RC Chalamila asema mjamzito anayegoma kununua gloves akajifungulie nyumbani. Hafai kuendelea kubaki madarakani

RC Chalamila asema mjamzito anayegoma kununua gloves akajifungulie nyumbani. Hafai kuendelea kubaki madarakani

Hali imepelekea wanaostahili kulazwa KCMC wanauguziwa vichochoroni. Ameumia staff mkubwa kwa ajali kavunjika mguu, hapa mjini lakini kakubali kwenda tibiwa BOMA, kalazwa chimba cha uwani na hataki kusikia neno KCMC.
Hii ni fedheha kwa hospitali yetu. Walio izunguka ni mapato ya kiasi gani yanapotea?
Na hali ikiendelea hivi, ipo siku patabaki majengo bila wagonjwa. Lau kama ndio lengo la mkurugenzi wa KCMC Mr, Masenga ajuwe limefikia 95% ya mafanikio. Lkn kama siyo lengo kutoa kitengo cha utabibu kibakie chuo pekee, namsihi achukuwe hatua za haraka mno. Laptop walizo nazo wanachuo wodini ni za kuchati muda wote, na baadae wanaenda kudanga Mimi'z, na kwenye Virokonya vya jirani, tena kwa kuwatapeli wazazi wao ety, kuna topic natakiwa nii downlood toka chuo flani america ama ulaya wazazi wanaenda kukopa kumbe hakuna chochote wanaibiwa.
Mfano Rafiki yangu nahifadhi jina, bint yake alipata ajali Dar, wakati ni mwanachuo KCMC wakati mchana wake aliwasiliana nae kumjulia hali na kamwambia yuko darasani KCMC.
 
Hospitali zipo hoi, wamepunguza pesa za basket fund kwa zaidi ya 60%! Mabango ya mama ameweza mnayoyaona nchi nzima ni "wapigaji na wakwepa Kodi" wanatafuta kinga ya kuendelea kukwepa Kodi.

Chalamila kaamua kutoboa Siri Tu ya jinsi Hali ilivyongumu kwenye taasisi za umma!
 
Tatizo lenu mkiambiwa ukweli mnaleta siasa..embu shauri ungekuwa wewe ungefanyaje..mgonjwa katibiwa bahati mbaya kafariki, je angekuwa amepona ndugu wasingelipa?? Je akifa inamaanisha hakutumia dawa ??? Au Rais aliwaambia serikali italipa??..
Nadhan RC amewaambia ukweli mchungu ambao inatakiwa tuuzoee..
Mimi nimempeleka mgonjwa atibiwe apone.. Sio atibiwe ili afe! Ni kama umepeleka gari kwa fundi likatengenezwe halafu halijapona kisha fundi akudai pesa ya vifaa!
 
Je mbaya ni yule anayeongelea suala hili ambalo ni ukweli linaloonyesha failure ya serikali au wale wanaotwambia kila kitu kipo vizuri wakati kitaa hapakaliki ? Kwahio unaona dawa ni kumfukuza huyu ili aje mwongo anayeficha au kubadilisha system inayotoa huduma kuendena na kodi zetu ?

Kaongea ukweli na hakuna alichokosea na ndiyo maana kaletwa Dar Es Salaam
 
Mimi nimempeleka mgonjwa atibiwe apone.. Sio atibiwe ili afe! Ni kama umepeleka gari kwa fundi likatengenezwe halafu halijapona kisha fundi akudai pesa ya vifaa!
Kuna fundi ataweka kifaa kwa kununua kwa pesa yake
 
Chura ndio tatizo NAMBA moja. Ndio maana mwamba anatapika atakavyo.kwakua anajua kua chura akuna anacho jua.
KAZI ni kipimo cha UTU
 
Kiongozi unapopigiwa Simu na mpiga kura akakueleza tatizo Usimnyanyapae bali mchukulie Kwa Upendo

Alimjibu hivi mama aliye katika Uchungu wa kutaka kujifungua? 🐼

Kwako Mary Chatanda
Amejibu Kama Kiongozi Na Sio Msimamizi wa Kura..
Siku Zote Mtu yoyote anayetaka Kuchonganisha Mamlaka ya Serikali Hafai..
Yoyote anayetaka Kuonyesha ufalme umefitinika Ni Mnafiki..
Alipiga Simu Kuuliza Kuhusu Haki kwanini Asingeenda Kwenye Ofisi za Utawala wa Hospitali na Angepata Ufafanuzi Mzuri kwanini kaagizwa na kama Ni sera ya Hospitali alitakiwa Aiheshimu..

Mkuu wa Mkoa Hawezi Kuingilia Proffesional Za Watu na Ndo maan Kampa JIBU la Kukitafakari
 
Ajabu sio muda mrefu utaona picha Jenista Mhagama, yupo na wazungu anawapiga porojo vifo vya uzazi vimepungua na matakwimu yao ya kupika.

