RC atoa namba yake kwa wananchi wampe taarifa wanapouziwa Sukari kwa bei ya juu (Kukamata Wauzaji)

Mjanja M1

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2018
Posts
4,058
Reaction score
14,382
Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Adam Malima, ametoa namba yake ya simu ya kiganjani kwa wananchi wa mkoa huo kwaajili ya kutoa taarifa au kutuma ujumbe mfupi pale wanapouziwa sukari kwa bei ya juu tofauti na bei elekezi ya sh 2700 hadi 3200 na wafanyabiashara ili waweze kukamatwa na kuchukuliwa hatua za kisheria.

Malima ametoa namba yake katika maadhimisho ya Kumbukizi ya miaka 47 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) iliyofanyika kimkoa katika Manispaa ya Morogoro.

Source - Nipashe
 
Hata DC Ametoa namba kule Sumbawanga ila wafanyabiashara wameficha sukari,imekuwa kama bangi
 
Wanazidi kuipeperusha,leo nimenunua sukari sh 7000kg 1
 
Wanaogoopa nini kuiweka hapa
 
KIZIMKAZI hajui chochote kuhusu sukari n umeme. watanganyika tuliambiwa mwishoni mwa January kule kwenye bwawa la umeme wangewasha geneleta Moja kwanza. Mpk sasa bilabila. Na KIZIMKAZI kasahau alisema nn?
 
Wanafanya maigizo
 
ningepewa nchi hii , wafanyabiashara wangekomaa
Shida ni kwamba ukiwawndea pupa wanakimbia utafanyaje? Kumbuka kabla ya Mwendazake sukari ilikuwa haisumbui ila alipoanzaga kuingilia soko ndio Hadi Leo hii haijawahi tengamaa Kwa sababu Sheria zilizopitishwa zimewapa viwanda ndio wawe wanaagiza badala ya wafanyabiashara
 
Tatizo limeelezwa kwamba mvua za kinyume na msimu zilijaza maji kwenye mashamba hivyo miwa imeshindwa kuvunwa ikizingatiwa pia Kila mwaka viwanda Huwa vinafanya Usafi miezi michache kabla ya mvua.
πŸ™πŸ™πŸ‘
 
Hivi sherehe za kuzaliwa CCM bado zipo? Aisee
 
Wanaujua ujinga wa watanzania, kwa ujinga wao watachukua namba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…