Pre GE2025 RC Chalamila atangaza uuzaji viwanja Mabwepande-Kinondoni

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
sema Serikali imeshapima viwanja zaidi ya 2274.

-Awataka wale wote waliovamia na kujenga kulipia viwanja hivyo mara moja kwa kuwa wamepunguziwa bei.

Soma Pia: RC Chalamila afafanua video inayo trend aliyosema "Kama hutaki kununua Gloves kajifungulie nyumbani"

Kufuatia maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kutaka waliovamia na kujenga kwenye eneo linalomilikiwa na shirika la maendeleo Dar es Salaam (DDC) lililopo Mabwepande kuuziwa viwanja kwa gharama nafuu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila kwa kushirikiana na shirika hilo pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya kinondoni ametangaza rasmi rasmi kuanza kuuza viwanja katika eneo hilo

Snapinst.app_474482216_18291649537246773_1209029131461921209_n_1080.jpg
Snapinst.app_475179356_18291649510246773_3505386225995960734_n_1080.jpg
 
Tupewe utaratibu na sisi wengine tununue
 
sema Serikali imeshapima viwanja zaidi ya 2274.

-Awataka wale wote waliovamia na kujenga kulipia viwanja hivyo mara moja kwa kuwa wamepunguziwa bei.

Soma Pia: RC Chalamila afafanua video inayo trend aliyosema "Kama hutaki kununua Gloves kajifungulie nyumbani"

Kufuatia maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kutaka waliovamia na kujenga kwenye eneo linalomilikiwa na shirika la maendeleo Dar es Salaam (DDC) lililopo Mabwepande kuuziwa viwanja kwa gharama nafuu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Albert Chalamila kwa kushirikiana na shirika hilo pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya kinondoni ametangaza rasmi rasmi kuanza kuuza viwanja katika eneo hilo

View attachment 3229499View attachment 3229500
Trump shikilia hapo hapo wstauza sana mwaka huu
 
Mabwepande inaanza kuchangamka sasa. Wajenge barabara tuone maghorofa yatakavyoanza kuinuka.

Wanaposema wamepunguza bei bila kutuambia bei ya awali na bei ya sasa tutaamini vipi kuna punguzo?

Na kwanini Serikali inauza kwa hasara kuna haraka gani au dharura gani mpaka tutangaziwe punguzo la bei?

Nunueni muanze kulipa kodi za ardhi, serikali ipate pesa.

Basi Serikali nayo iwe inajenga Barabara wao wanauza na kuchukua pesa tu miundo mbinu wamesahau.
 
Hivi joto na vumbi la Dar es Salaam linapozwa na pori gani? Kila sehemu makazi tu...buffer zones hakuna. Badala ya serikali kuna na njia muafaka wa kutwaa na kuendeleza arshi za sehemu kama Magomeni, Msimbazi, mwananyamala yote, Sinza yote, Manzese, Kiwalani, michikichini, karume, na maeneo yote ya Dar es salaam yaliyo na makazi yasiyofaa.
Mipango mji unakimbilia kupima maeneo yanayofaa kubaki pori la kupoza joto la Jiji.
Mji gani usiyikuwa na pori?
 
Tuone Sasa na Nkuhungu broad acre Dodoma maeneo ya watu walikuwa wamepimiwa na kupewa nyaraka na baadaye Halmashauri ya Jiji upande wa maafisa Ardhi wakishirikiana na kupandikiza kuwa wenyeviti wa mitaa kupima eneo hilohilo lililokuwa limepimwe na kuhalalisha Uvamizi kuwa Urasimishaji

Tuone nako itakuwaje kumpunuzia bei mvamizi?

Tuheshimu Katiba

Haki itendeke na ionekane Waziri sio kwa upendeleo!!
 
Mabwepande inaanza kuchangamka sasa. Wajenge barabara tuone maghorofa yatakavyoanza kuinuka.

Wanaposema wamepunguza bei bila kutuambia bei ya awali na bei ya sasa tutaamini vipi kuna punguzo?

Na kwanini Serikali inauza kwa hasara kuna haraka gani au dharura gani mpaka tutangaziwe punguzo la bei?

Nunueni muanze kulipa kodi za ardhi, serikali ipate pesa.

Basi Serikali nayo iwe inajenga Barabara wao wanauza na kuchukua pesa tu miundo mbinu wamesahau.
We endelea kukaa kwa shemeji,ukikua utajua umuhimu wa ardhi bwana mdogo,wenzio tushaanza mchakato wa kununua tayari
 
Hivi joto na vumbi la Dar es Salaam linapozwa na pori gani? Kila sehemu makazi tu...buffer zones hakuna. Badala ya serikali kuna na njia muafaka wa kutwaa na kuendeleza arshi za sehemu kama Magomeni, Msimbazi, mwananyamala yote, Sinza yote, Manzese, Kiwalani, michikichini, karume, na maeneo yote ya Dar es salaam yaliyo na makazi yasiyofaa.
Mipango mji unakimbilia kupima maeneo yanayofaa kubaki pori la kupoza joto la Jiji.
Mji gani usiyikuwa na pori?
Dar Es Salaam inatakiwa kupanuliwa kwenda Mapinga, KIbaha, Makurunge ya Kisarawe na Vikindu ya Mkuranga.

Pori la mabwe kuzidi kuligawa kwa jili ya ujenzi wa makazi ni uharibifu wa mazingira
 
Kuna majiji makubwa kwa idadi ya watu lakini madogo ki eneo kuliko Dar lakini kuna mapori na wametunza mazingira vizuri sana.
Bams za mto msimbazi ilifyeka makazi ya watu Mbezi kwa Msuguli ila serikali ata hawajui chanzo ni mipango miji mibovu.
WanaMazingira kama NEMC sijui kazi yao ni nini sasa. Hopeless kabisa.
Dar Es Salaam inatakiwa kupanuliwa kwenda Mapinga, KIbaha, Makurunge ya Kisarawe na Vikindu ya Mkuranga.

Pori la mabwe kuzidi kuligawa kwa jili ya ujenzi wa makazi ni uharibifu wa mazingira
 
Hii kali mnauza bila Bei!!
Kazi ni kipimo cha UTU
 
Wavamizi wakati wana hati?je hizo hati zilitolewa na nani?na watu wamekuwa wakilipia hizo hati mpaka sasa leo wanaitwa wavamizi?!

Viwanja vimeuzwa vyote ndani ya dakikoa moja?!
 
Back
Top Bottom