Mkulima na Mfugaji
JF-Expert Member
- Jul 26, 2013
- 1,057
- 1,868
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Paul Chacha amesitisha mkutano wa injili uliotarajiwa kuanza Machi 19 hadi Machi 22 mwaka huu na Mchungaji Dana Morey kutoka nchini Marekani, baada ya kubaini kuwepo kwa viashiria vinavyodaiwa kuhusishwa na mapenzi ya jinsia moja.
Akizungumza na waandishi wa habari, Chacha amesema kabla ya mkutano huo kulikuwa na kampeni iliyokuwa ikiambatana na mabango na vipeperushi vilivyobandikwa katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Tabora vikiwa na ujumbe unaosomeka “Maisha yako Mapya.”
Amesema sambamba na kampeni hiyo kulikuwa na ugawaji wa mipira katika taasisi mbalimbali za elimu pamoja na shule, ambapo taarifa zinaonyesha kuwa jumla ya shule 55 ziligawiwa mipira hiyo.
Mkuu huyo wa mkoa amesema baada ya uchunguzi kufanyika imebainika kuwa baadhi ya mipira hiyo pamoja na vipeperushi vilivyokuwa vikisambazwa vina alama za vidole zinazodaiwa kuwa na viashiria vinavyohusishwa na mapenzi ya jinsia moja.
Ameongeza kuwa tofauti na alama zinazotambulika katika imani ya Kikristo kama msalaba, lakini vipeperushi hivyo havikuwa na alama hiyo, bali vilikuwa na alama za vodole ambazo zimeibua maswali mengi.
Amesema nyuma ya vipeperushi hivyo kulikuwa na kadi maalum za kujaza taarifa, jambo lililoibua wasiwasi kuhusu madhumuni mahususi ya kampeni hiyo.
Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa Mkoa ameagiza mabango yote yaliyowekwa mitaani yaondolewe mara moja, huku mipira yote iliyogawiwa imeshakusanywa.
Pia amemtaka Mchungaji mwenyeji anayehusika na maandalizi ya mkutano huo, Mchungaji Rashid, kufika mbele ya kamati ya ulinzi na usalama kwa maelezo zaidi kuhusu shughuli hiyo.
Amefafanua kuwa kwa mujibu wa taratibu za nchi, hairuhusiwi kufanya shughuli za Uinjilisti ndani ya shule, kwa kuwa wanafunzi wapo chini ya uangalizi wa wazazi na walezi wao na kwamba misaada au zawadi zinazogawiwa kwa wananchi lazima ziwe wazi na zisizo na ujumbe au viashiria vinavyokwenda kinyume na maadili ya jamii.
Kutokana na sababu hizo, Mkuu wa mkoa wa Tabora ameagiza wahusika wote wa kampeni hiyo kuondoka mara moja mkoani Tabora.
================