ChekoFagia
Senior Member
- Sep 20, 2025
- 115
- 339
Siku moja baada ya raia wa Kichina kukamatwa na mabilioni ya fedha huko Oysterbay, jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert ametoa wito kwa wananchi kujenga desturi ya kawaida ya kufuatilia sheria na miongozo mbalimbali iliyopo nchini ili kuepuka matatizo yasiyokuwa ya lazima
Chalamila ametoa wito huo leo, Jumatano Januari 07.2026 akiwa Kunduchi, Dar es Salaam alipokwenda kutatua mgogoro wa ardhi ambapo amesema Tanzania ni nchi nzuri iliyoweka sheria nzuri za kufuatwa lakini tatizo lililopo kwa Watanzania wenyewe ni kutosoma sheria hizo
"Hivi kwenye Sheria za Fedha kukaa na milioni 10 cash inakubalika?..., sasa mnajuwa hilo?..., sasa wewe uko na 'milela' pale mingi tukikuuliza hebu tueleze vizuri hii ni mauzo ghafi au faida, justify hilo tu, kama ni faida tujuwe na kama ni mauzo ghafi tujuwe ni shilingi ngapi, halafu tuone je ulikata risiti?, uliomba risiti au je ulilipa kodi ya serikali? hilo tu, lakini mngekuwa mnasoma vizuri sheria za nchi hii hata milioni 10 tu cash ni kinyume cha sheria kuwanayo"