RC Chalamila: Kukaa na Milioni 10 nyumbani ni kosa kisheria

Pesa nitafute mimi kwa shida mje mnipangie ninyi uliona wap!!?, hata milion 100 nakaa nazo tu si zangu bhana.
 
Mkuu kila mtu akiweka hela zake nyumbani kiuchumi haina madhara kwa nchi?
Haiwezekani kila mtu akaweka pesa zake nyumbani, Kuna watu wanapenda kuweka pesa benki tu bila hata kulazimishwa na sheria, kuna watu hawapendi kuwa na pesa nyingi cash au bank bali wangependa wawe na hifadhi ya dhahabu, ardhi, majengo, bonds, shares n.k
 
Hakuna SHERIA Tanzania inasema kukaa na 10m ni illegal.

Chalamila aache utapeli.

10m ni kama $4000 only.
 
Kwanini wanatambulishwa kama Wachina badala ya majina yao?

Hii sio kwamba inakua inawachafua wachina wote?

Wataalamu naomba kueleweshwa kwenye hili jambo.
Kama waliweza kutaja yule mmarekani aliyekutwa na vinavyosemekana vifaa vya ulipuzi itakuwa hawa wachina.?
 
Walioichangia CCM walienda na cash kubwa kuliko hiyo
 
Anavyoongea utadhani kuna rule of law kwenye hii nchi kumbe mambo yote ni ujambazi kwa kwenda mbele!
 
Alete hicho kifungu cha Sheria kinachosema hivyo maana CCM wamezoea kuendesha nchi kwa uongo, mazoea, ulaghai na ujanjaujanja.
Maajabu ni kwamba mtu kama huyu hata hajui kabisa kuwa serikali anayoitumikia sasa hivi ndiyo mkiukaji mkuu wa sheria kote nchini!
 
Huo ukamataji wa mabilioni, usije ukawa ni mpango ili baadae waseme hizo hela zilitaka zitumike kuwahonga vijana waandamanaji.
 
Usilalamike.
Unapojitambulisha kuwa upande wa uovu unakuwa umepoteza hadhi na 'credibility', hata pale unapozungumzia mazuri kama ulivyofanya hapo.

Sasa hata unapozungumzia sheria kama ulivyoeleza vizuri hapa, wakati huo huo huwezi kugeuka nyuma na kuzungumzia ubovu wa usimamizi wa sheria hizohizo.
Maana yake ni kuwa kuna kundi ambalo hizo sheria wao haziwahusu, na hao ndio utatokwa na jasho hapa hapa kuwatetea kama hujui kuwa sheria hizo zipo.
 
Kwa ufahamu wangu, kama wakili mwandamizi, hakuna Sheria yeyote inayokataza mtu kukaa na fedha nyingi ndani. Vilevile si lazima kuweka fedha benki.

Ni aibu kiongozi mkubwa kama RC, anapoongea tu mambo ya Sheria bila kupata kushauri.......
 
Kwa ufahamu wangu, kama wakili mwandamizi, hakuna Sheria yeyote inayokataza mtu kukaa na fedha nyingi ndani. Vilevile si lazima kuweka fedha benki.

Ni aibu kiongozi mkubwa kama RC, anapoongea tu mambo ya Sheria bila kupata kushauri.......
 
Kwani wao wanapoweka hizo hela benki na kutokukatia kodi sio kosa? Viongozi wengi wa serkali hawana tofauti na hao wachina. Wanapiga hela za serikali kifisadi wanaficha kwenye mabenki bila kukatia kodi kama sheria za nchi zinavyotaka.
 
Naona Yoda amekufurahisha sana. Anyway kila mmoja yuko entitled with his opinion, ndiyo freedom of expression
 
Kukaa na shilingi Milioni 10 ni kinyume na sheria kosa la kisheria? Lohhh Majangaa kweli nchi yetu bado tunafuata Siasa ya kijamaa na kujitegemea. Sheria alizo ziacha baba wa Taifa Mwalim Nyerere tunazitumia mpaka sasa. Kuna haki kweli ya kurekebisha katiba ya nchi kumbe anachogombea Mheshimiwa Tundu lissu kuhusu kurekebisha sheria za nchi ni haki ya ukweli kabisa. Sisi tuliopo nje ya nchi Disapora tutaogopa kuja na pesa nyingi nchini kwetu kuja kuwekeza kwani ukifika Airport Serikali ya Mama Samia Suluhu Hassan, itazichukuwa pesa zako. Bora tukawezekeze nchi jirani ya kenya kuliko kuwekeza nchini kwetu bado tunafuata Siasa ya kijamaa na kujitegemea siasa inayowanyima .haki na uhuru wa wananchi wake. mtihani kweli. Unasemaje? Pascal Mayalla


Your browser is not able to display this video.
 
Naona Yoda amekufurahisha sana. Anyway kila mmoja yuko entitled with his opinion, ndiyo freedom of expression
Nifurahi sana au nisifurahi, hilo halikuhusu, linalokuhusu ni ujumbe uliokulenga wewe.
 
Hukuniita, lakini sikubaliani na haya maneno yako ya kiujumla jumla namna hii.
Unacholalamikia hapo hakina uhusiano wowote na Ujamaa; na hata pangekuwa na uhusiano, maswala yaliyofanyika miaka ya sabini uyachukulie kuwa yatakuwa hivyo hivyo tu, kwa kuwa ni ya kijamaa, huku ni kukosa weledi.

Sasa ngoja nikufahamishe hili kama hulijui: hata huko kwenye nchi za kibepari unakoishi wewe, huwezi kujichukulia tu mahela kiwango chochote ukasafiri nayo bila ya taratibu za kutambulisha kuwa mapesa hayo umeyabeba. Hapa jirani Kenya unakokusema wewe; huwezi kuingiza tu kinyemela zaidi ya dolla elfu kumi!.

Uchina bado ni wakomunisti kabisa, unaweza kuwa na mahela nyumbani, lakini yakizidi kiwango fulani, sheria itakuandama vilevile.
Kwa hiyo hapa siyo swala la Ujamaa au Ubepari; ni sheria zinazosimamia mfumo wa kipesa duniani kote kuzuia utakatishaji wa hayo mahela.
 
Kwa ufahamu wangu, kama wakili mwandamizi, hakuna Sheria yeyote inayokataza mtu kukaa na fedha nyingi ndani. Vilevile si lazima kuweka fedha benki.

Ni aibu kiongozi mkubwa kama RC, anapoongea tu mambo ya Sheria bila kupata kushauri.......
Kama wewe ni Wakili basi labda ni Wakili wa kesi za kuku. Hli eneo la financial crimes maarufu kama money laundering wewe ni mbumbumbu kama fundi Maiko tu
 
Kama wewe ni Wakili basi labda ni Wakili wa kesi za kuku. Hli eneo la financial crimes maarufu kama money laundering wewe ni mbumbumbu kama fundi Maiko tu
Acha generalization, itaje Sheria husika na kifungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…