RC Chalamila: Alipouawa Afisa wa TRA patasafishwa

RC Chalamila: Alipouawa Afisa wa TRA patasafishwa

Etii jamaa alielamba udongo achangiwe hata afu 10 10 familia inunuliwe bond ila wanasiasa wanajua kucheza na akili za watuuu...jamaa kajimix kapata alichopata wapo kibao waliopotea na bado wengine kesi zao hata haziongelewi kama hakuna kilichotokea.
 
Hapa naona kama anachokozwa baba muumba .........yaani binadamu mwingine akiuawa sawa mwingine hakuna sio sawa...........inamaana wanajaribu ukuu wa mungu ?? Sisi sote ni wamavumbini tu na kwake tutarudi.......huu ushupazaji shingo unatokea wapi tena?? BABA MUNGU TUNAKUOMBA SANA KAMA ITAFAA HUYU HUU MWAKA HUWE NDIO WA MWISHO KWENYE HII DUNIA YAKO ULIYOSEMA TUKAE KWA AMANI KUKUABUDU WEWE TU NA WALA SI MADARAKA WALA VYEO AU NAFASI TULIZONAZO........KUWAANGUSHA WENGINE MAKUSUDI NA BILA HATIA HILI TUPENDWE NA KUJILIMBIKIZIA HAZINA ZISIZOKUA ZETU HALALI........AMINA
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amezungumzia kifo cha Mtumishi wa Mamala ya Mapato Tanzania (TRA) Amani Kamguna ambaye ameagwa Jumapili, Disemba 8 katika viwanja vya michezo vya TRA Kurasini Dar es salaam ambapo amesema kifo chake ni hasara kwa Familia na kwa Taifa huku akisema eneo palipofanyika tukio patasafishwa.

Akiongea wakati wakuaga mwili, RC Chalamila amesema "Kitendo hiki kilichotokea hakina maelezo mengi kwa sababu walijitambulisha kwamba wanafanyakazi TRA na yule Bwana akafunga vioo katika gari lake kwamba hashuki akatumia muda mwingi kuwaita wenzake na akapiga kelele kwamba anatekwa mwisho wa siku kikatokea hiki kilichotokea"

"Kamishna Jenerali amesema kwamba kuna Watu wanatoka nyumbani wakiwa wamejipanga kwamba watatii sheria na shuruti, mambo haya yatapatiwa majibu muda sio mrefu, hasara hii haina mbadala, ni hasara kwa Taifa na kwa familia yake"
View attachment 3172687
Isivyo bahati yeye ndio watamsafisha kabisa na ataisikia hewani mji unaoitwa Dar Es Salaam. Anatishia wananchi wanaostahiki kulindwa lakini anajitutumua kufanya mambo ya ajabu.

Wanatengeneza uasi mkubwa sana nchini na huyu RC hawezi kuendelea kuwepo hapo alipo ataondolewa na kuwekwa pembeni kabisa ili asubiri kwenda kugombea ubunge kwao Mufindi au Njombe
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amezungumzia kifo cha Mtumishi wa Mamala ya Mapato Tanzania (TRA) Amani Kamguna ambaye ameagwa Jumapili, Disemba 8 katika viwanja vya michezo vya TRA Kurasini Dar es salaam ambapo amesema kifo chake ni hasara kwa Familia na kwa Taifa huku akisema eneo palipofanyika tukio patasafishwa.

Akiongea wakati wakuaga mwili, RC Chalamila amesema "Kitendo hiki kilichotokea hakina maelezo mengi kwa sababu walijitambulisha kwamba wanafanyakazi TRA na yule Bwana akafunga vioo katika gari lake kwamba hashuki akatumia muda mwingi kuwaita wenzake na akapiga kelele kwamba anatekwa mwisho wa siku kikatokea hiki kilichotokea"

"Kamishna Jenerali amesema kwamba kuna Watu wanatoka nyumbani wakiwa wamejipanga kwamba watatii sheria na shuruti, mambo haya yatapatiwa majibu muda sio mrefu, hasara hii haina mbadala, ni hasara kwa Taifa na kwa familia yake"
View attachment 3172687
Wasiojulikana wameanza kupata TIBA STAHIKI, huyo RC mlevi ajue tu kwamba kwasasa hali itakuwa mbaya zaidi kwa MAGENGE YAO YA UTEKAJI.
 
