Nadhani watu wa CCM hawapeani report, kila mtu anafanya anavyojiskia. Hakuna boss wala wa chini. Halafu hata social media hawasomi. Inakuaje serikali inayokaa Dar ilikua haijui kwamba DART ina matatizo mazito hadi vurugu za Magomeni.?
Inawezekana kabisa Majaliwa ndio leo amesikia UDART kuna shida ndio kaja mbio mbio.
Rais naye si ajabu leo ndio amejua kuna tatizo ndio maana kamfukuza kazi Kibamia.
Nchi nyingine by the time rais anakunywa supu asubuhi anakua keshapitia magazeti yote, kesha pata ripoti za kiintelejensia kutoka kwenye majeshi yote. Kutoka mikoa yote na wizara zote.
Kwa kumuabgalia tu Chalamila alivyokua na kiburi unaona kabisa hapeleki report popote.