Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaaam, Albert Chalamila amewataka Watanzania kuacha kuingiza siasa katika masuala muhimu hasa katika afya kwani hazitasaidia badala yake zitawachelewesha na kusababisha kuwa na madhara makubwa zaidi kwa Wananchi.
Amesema hayo leo January 26,2025 wakati akitoa ufafanuzi baada ya taarifa iliyotolewa na chombo kimoja cha habari kuhusu kauli yake aliyomwambia Mwananchi mmoja wa Temeke kuwa kama hana vifaa vya kujifungulia kwamba aende akajifungulie nyumbani ambapo RC Chalamila amesema taarifa hiyo imenukuliwa kimakosa na lengo lake yeye ni kuhamasisha Wananchi kuwekeza kwenye afya huku ikisaidiana na Serikali nchini ambapo amesisitiza clip nzima ya yote aliyoyasema ipo ofisi ya RC na kutaka Watu wasisambaze clip ambayo imekatwakatwa ili kupotosha.
RC Chalamila amesisitiza umuhimu wa Watanzania wote kuachana na kauli chonganishi akisema hii inaweza kuleta athari kubwa kwa Tanzania kwa sasa akisema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imewekeza fedha nyingi zaidi kwenye Sekta ya Afya ila pia muhimu kwa Wananchi kuwekeza kwenye masuala ya msingi na kuacha kuwekeza kwenye masuala yasiyofaa “Kuelekea uchaguzi upotoshaji ni mwingi”