RC Chalamila ahoji kama Bandari imeuzwa mbona soko la Ferry bado lipo. Asema waliopotosha wote wako ndani na wataendelea kukamatwa wakiibuka wengine

RC Chalamila ahoji kama Bandari imeuzwa mbona soko la Ferry bado lipo. Asema waliopotosha wote wako ndani na wataendelea kukamatwa wakiibuka wengine

Chanzo ni East Africa Tv,
Akizungumza katika kipindi cha superbreakfast leo asubuhi ,Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Albert chalamila amesisitiza wote wanaopinga bandari watakamatwa na kuwekwa ndani na yeye mwenyewe ata dili na wote wanaopinga mmoja mmoja mpaka watakapoisha

Mpaka sasa amesisitiza wale vinara wameshawakamata na kuwaweka ndani

Unaweza pia ukafuatilia audio ya maelezo ya Albert chalamila kwenye page ya East Africa TV leo hii kuhusu wanaopinga bandari

Je yawezekana Albet Chalamila amepata mamlaka makuu kama Paul Makonda

Je uhamisho wa chalamila kuja Dar lengo ilikuwa afanye fujo na kuvunja sheria kama Paul Makonda

Ukamataji wa Dkt slaa na wengine ndiyo nguvu ya Albert chalamila sasa kuliendesha jeshi kama Paul Makonda?

Nini maoni yako kwa kauli hii ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam
View attachment 2718985
 
Asishangae tutamkata yeye one day
Mmmh,Hakuna episode mpya

Series za bandari hazijaisha tu au kila series mpya inabuma

Na hii series ya uhaini bado inataka kubuma tena

Kweli Director wa episode wa bandari kosa kubwa alimwacha steriling mpaka mwisho akitabasamu bila jereha

Majibu ya hoja za bandari ilibidi wanaojibu waushambulie ushahidi wa wanaolalamika

Watu wanasema ukituhumiwa inakupasa uchane chane ushahIdi au STRIKE THE EVIDENCE TO PROVE THEM WRONG

Naona ishu ya bandari Mamlaka imezidiwa nguvu kwenye vifungu vya mkataba

Chalamila ajibu vifungu vya mkataba
Azijibu zile articles
Wenzake hapa tulisema tatizo ni lugha na yeye chalamila aje na hoja zake sio vitisho
 
20230816_154837.jpg

Kauli za viongozi wa kibongo zinakinzana sana
 
anaweza fikiri anamfurahisha mama kumbe anajichimbia kaburi
 
Dawa ni KATIBA MPYA ili vyeo hivi vya Kindezi vipotee
 
Viongozi tendeni kwa hekima na muwe na kiasi. Kuna kesho pia.

Power is not permanent!

-Kaveli-
 
Kuna ambaye ameona hii ni hoja sahihi ya kwamba kwakua wavuvi wapo basi hapajauzwa?

Kuna uhusiano wa bandari na soko la Ferry?

Nafikiri RC ameharibu kuonyesha kwamba wanaokamatwa ni yeyote atakayetaka kuongelea ishu ya bandari.
Hata aliemteuwa hakubaliani nahiyo kauliyake.
 
Viongoziwa hovyo kama chalamila eti anakua RC OVYO HATA HOJA ZAO ZA HOVYO HULKA YAKE YA KILEVI SANA
 
Jamaa wakati mwingine awe ananyamaza tu.

Kumbe bandari inahusika na kuuza samaki?!

Hiyo ndio akili ya Rais wa Mkoa wa Dsm
Kuna wakati mtu akiwa anaongea mie huwa naona aibu amabe nasoma maneno yake
 
Huyu anaidhalilisha serikali.
Kwa hiyo kukosoa ndiko kumepelekea watu kukamatwa na kuwa wahaini?.
Huyu hafai kuwa RC.
 
Back
Top Bottom