RC Chalamila: Nimemwandikia barua Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda aitishe kikao cha wadau kujadili bei ya Saruji!

RC Chalamila: Nimemwandikia barua Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda aitishe kikao cha wadau kujadili bei ya Saruji!

Sijawahi kuona mifuko ya saruji
Kg 25
Kg 10
Kg 5

Hivi hili jambo haliwezekani ? Au ni utarstibu wa dunia nzima
Wazo zuri, sijawahi kuziona saruji chin ya kg 50.

Bora ziwepe kama sukar ilikua kweny paketi spesho inaanzia kg 1, sahiz mpaka robo ipo ya jero.
 
Ukiona wanaanza kuzungumzia maswala ya ‘capital allowance’ kwa wawekezaji ndio ujue wanaanza kuwa serious na Tanzania ya viwanda na uwezekano wa kutengeneza ajira millioni nane.
 
Safi sana mkuu wa Mkoa, huyu Katibu mkuu wa Viwanda na Biashara hata hasaidii, kwa crisis kama hiii alitakiwa kujitokeza hadharani kutoa kauli ya Serikali. Hongera sana Katibu mkuu Wizara ya Kilimo unaonekana kujua wajibu wako, kila siku tunakuona ukishughulikia kero za wananchi.Viwanda na Biashara mmeiangusha Serikali kwa hili la Cement. Ni hayo tu
 
Ahaaa ahaaa, halafu utasikia "nasema uongo ndugu zangu"
Kiongozi anatoa vision ni jukumu la makatibu wakuu kuwashauri mawaziri namna sahihi ya kufikia hiyo azma.

Na makatibu wakuu pamoja na senior servants wengine kama mkurugenzi wa TRA ni watu wanaotengenezwa na kupikwa kweli kweli nchi za wenzetu. Mkurugenzi wa TRA anatakiwa amshauri waziri cost benefit analysis ya maamuzi ya taxation na mambo mengine ya opportunity cost ili kwenda Tanzania ya viwanda.

Nchi nyingi zenye mfumo kama wetu wa unitary constitution hao ndio watu ambao technically indirectly wanaongoza nchi.

Sisi tunaokota tu kutoka vyuo vikuu, katibu mkuu ajawahi kuwa research assistant wizarani, he didn’t ascend based on performance, kama kateuliwa kutoka nje ya wizara ajawahi kuwa ata mkurugenzi wa wilaya kuelewa changamoto za kuimplent sera at delivery level au kushika nafasi yoyote ya strategic position katika maisha yake boom huyo kateuliwa nafasi sensitive.

Phase ya miundombinu imefanyika kwa ufasaha hila kama wapo serious na maswala ya kujenga uchumi wa viwanda things have to change.
 
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Albert Chalamila amemtaka Katibu mkuu wizara ya viwanda na biashara kuandaa kikao cha wadau wa cement kujadili bei ya bidhaa hiyo.

Chalamila amesema Mbeya wamefanikiwa na bei ya cement haijapanda hivyo anataka ubunifu wake utumike katika level ya taifa ambapo wasafirishaji cement ni sekta muhimu ya kujadiliana nao kumaliza kadhia hii.

Chanzo: ITV habari!
Huyu Chalamila akili zinamtosha kweli?
 
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Mh. Albert Chalamila amemtaka Katibu mkuu Qizara ya Viwanda na Biashara kuandaa kikao cha wadau wa Cement kujadili bei ya bidhaa hiyo.

Chalamila amesema Mbeya wamefanikiwa na bei ya Cement haijapanda hivyo anataka ubunifu wake utumike katika level ya taifa ambapo wasafirishaji Cement ni sekta muhimu ya kujadiliana nao kumaliza kadhia hii.

Chanzo: ITV habari!
Huyu kauona ukweli upo wapi na alichofanya ni busara
 
Acha uongo bei ya simenti kiwandani ni ile ile ila mtaani ni tofauti alicho sema anataka wajadili hali hii sio kwamba Mbeya simenti haijapanda
Na kujadili itapendeza maana watajua wapi kuna tatizo
 
Mwambieni afanye utaratibu wa kurudisha viwanda vilivyouzwa hapo Mbeya vianze uzalishaji.

Mbeya cement iko mkoani kwake huku tuliko hakuna kiwanda cement haipo
 
Nashangaa jambo moja kuna mikoa tangia 2016 sarujui hajawahi kushuka elfu 20/21. Ila kwa sasa naona wengi wanalalamika
 
Sijawahi kuona mifuko ya saruji
Kg 25
Kg 10
Kg 5

Hivi hili jambo haliwezekani ? Au ni utarstibu wa dunia nzima
Mimi sio Engineer wa ujenzi, lakini kutokana na uzoefu wangu wa saidia fundi, Mara nyingi mfuko wa cement una zile klai za zege 3 ambazo zinatumika kubalance uwiano wa mchanga kwenye plaster (sjui kiswahili chake vizuri) na kusakafia ..au kubalance na kokoto wakati wa kumwaga zege.kwa mantiki hiyo basi unakuta mfuko mzima unachukua uwiano wa 3:12 yaan kalai moja ya cement ina chukua kalai 4 za mchanga. Nimechangia tu sio kwamba ndo mantiki yake ..
 
Back
Top Bottom