RC Chalamila: Kukaa na Milioni 10 nyumbani ni kosa kisheria

Kwanini wanatambulishwa kama Wachina badala ya majina yao?

Hii sio kwamba inakua inawachafua wachina wote?

Wataalamu naomba kueleweshwa kwenye hili jambo.
Ni kosa la kiuandishi, unajuwa tena waandishi wetu wamesoma kwa kuungaunga
 
Tunazungumzia kufanya muamala au kukutwa na ...
Of course kukutwa na fedha ni matokeo wakati kufanya muamala ni mchakato. Hivyo matokeo lazima yana mchakato fulani uliotangulia (predicate event). Na hapo ndipo jinai inatafutwa. Jinai kama utakatishaji fedha, uhalali wa kufanya kazi nchini, ulipaji kodi TRA etc.

Ni maelezo mazuri tu yanahitajika
 
  1. Kwahiyo ukikutwa na kiasi hicho cha fedha nyumbani kwako kunaondoa uhalali wa wewe kua ndio mmiliki wa hizo hela?
  2. Kama utathibitisha kua hizo hela ni halali na ukaonyesha ushahidi wa zilivyopatikana,bado kosa la wewe kua na hizo hela Nyumbani itakua ni kosa? hata kama utasema kua ulikua kwenye mchakato wa kuzipeleka Benki?
  3. So,ukifunguliwa kesi ya kukutwa na hizo fedha Nyumbani,hukumu yake ni ipi? nini hatima ya hizo hela?
Naomba kueleweshwa hapa.
 
Wewe kilaza mataifa ya hovyo ndio huwa yanatafuta jinai kwa mbinu za uvuvi(fishing expedition) na hii husababishwa na incompetency ya vyombo vya uchunguzi au kuwasambua na kuwatesa wapinzani wa kisiasa kwa weaponizasition of law/lawfare. Katika utawala wa sheria wa kistaarabu mtu huanza kuchunguzwa pale ambapo ushahidi wa kosa kama ni ujambazi, ukwepaji kodi n.k unaonyesha alama kuelekea mtu fulani, sio huu ujinga wa kukamata mtu kwa hisia tu kisa ana bilioni nyumbani kwake unasema akupe maelezo amezipataje.
 
Kama 10,000,000 ni kosa kisheria kukaa nazo ndani, basi hiyo sheria ni nzuri na ni very protective

Lakini Ofisi ya Kampuni ya Mabasi ya Mwigulu Nchemba - ESTHER LUXURY COACH wanadai siku ya tarehe 29/10 wakati wa maandamano kupinga uchaguzi, walikuwa na pesa taslimu zaidi ya TZS 2.5B. Wanadai hizo ziliibiwa zote na waandamanaji!!

Huyu Mwigulu bila shaka ni muhuni wa mwisho kabisa. Na usikute alishapeleka Invoice Hazina ili afidiwe

Hizo Chalamila anasemaje?
 
kudai Kodi mnatumia nguvu nyingi hata kufunga watu au kutaifisha ..ila kushugulika na majizi na mafis
 
Sheria yoyote inayolazimisha au itakayolazimisha watu waweke kiasi chochote cha pesa za binafsi benki ni ya hovyo na ya kipuuzi inayopaswa kupingwa kwa nguvu zote.
Mkuu kila mtu akiweka hela zake nyumbani kiuchumi haina madhara kwa nchi?
 
Majibu ni kama ifuatavyo:-
1.Kukutwa na fedha nyingi nyumbani hakuondoi uhalali wako wa umiliki wa fedha hizo moja kwa moja. Sheria haikatazi kumiliki au kuhifadhi fedha taslimu nyumbani, hata kama ni nyingi. Umiliki wako unabaki halali mpaka ithibitishwe kinyume chake.
Lakini: Vyombo vya dola vina haki ya kuhoji chanzo cha fedha hizo kama kuna mashaka ya uhalifu (utakatishaji fedha, dawa za kulevya, rushwa n.k.).

