RC Chalamila awataka wakazi wa Mwanza kunywa pombe ili kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi, asema baadhi ya baa kuwa na kelele za muziki ni sawa

RC Chalamila awataka wakazi wa Mwanza kunywa pombe ili kuchangia ukuaji wa uchumi wa nchi, asema baadhi ya baa kuwa na kelele za muziki ni sawa

Mkuu nakukaribisha sana weekend hii tuanzie kupiga UGIMBI kule Kitangiri Matako baa, tushuke kidogo hadi kona ya Bwiru pale Diamond na Las Vegas, halafu tukamalizie pale kwa misifa bia zote ndogo zinauzwa sh 1300 naamini utainjoi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Point wacha tu tunywe maisha yenyewe mafupi hivi jiwe tumemzika hata urais ajaufaidi vizuri.

Wacha tulewe tu maisha ni mafupi sana pesa tumeshatafuta na tunaendelea kutafuta halafu tufe tuziache ..

Kelele maana yake ulichagua mwanza kuna maeneo mengi sana yasiyo na usumbufu wa kelele

Kama Kiseke, Buswelu usagala, Nyasaka,Kiloleli, Nyamongoro na maendeo mengine mengi

Uza kwenye kelele kajenge kwenye utulivu.

Yupo sahihi 100%.
View attachment 1800253
nyamongolo ndo penyewe me ndo makazi yangu nlipoweka mjengo japo napiga mishe zangu pwani.
 
Swala la kelele wakiliingiza tutaingia hadi haya makanisa ya uswahili yanayokesha.
wewe sasa ndo umemuelewa anamaanisha jamani mambo ya kufuatiliana machaguo ya staili yamaisha vita yake hashindi mtu na sisi tutakomaa hakuna mangoma ya kusifu usiku waanze kusema tunamkufuru mungu tena
 
View attachment 1800234

MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila, amewataka wakazi wa mkoa huo kunywa pombe kwa kuwa inachangia kukuza uchumi wa nchi kupitia kodi za serikali.

Chalamila ameyasema hayo jana jijini Mwanza alipozungumza na uongozi wa Mamlaka ya Mapato (TRA).

Alisema watu wakiacha kunywa pombe maana yake mapato ya serikali yatapungua kwa sababu unywaji pombe unaongeza kodiza serikali.

Kuhusu baadhi serikali ya baa kupiga kelele za muziki, Chalamila alisema hapo ndiyo mahala pake, kwa kuwa asingetegemea sehemu kama hizo ziwe na utulivu.

Aidha, alitaka TRA kukusanya mapato ya serikali kwa “kuwafinya kidogo” wafanyabiashara wasiotaka kulipa kwa hiari.

Alisema licha ya Rais Samia Suluhu Hassan kuagiza TRA kutumia busara na akili, lakini wakati mwingine lazima wawe wakali kwa wafanyabiashara wasiotaka kulipa kwa hiari.

Kuhusu wafanyabiashara kutoa risiti halali wanapouza bidhaa zao, Chalamila alitaka TRA kusimamia hilo.

Aidha, Chalamila alisema wafanyabiashara wengi hawatoi risiti za mashine wakati wa kuuza bidhaa zao, hatua ambayo inaikosesha mapato serikali na kuagiza TRA kuweka mkazo katika eneo hilo.

Mkuu wa huyo wa mkoa baada ya kukabidhiwa ofisi, alianza ziara ya kutembelea taasisi mbalimbali za serikali na kuzungumza na watumishi.
Yes, tena watu wanywe tu , maana serikali haijali afya ila inajali mapato.
 
Nilishangaa kule Songea saa nne asubuhi ukienda bar ukiagiza bia wanakuambia hatuuzi tunaogopa kukamatwa, ukikamatwa faini laki mbili
 
Swala la kelele wakiliingiza tutaingia hadi haya makanisa ya uswahili yanayokesha.
Hata hao walokole wapiga kelele waambie wasali taratibu..sio kusumbua watu wakiwa wamepumzika.

Noisy pollution yoyote ni ya kupigwa vita.
 
Huyu so alituasa Wananchi tumuombee ili aache Ujinga?

Ina maana M/Mungu ameyakataa maombi yetu mapema hivi?
 
Mara pah!!! Watu wanaamia kwenye gongo ambayo hailipiwi kodi
 
kwenye suala la makelele kwenye makazi ya watu siungi mkono, mimi ni mnywaji ambaye sipendelei kunywa kwenye makelele au mziki mkubwa sana
Kuna baadhi ya bar zinapiga mziki kwa sauti kubwa sana hadi mida ya alfajiri saa 11
nyingi hazina vibali vya nightclubs na pia hazina sound proof
hii inaleta usumbufu mkubwa sana kwa wanaoishi jirani na bar hizo hili jambo sio zuri na pia ni kinyume na sheria za uuzaji wa vileo
RC kwenye suala la kelele kachemsa
Watuuzie tu bia hata ikiezekana masaa 24 ila wasibughuzi wananchi wengine kwa sauti kubwa za miziki
 
Wewe na chalamila akili zenu zinafana!! ona hata ulivyoandika!!
Mimi na Chalamila hatufanani, angeongelea bangi sawa, hiyo habari imekuwa automatically extracted kwa kutumia OCR (Optical Character Recognition) kutoka kwenye gazeti la nipashe najaribu kufanya optimization ya huo mfumo uliotumika kubadili maandishi yaliyopigwa picha au kutolewa kama picha kwa haraka, sio kila kitu kinaandikwa humu hiyo kazi Chalamila mwenyewe hawezi kuifanya. Habari yenyewe ni hiyo hapo 👇
IMG_20210528_155508.jpg
 
Back
Top Bottom