Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewataka waandishi wa habari na vyombo vya habari nchini kuwa mabalozi wema katika kueneza na kuunga mkono jitihada za maridhiano ya kitaifa zinazoongozwa na Rais Samia
Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 11, 2026, Chalamila amesisitiza kuwa mchakato wa maridhiano ni nguzo muhimu katika kulinda amani na kuchochea maendeleo ya nchi, na kwamba hakuna nafasi ya kuendeleza migogoro isiyo na tija.
"Kama kuna mahali popote panahitaji sisi kuridhiana, tufanye kazi ya kuridhiana. Tusiendeleze ugomvi ambao utarudisha nyuma maendeleo ya taifa letu," amesema Chalamila.
Aidha, RC Chalamila ameeleza kuwa kutofautiana mawazo ni jambo la kawaida katika jamii yoyote, lakini hakupaswi kugeuka kuwa chanzo cha kuvunja amani ya nchi, amewataka wananchi na wadau wote wa maendeleo kujitokeza na kuunga mkono mchakato huo bila kujitenga, akibainisha kuwa milango ya kutoa maoni ipo wazi na kila sauti itasikilizwa.