Serikali kama wanaakili inabidi wabadilike namna ya ukamataji wao.waepuke ukamataji wa kiutekaji.wakiendelea ukamataji wa kiutekaji ipo siku wananchi wataitoa serikali nzima madarakani.wananchi wakiamua hakuna kitakachowazuia
Watekaji wa Mzee Kibao hao, wanabahati sana wale wengine wenye silaha walichomoka mbio. Kwasasa wananchi tumeamua ni mwendo wa kiberiti tu, hadi pale tutakapoheshimiana.
 
Hii si sawa na Wananchi tuikemee. Hakuna damu yenye thamani na isiyo na thamani. Binadamu wote ni sawa, leo unajiona una cheo, kesho nawe ni mwananchi wa kawaida.

Huyu Chalamila kwanini anapenda kuropoka ropoka. Katika nchi zenye viongozi wa hovyo, kuanzia chini mpaka juu Tanzania iko kwenye 10 bora.

Hawana hofu ya Mungu ndani yao, kwahiyo wamekufa watu hapa, wametekwa hao haina haja ya kusafishwa waliotenda. Leo kafa huyo eti patasafishwa. Itaanziwa yeye na ukoo wake.
Hata hivyo KIFO NI KIFO.
 
Alipouwawa mzee Ali Kibao, palisafishwa nini?

Au hapa duniani kuna vifo ambavyo ni 'special' na vifo vya wengine ni kama kauawa mnyama?

RC Chalamila, hebu muwe mnachuja ndimi zenu mnapokuwa kwenye hayo majukwaa. Kumbukeni mnaishi kwa kodi za wananchi.

Cheo cha umma ni kama koti la kuazima. Leo unacho, kesho hauna.

Kifo ni kifo tu.

-Kaveli-
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amezungumzia kifo cha Mtumishi wa Mamala ya Mapato Tanzania (TRA) Amani Kamguna ambaye ameagwa Jumapili, Disemba 8 katika viwanja vya michezo vya TRA Kurasini Dar es salaam ambapo amesema kifo chake ni hasara kwa Familia na kwa Taifa huku akisema eneo palipofanyika tukio patasafishwa.

Akiongea wakati wakuaga mwili, RC Chalamila amesema "Kitendo hiki kilichotokea hakina maelezo mengi kwa sababu walijitambulisha kwamba wanafanyakazi TRA na yule Bwana akafunga vioo katika gari lake kwamba hashuki akatumia muda mwingi kuwaita wenzake na akapiga kelele kwamba anatekwa mwisho wa siku kikatokea hiki kilichotokea"

"Kamishna Jenerali amesema kwamba kuna Watu wanatoka nyumbani wakiwa wamejipanga kwamba watatii sheria na shuruti, mambo haya yatapatiwa majibu muda sio mrefu, hasara hii haina mbadala, ni hasara kwa Taifa na kwa familia yake"
View attachment 3172687
Ninawashauri waanze kuisafisha ccm na genge la polisi kwanza, maana hawa ndio walioifikisha jamii/wananchi kwenye hatua hiyo.
Wanapaswa kujua kuwa,wao sio miungu na kamwe hawatakuwa, wajifunze yanayoendelea huko Syria na baadhi ya mataifa mengine..
 
Wanataka kupasafisha ? RC aangalie asije akawa anazidi kuwagawa na kuwatenga hao wananchi wa Tegeta na vyombo vya serikali maana inaonekana ni kama raia wamejiwekea kuwa ni sisi dhidi "yao"

Na mazingira ni karibu na alipotekwa na kuuawa Hayati Ali Kibao.
Kwa hiyo ni kama wako alerted namna fulani hivi isiyo kawaida.
 
Stupid RC. Wakati Ally Kibao anatekwa na kuuawa walijifanya hayawausu. Leo mtu asiyejulikana Kauawa wanapiga mikwara kila Kona.
 
Back
Top Bottom