PostGE2025 RC Anthony Mtaka awatoa hofu wananchi wa mkoa wa Njombe

PostGE2025 RC Anthony Mtaka awatoa hofu wananchi wa mkoa wa Njombe

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Mkuu wa Mkoa wa Njombe Anthony Mtaka amewataka wananchi wa Mkoa wa Njombe kuendelea na shughuli zao bila hofu yoyote

Ameyasema hayo Novemba 6,2025 wakati akizungumza na Wafanyabiashara wa Makambako Mkoa wa Njombe na kuwataka kuendelea na shughuli zao za kiuchumi bila hofu yoyote kwani vyombo vya Ulinzi na Usalama vinashirikiana vyema kuhakikisha amani inakuwepo wakati wote.

Pia, amewataka Wananchi wa Mkoa wa Njombe kutoa ushirikiano kwa vyombo vya Ulinzi na Usalama ili hatua zichukuliwe mapema kwa wale ambao Awana nia Njema.

Sambamba na hilo, amewahasa vijana kuacha kushabikia matendo maovu katika jamii ambayo yanaleta madhara na taharuki Wananchi na badala yake washirikiane na vyombo vya Ulinzi na Usalama katika kuimarisha ulinzi na amani wa Raia na Mali zao.
 
Matendo maovu makubwa zaidi ni wizi wa kura, hata yeye ni RC haramu aliyewekwa na watawala haramu walioporwa uchaguzi.
 
Back
Top Bottom