Sorry Mkuu nimekufananisha kumbe ..Mimi ndio Chalamila tena? 🤣🤣
nyamongolo ndo penyewe me ndo makazi yangu nlipoweka mjengo japo napiga mishe zangu pwani.Point wacha tu tunywe maisha yenyewe mafupi hivi jiwe tumemzika hata urais ajaufaidi vizuri.
Wacha tulewe tu maisha ni mafupi sana pesa tumeshatafuta na tunaendelea kutafuta halafu tufe tuziache ..
Kelele maana yake ulichagua mwanza kuna maeneo mengi sana yasiyo na usumbufu wa kelele
Kama Kiseke, Buswelu usagala, Nyasaka,Kiloleli, Nyamongoro na maendeo mengine mengi
Uza kwenye kelele kajenge kwenye utulivu.
Yupo sahihi 100%.
View attachment 1800253
wewe sasa ndo umemuelewa anamaanisha jamani mambo ya kufuatiliana machaguo ya staili yamaisha vita yake hashindi mtu na sisi tutakomaa hakuna mangoma ya kusifu usiku waanze kusema tunamkufuru mungu tenaSwala la kelele wakiliingiza tutaingia hadi haya makanisa ya uswahili yanayokesha.
Yes, tena watu wanywe tu , maana serikali haijali afya ila inajali mapato.View attachment 1800234
MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila, amewataka wakazi wa mkoa huo kunywa pombe kwa kuwa inachangia kukuza uchumi wa nchi kupitia kodi za serikali.
Chalamila ameyasema hayo jana jijini Mwanza alipozungumza na uongozi wa Mamlaka ya Mapato (TRA).
Alisema watu wakiacha kunywa pombe maana yake mapato ya serikali yatapungua kwa sababu unywaji pombe unaongeza kodiza serikali.
Kuhusu baadhi serikali ya baa kupiga kelele za muziki, Chalamila alisema hapo ndiyo mahala pake, kwa kuwa asingetegemea sehemu kama hizo ziwe na utulivu.
Aidha, alitaka TRA kukusanya mapato ya serikali kwa “kuwafinya kidogo” wafanyabiashara wasiotaka kulipa kwa hiari.
Alisema licha ya Rais Samia Suluhu Hassan kuagiza TRA kutumia busara na akili, lakini wakati mwingine lazima wawe wakali kwa wafanyabiashara wasiotaka kulipa kwa hiari.
Kuhusu wafanyabiashara kutoa risiti halali wanapouza bidhaa zao, Chalamila alitaka TRA kusimamia hilo.
Aidha, Chalamila alisema wafanyabiashara wengi hawatoi risiti za mashine wakati wa kuuza bidhaa zao, hatua ambayo inaikosesha mapato serikali na kuagiza TRA kuweka mkazo katika eneo hilo.
Mkuu wa huyo wa mkoa baada ya kukabidhiwa ofisi, alianza ziara ya kutembelea taasisi mbalimbali za serikali na kuzungumza na watumishi.
kwani usipikunywa huugui??Yes, tena watu wanywe tu , maana serikali haijali afya ila inajali mapato.
Hata hao walokole wapiga kelele waambie wasali taratibu..sio kusumbua watu wakiwa wamepumzika.Swala la kelele wakiliingiza tutaingia hadi haya makanisa ya uswahili yanayokesha.
una mawazo kama ya wabunge wa viti maalum CCM.kwani usipikunywa huugui??
kunywa bia weweeee, uone utamu wa maisha, RC atadumu mileleuna mawazo kama ya wabunge wa viti maalum CCM.
Piga vyomboSawa sawa kabisa
Rc yuko sawa kabisa
Ova
Mimi na Chalamila hatufanani, angeongelea bangi sawa, hiyo habari imekuwa automatically extracted kwa kutumia OCR (Optical Character Recognition) kutoka kwenye gazeti la nipashe najaribu kufanya optimization ya huo mfumo uliotumika kubadili maandishi yaliyopigwa picha au kutolewa kama picha kwa haraka, sio kila kitu kinaandikwa humu hiyo kazi Chalamila mwenyewe hawezi kuifanya. Habari yenyewe ni hiyo hapo 👇Wewe na chalamila akili zenu zinafana!! ona hata ulivyoandika!!
Nilishangaa kule Songea saa nne asubuhi ukienda bar ukiagiza bia wanakuambia hatuuzi tunaogopa kukamatwa, ukikamatwa faini laki mbi