana nchi hii,hakuna taasisi iliyo active zote zimeoza
Tangu lini nchi hii kwenye suala la uhokoaji wakaweza,nchi ikitokea majanga hesabuni viliooo tu

Ova
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amesema tayari gari maalum lililobeba greda na mitambo mingine linakaribia kufika Kariakoo kwa ajili ya kusaidia uokoaji wa Watu waliofukiwa na kifusi baada ya ghorofa kuporomoka ambapo amewataka Watanzania kutolaumiana kwa sasa bali kuweka nguvu kwenye kuokoa waliofukiwa.

Pia, soma: Ghorofa limeporomoka Kariakoo asubuhi ya leo Novemba 16

"Kama kuna vifo tutaendelea kuhabarishana lakini hadi muda huu hali ya usalama katika eneo hili ni kubwa na niwaombe Wafanyabiashara wote pamoja na Ndugu na Jamaa ambao Rafiki na Ndugu zao wapo kwenye jengo hili tuendelee kuwa na subira, hadi sasa tumefanya jitihada za kuleta mitambo, mnafahamu greda hauwezi kupitisha barabarani lazima ubebe kwenye gari maalum la mitambo na hadi muda huu lipo karibu kuja kusaidia uokozi"

"Niombe sana tuendelee kuwa na usikivu na ustahimilivu na Mh. Rais ametoa pole kwa waliopata na majanga, nitoe rai kwamba muda huu sio muda wa kulaumiana, ni muda wa kuwakoa wenzetu, jengo hili lina underground tunaambiwa wapo Watu ndani, baada ya muda tutatoa taarifa sahihi wangapi wamepatikana chini na wakiwa na hali gani, Vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama na Viongozi tupo hapa, tusilaumiane kwanza hadi tafiti zikianza tubaini chanzo"
View attachment 3153644
Ghorofa limeanguka huyu mjinga anasema hali ya usalama ni kubwa?
 
Masaa yashapita zaidi ya manne alafu hapo ni kkoo kitovu Cha biashara nchi nzima, sasa huku mikoani si mtakuja baada ya wiki!!!

Haya sasa Wana kariakoo mkiwa dukani hakikisheni mna stock ya chakula na maji hata ya wiki maana nchi hii haieleweki lolote linaweza kutokea
Binadamu ukisha mu-hold masaa matano tu sehemu yenye hewa ndogo na joto linalozidi nyuzi 40 hesabu umempoteza unless kuwe na hewa huko chini. So sad kwa kweli !Mungu atusaidie sana imagine mimi nimekaa nakunywa beer kumbe kuna binadamu mwenzangu amenasa kwenye gorofa lililoanguka!?? Mungu baba tusamehe
 
Na Tanzania kukabiliana na majanga zerooo kabisa
Alafu ikifika Dec ngapi ile utawaona wanavyojitutumuaaa
Kwenye parade zao

Ova
 
Screenshot_20241116-162911.jpg
 
Masaa yashapita zaidi ya manne alafu hapo ni kkoo kitovu Cha biashara nchi nzima, sasa huku mikoani si mtakuja baada ya wiki!!!

Haya sasa Wana kariakoo mkiwa dukani hakikisheni mna stock ya chakula na maji hata ya wiki maana nchi hii haieleweki lolote linaweza kutokea
Katika hali ya dharura kama hii walipaswa wasafishe barabara inayoelekea hapo... Kuondoa foleni ya namna yoyote ile, kama na hiki pia hakikufanyika basi ni tatizo kubwa
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amesema tayari gari maalum lililobeba greda na mitambo mingine linakaribia kufika Kariakoo kwa ajili ya kusaidia uokoaji wa Watu waliofukiwa na kifusi baada ya ghorofa kuporomoka ambapo amewataka Watanzania kutolaumiana kwa sasa bali kuweka nguvu kwenye kuokoa waliofukiwa.

Pia, soma: Ghorofa limeporomoka Kariakoo asubuhi ya leo Novemba 16

"Kama kuna vifo tutaendelea kuhabarishana lakini hadi muda huu hali ya usalama katika eneo hili ni kubwa na niwaombe Wafanyabiashara wote pamoja na Ndugu na Jamaa ambao Rafiki na Ndugu zao wapo kwenye jengo hili tuendelee kuwa na subira, hadi sasa tumefanya jitihada za kuleta mitambo, mnafahamu greda hauwezi kupitisha barabarani lazima ubebe kwenye gari maalum la mitambo na hadi muda huu lipo karibu kuja kusaidia uokozi"

"Niombe sana tuendelee kuwa na usikivu na ustahimilivu na Mh. Rais ametoa pole kwa waliopata na majanga, nitoe rai kwamba muda huu sio muda wa kulaumiana, ni muda wa kuwakoa wenzetu, jengo hili lina underground tunaambiwa wapo Watu ndani, baada ya muda tutatoa taarifa sahihi wangapi wamepatikana chini na wakiwa na hali gani, Vyombo vyote vya Ulinzi na Usalama na Viongozi tupo hapa, tusilaumiane kwanza hadi tafiti zikianza tubaini chanzo"
View attachment 3153644
Baafa ya kuona Chadema hawahusiki akaona ni tukio la kawaida halihitaji haraka.
 
Back
Top Bottom