Kama sera ni mbovu tu, hiyo huduma itakuwaje ndani ya hospitali.

Watu wamelalama Ummy hatoshi hapo atolewe, huyu mama alivyo nadharau kaenda weka bogus zaidi. Walau, huyo Ummy kwa hiyo kauli angesha tweet sio msimamo wa serikali (huku kimomoyo anasema watajua wenyewe hospitali watapotoa hizo gloves).

Jenista yeye wala hana habari hapo ndio kwanza huu mwaka wa uchaguzi anawaza siku akirudi kijijini kwao wamama wajigalalaze awakanyage na alivyo bonge. Sijui kwanini ‘bi-tozo’ akushuka kwenda kumkanyaga Jenista siku aliyojigalagaza mbele yake na yeye aone maumivu ya kukanyagwa na kibonge kama alivyozoea.

Hizo habari za vifo vya wamama kisa kukosa gloves havimnyimi usingizi Jenista wala raisi wa Tanzania.
 
I think katumwa na Mkuu wa Nchi ayaseme haya sababu mambo aliyo zungumza ni mazito mno. Elfu hamsini ni hela kubwa kwa watanzania wa kawaida hasa vijijini, kuna huduma kiongozi unapotolea maelekezo lazima kutuliza kichwa. Kama hospital inakosa vifaa vya bei rahisi tu, je hali ikoje katika masuala nyeti tusiyo yaona?
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Albert Chalamila amewataka wananchi wa mkoa huo kuacha kuingiza siasa katika mambo yanayowahusu binafsi hasa katika Afya kwani hazitawasaidia badala yake zitawachelewesha na pia kuwa na madhara zaidi.

Akizungumza hivi karibuni na wanachi wa Temeke jijini Dar Es Salaam, Chalamila aliwaambia kuna vifaa vya hospitali inapowalazimu wanunue kwani sio wakati wote hospitali zitakuwa na vifaa kamili.

Pia soma:
Chalamila alimuelezea mama mmoja mjamzito aliyempigia simu akilalamika kuambiwa na Daktari atoe shilingi elfu 50,000/= ili inunulie vifaa vya kumsaidia kujifungua ikiwemo gloves ambapo Chalamila alimwambia asitoe fedha aende nyumbani akajifungue.

==================================================

Mwenye direct connection amfikishie mama SSH ujumbe huu, atuondolee huyu MTU hapa dsm, ampeleke Rauha akalinde wanyama, hafai kuwa kiongozi

Aliteleza ulimi ila Bado ni Kiongozi mzuri,kikubwa aombe radhi.
 
I think katumwa na Mkuu wa Nchi ayaseme haya sababu mambo aliyo zungumza ni mazito mno. Elfu hamsini ni hela kubwa kwa watanzania wa kawaida hasa vijijini, kuna huduma kiongozi unapotolea maelekezo lazima kutuliza kichwa. Kama hospital inakosa vifaa vya bei rahisi tu, je hali ikoje katika masuala nyeti tusiyo yaona?
🚮🚮
 
Ndo maana watoto wangu wote wamezaliwa kairuki. Ila twende mbele turudi nyuma vifaa vya elf 20 mwanaume kamili unashindwaje kununua?
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Albert Chalamila amewataka wananchi wa mkoa huo kuacha kuingiza siasa katika mambo yanayowahusu binafsi hasa katika Afya kwani hazitawasaidia badala yake zitawachelewesha na pia kuwa na madhara zaidi.

Akizungumza hivi karibuni na wanachi wa Temeke jijini Dar Es Salaam, Chalamila aliwaambia kuna vifaa vya hospitali inapowalazimu wanunue kwani sio wakati wote hospitali zitakuwa na vifaa kamili.

Pia soma:
Chalamila alimuelezea mama mmoja mjamzito aliyempigia simu akilalamika kuambiwa na Daktari atoe shilingi elfu 50,000/= ili inunulie vifaa vya kumsaidia kujifungua ikiwemo gloves ambapo Chalamila alimwambia asitoe fedha aende nyumbani akajifungue.

==================================================

Mwenye direct connection amfikishie mama SSH ujumbe huu, atuondolee huyu MTU hapa dsm, ampeleke Rauha akalinde wanyama, hafai kuwa kiongozi

Hakuna Huduma za Bure Wala daktari hakuomba rushwa na Wala RC hajaongea uongo ila tuu alivyofikisha ujumbe sio Kwa Staha.

Ila RC ajiandae maana Mama anaweza watetea wa mama wenzie Kwa kumfukuza,awahi aombe radhi kabla ya mkutano wa Nishati haujakamilika.
 
Back
Top Bottom