RC Chalamila afafanua video inayo trend aliyosema "Kama hutaki kununua Gloves kajifungulie nyumbani"

RC Chalamila afafanua video inayo trend aliyosema "Kama hutaki kununua Gloves kajifungulie nyumbani"

Akizungumza na wanahabari siku ya leo, Chalamila amesema kuwa kauli yake dhidi ya wamama wajawazito waliokosa hela imetumika vibaya ukizingatia kwamba sasa tuko kipindi cha Uchaguzi,

Chalamila amesema kwamba kuna haja ya watu kuangalia clip nzima ya video hiyo kwani kuna upotoshaji mkubwa unaendelea kutokana na sehemu ndogo tu ya clip hiyo kusambazwa kwenye mitandao ya kijamii

Soma pia: RC Chalamila asema mjamzito anayegoma kununua gloves akajifungulie nyumbani. Hafai kuendelea kubaki madarakani


Naona anacheza tu na maneno na sio kauli yake ya kihuni.
 
Sasa kwanini upate pesa ya kuchezesha Ngoma ukose pesa ya kuchangia huduma ya kujifungua
Uliekuwa unamtetea baada ya kugundua kachemka anajaribu kujisafisha,wewe bado unapayuka tu.
 
Anapaswa kuangalia lugha anazutumia na kufikiria kwa kina kabla ya kuongea
 
  1. Kama huna nauli kwenda Kigamboni piga mbizi
  2. Watanzania watakula nyasi ili ndege ya Rais inunuliwe
  3. Kila mtu atauchukua mzigo wake
  4. Kama huna hela ya kuchangia huduma ya uzazi nenda kwa mumeo akuchane na mikasi
Hii tabia ya ropo ropo nchi za watu inaweza kugharimu kibarua cha mtu ila hapa kwetu ni kama kitu cha kawaida. Hata humu unakuta kuna habari sensitive anatoka mtu huko anakuja kuharisha uongo.
 
Nina mashaka Ile story sio ya kweli , maana hata hiyo hospital hajaitaja,,Ukute Rc Ile story kajitungia tu kichwani ili kufurahisha watu😁 ila kitamlamba vibaya kasahau huu ni muda wa kampen
 
Chalamila anajiona ufahamu tu hapo anaelewa kabisa kuwa walicholalamikia ni lugha yake ya kifedhuli kumwambia huyo mama mjamzito kuwa arudi nyumbani amwambie mumewe akanunue visu kwa ajili ya kumtoa mtoto aliyekuwa tumboni. Huyu hizo bangi anazovuta zinamfanya ajione nyati sana.
 
Mkuu wa mkoa wa DSM Mh Albert Chalamila amewataka waandishi wa Habari kutafsiri Kwa usahihi hotuba za Viongozi badala ya kuwawekea Maneno mdomoni

Chalamila amesema ni muhimu Watu wakaelewa kuna Huduma ya Afya Kwa gharama nafuu na kuna Huduma ya Afya Bure Kwa makundi maalumu na mara nyingi Vitu Vya Bure huisha mapema

Aidha Chalamila amesema Wakazi wa Temeke huwekeza zaidi Kwenye Ngoma zao za vigodoro na linapokuja swala la kuugua wanataka Watibiwe Bure kabisa, this is nonsense na Watu kama hawa huko mbele watastahili hata adhabu

Chalamila amesisitiza ni azma ya Serikali kuwapatia Wananchi Huduma ya Afya Kwa gharama nafuu ndio sababu Rais Samia ameleta Madaktari Bingwa wanaotoa Huduma za kitabibu Kwa gharama nafuu siyo Bure kabisa

Source: Ayo TV

Ahsanteni sana
 
Chalamila yupo sahihi,hatuwezi kubembelezana kweny Mambo kama hayo.
Mimba sio dharula,yaan miezi tisa yote unashindwa kuweka akiba hata ya 50k na wakati unajua badae gharama zitaitajika? Vichwa vya dar es salaam sio vya kubembelezana
 
Chalamila yupo sahihi,hatuwezi kubembelezana kweny Mambo kama hayo.
Mimba sio dharula,yaan miezi tisa yote unashindwa kuweka akiba hata ya 50k na wakati unajua badae gharama zitaitajika? Vichwa vya dar es salaam sio vya kubembelezana
Hivi Sera yenu na Ilani ya Uchaguzi inasemaje kuhusu huduma za kujifungua kwa mama wajawazito?
 
Back
Top Bottom