2.Iwapo umeonyesha chanzo halali cha fedha (mf. biashara, mauzo ya mali, mshahara, mkopo n.k.) Ushahidi unaeleweka na unaridhisha (stakabadhi, mikataba, risiti, taarifa za biashara)

Hakuna kosa la kisheria la wewe kuwa na hizo fedha nyumbani.

3.Ikiwa unashindwa kuthibitisha chanzo halali, Mahakama inaweza;
-KUTAIFISHA fedha (forfeiture)
-Kukutia hatiani kwa kosa la money laundering
Adhabu inaweza kuwa; Faini kubwa, Kifungo (kulingana na kosa lililothibitishwa)

Ikiwa unathibitisha fedha ni halaliKesi itakuwa dismiss na Fedha zitarejeshwa kwako na HAZITAIFISHWA
 
Mkuu Yoda naomba tumalize tofauti zetu za kiitikadi. Maana unfanya upotoshaji wa wazi.

Kauli yako inaonyesha mchanganyiko wa jazba, uelewa mdogo wa sheria, na kupenda propaganda kuliko misingi ya utawala wa sheria.
Kwanza, ni upotoshaji mkubwa kudai kwamba kuhoji chanzo cha fedha ni “fishing expedition”.

Katika mifumo ya kisasa ya AML/CFT, mashaka yanayozuka kutokana na hali isiyo ya kawaida (red flags), ikiwemo kumiliki kiasi kikubwa cha fedha taslimu ni msingi halali wa uchunguzi wa awali, si hukumu, si unyanyasaji.

Pili, hakuna anayesema mtu akikutwa na fedha nyingi amekosa kosa moja kwa moja. Unachokosa kuelewa (au unapuuza kwa makusudi) ni kwamba uchunguzi SIYO hatia. Sheria hairuhusu dola kufumba macho pale mazingira yanapoibua mashaka yanayoweza kuhusiana na uhalifu wa kifedha.

Tatu, hoja yako ya kusema “mtu achunguzwe tu kama tayari kuna ushahidi unaomlenga” ni ujinga wa kisheria. Ushahidi hauanguki kutoka angani bali unapatikana kupitia uchunguzi. Kama ungesoma hata kidogo sheria za AML, ungejua kuwa:
Uchunguzi huanza kwa viashiria (indicators). Sio lazima kosa la awali liwe tayari limethibitishwa

Nne, kuingiza siasa na lawfare hapa ni kisingizio cha watu wanaotaka kinga dhidi ya uwajibikaji wa kisheria. Utawala wa sheria wa kweli hauwalindi wahalifu kwa kisingizio cha “haki za kiraia”, wala hauwatesi raia, unasimamia uwazi na uthibitisho.

Mwisho, kusema kuwa kuhoji chanzo cha bilioni ni “ujinga” ni kiburi cha kutojua. Nchi nyingi unazozisifia ndizo hizo hizo zinataka maelezo ya chanzo cha fedha, zinataifisha fedha zisizoelezeka na zinaheshimu presumption of innocence bila kuua uwezo wa dola kuchunguza
Kwa kifupi:
  • Kuulizwa maswali sio kunyanyaswa.
  • Uchunguzi sio hukumu.
-Kelele zako hazibadili misingi ya sheria.
Kama huwezi kutofautisha kati ya uchunguzi wa kisheria na mateso ya kisiasa, basi tatizo si sheria BALI ni uelewa wako
 
Kutoa pesa Bank ni njia moja ya haraka kuiangusha serikali ya CCM.
 
Waingereza wana msemo wao kabla ya kutunga sheria angalia gharama ya hiyo sheria.
Ni kweli hiyo sheria ipo lakini umetunga sheria ya tozo kwa pesa mtu akiweka benki, kipi bora nikae na pesa zangu nivunje sheria au niweke benki zikatwe tozo zipungue halafunajiita madr wa uchumi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…