RC Chalamila ajibu madai ya Hospitali za Mbeya kujaa wagonjwa

RC Chalamila ajibu madai ya Hospitali za Mbeya kujaa wagonjwa

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Joined
Aug 24, 2011
Posts
53,868
Reaction score
121,001
RC Mbeya, Albert Chalamila akiwa Kanisa la KKKT Dayosisi ya Konde kwenye Uzinduzi wa Ofisi Kuu ya Dayosisi na Kanisa Kuu amenena haya kuhusu hospitali mkoani humo kujaa wagonjwa

Mkuu-wa-Mkoa-wa-Mbeya-Albert-Chalamila.jpg

“Wapo Watu wanatishia Watu wanasema Mahospitalini huko kumejaa sana wagonjwa, Serikali ijenge Vituo vya Afya kwa Mabilioni ya pesa halafu viwe havina mgonjwa!?”

“Ukisema Hospitali zimejaa unataka wajae walevi au waumini?, Kanisa linajaa likiwa na waumini, Hospitali zinajaa zikiwa na wagonjwa, vilabu vinajaa vikiwa na walevi, mashamba yanajaa yakiwa na wakulima, sasa unachoshangaa kujaa kwa wagonjwa Hospitali ni kitu gani?”
 
Nadhani akijua maana ya overcapacity / undercapacity na optimum capacity asingeongelea haya ?

Kama kila siku zinajaa basi hazitoshi / hazikidhi mahitaji.....

Kama kipindi hiki zimejaa isivyo kawaida basi kuna mfumuko / tatizo ambalo inabidi ijulikane limesababishwa na nini ili kulitafutia ufumbuzi
 
Makanisa siku hizi yamekuwa sehemu za kupiga siasa wazi?

Mkuu wa Mkoa kashindwa kuitisha mkutano ofisini kwake kusema habari ambazo hazihusiani na dini?

Kwa nini tunavunja separation of church and state?

Nimeona Magufuli kaanza hizi habari, sasa mkuu wa mkoa anamfuatisha.
 
Huyu RC Chalamila ana majibu ya kunya utadhani naye hakuzaliwa kwa njia ya kawaida.
 
Back
Top Bottom