Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amezungumzia kifo cha Mtumishi wa Mamala ya Mapato Tanzania (TRA) Amani Kamguna ambaye ameagwa Jumapili, Disemba 8 katika viwanja vya michezo vya TRA Kurasini Dar es salaam ambapo amesema kifo chake ni hasara kwa Familia na kwa Taifa huku akisema eneo palipofanyika tukio patasafishwa.
Akiongea wakati wakuaga mwili, RC Chalamila amesema "Kitendo hiki kilichotokea hakina maelezo mengi kwa sababu walijitambulisha kwamba wanafanyakazi TRA na yule Bwana akafunga vioo katika gari lake kwamba hashuki akatumia muda mwingi kuwaita wenzake na akapiga kelele kwamba anatekwa mwisho wa siku kikatokea hiki kilichotokea"
"Kamishna Jenerali amesema kwamba kuna Watu wanatoka nyumbani wakiwa wamejipanga kwamba watatii sheria na shuruti, mambo haya yatapatiwa majibu muda sio mrefu, hasara hii haina mbadala, ni hasara kwa Taifa na kwa familia yake"