RC Chalamila kuwalipia nauli wana Dar Es Salaam 200 kushiriki betika Mbeya Tulia Marathon

RC Chalamila kuwalipia nauli wana Dar Es Salaam 200 kushiriki betika Mbeya Tulia Marathon

Pfizer

JF-Expert Member
Joined
Mar 25, 2021
Posts
819
Reaction score
1,093
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameyasema hayo leo April 15,2025 akiongea na waandishi wa Habari Ofisini kwake Jijini Dar es Salaam wakati akikabidhiwa Jezi maalum ya kushiriki Betika Mbeya Tulia Marathon ambayo mwaka huu inatarajiwa kufanyika Mei 9 - 10, 2025 Jijini Mbeya.

RC Chalamila ameeleza kwa kutambua kazi nzuri inayofanywa na Tulia Trust Faundation Mkoa huo utaanza amsha amsha ya kujinoa kuelekea Betika Mbeya Tulia Marathon mwezi huu April 19, 2025 kuanzia saa 12:00 Asbh katika eneo la Aghakan hadi Cocobeach.

Aidha kupitia amsha amsha hiyo wale ambao watafanya vizuri katika Marathon hiyo ofisi yake itawagharamia wana Dar es Salaam 200 nauli ya kwenda tu Mbeya ili kushiriki Betika Mbeya Tulia Marathon wakati wa kurudi watajigharamia wenyewe.

Vilevile RC Chalamila amesema kufanya mazoezi ni kuunga Mkono juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Dkt Samia Suluhu Hassan za kuhamasisha jamii kufanya mazoezi ili kuepuka magonjwa yasiyoambukiza ambayo yamekuwa na athari kubwa katika jamii.

Naye Afisa habari wa mchezo wa Kubahatisha wa Betika Bwana Rugambwa Pius amesema wamekuja kumuona mkuu wa Mkoa na kumkabidhi Jezi ya kushiriki Betika Mbeya Tulia Marathon kwa lengo la kumkaribisha yeye binafsi lakini pia wana Dar es Salaam ili waweze kushiriki Marathon hiyo kwa wingi zaidi wakiungana na wakazi wa Mbeya na maeneo mengine ndani ya nchi yetu ya Tanzania.
IMG-20250416-WA0004.jpg
IMG-20250416-WA0002.jpg
 
Rushwa za uchaguzi hizi. Ndo kazisema jana Wakili wa Lissu, Rugumeleza

Afrika, matajiri ni watumishi wa umma

Sijaona Ulaya eti charity foundation imetokana na hela ya ajira ya utumishi wa umma au ubunge na uspika. Yani unatajirika kwa utumishi.

Na zamani kamali ilikuwa unlawful. Baada ya kuruhusiwa, viongozi wanahimiza kamari. Waliisakama pool table weeee wakati fulani, wakasema inazaa uzembe na uzururaji na uteja na uvivu. Kumbe ni kwa vile hamna kodi mule!

Makodi ya Betika ndio wanagawana kwa maposho na mafao wanafungua vi foundation vya hela za umma, wanawalipia tileti za kwenda.

Kurudi mtajilipia! Na kula na kulala Mbeya. Na ma risk ya barabarani.

Tumefanywa ma zombie na majini.
.
 
CCM sijui anayejiamini mpaka sasa ni nani... Maana upepo wa kisulisuli wa CHADEMA umechakaza kula kona kona ya Tanganyika
 
Thinking yake siyo clear.
Atawalipia kwenda, halafu hatawalipia kurudi.
Au amesema nini?
 
Mambo mengine ni upuuzi na utoto unaofanywa na watu wazimq mpakq yanakera
 
Back
Top Bottom