John John Msakuzi
JF-Expert Member
- Jun 17, 2025
- 296
- 103
Akiongea na Wanahabari, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anamringi Macha, amesema kuwa kupitia kampeni ya Kitaifa ya Samia Legal Aid, wananchi 177,114 (wanaume 80,000 na wanawake 97,114) wamepata elimu ya msaada wa kisheria ili kuongeza uelewa wa haki zao na taratibu za kisheria. Vilevile, watoa huduma 108 kutoka kata 108 kati ya 133 na wasaidizi 13 (wanaume 11, wanawake 2) wamepatiwa mafunzo maalum ya kuimarisha uwezo wa kutoa msaada wa kisheria katika ngazi za jamii.
Aidha, amesema kampeni hiyo imewezesha kutatuliwa migogoro ya ardhi 452 kwa njia ya amani na kupunguza mashauri yaliyohamishiwa kwa watoa huduma wengine kutoka 470 mwaka uliopita hadi 18 pekee, hatua inayoongeza ufanisi wa upatikanaji wa haki. Pia, mkoa umepata mashirika matano yasiyo ya kiserikali yanayotoa huduma za msaada wa kisheria katika kila wilaya, jambo linalosogeza huduma karibu na wananchi, kupunguza msongamano wa mashauri mahakamani, na kuimarisha hali ya ulinzi na usalama mkoani Simiyu.