RC Chalamila: Tufanye kazi ya kuridhiana, tusiendeleze ugomvi. Asitokee mtu kusema mimi sitaki kuridhiana

Richer

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2025
Posts
2,318
Reaction score
4,079

Your browser is not able to display this video.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, amewataka waandishi wa habari na vyombo vya habari nchini kuwa mabalozi wema katika kueneza na kuunga mkono jitihada za maridhiano ya kitaifa zinazoongozwa na Rais Samia

Akizungumza na waandishi wa habari leo Agosti 11, 2026, Chalamila amesisitiza kuwa mchakato wa maridhiano ni nguzo muhimu katika kulinda amani na kuchochea maendeleo ya nchi, na kwamba hakuna nafasi ya kuendeleza migogoro isiyo na tija.

"Kama kuna mahali popote panahitaji sisi kuridhiana, tufanye kazi ya kuridhiana. Tusiendeleze ugomvi ambao utarudisha nyuma maendeleo ya taifa letu," amesema Chalamila.

Aidha, RC Chalamila ameeleza kuwa kutofautiana mawazo ni jambo la kawaida katika jamii yoyote, lakini hakupaswi kugeuka kuwa chanzo cha kuvunja amani ya nchi, amewataka wananchi na wadau wote wa maendeleo kujitokeza na kuunga mkono mchakato huo bila kujitenga, akibainisha kuwa milango ya kutoa maoni ipo wazi na kila sauti itasikilizwa.
 
Mchakato ya Maridhiano
 
Si ndio hawa kabla ya uchaguzi, walikuwa hawataki kitu chochote zaidi ya kusikilizwa wao na kuwa buruza wengine. Sasa wameokoka au
 
Chalamila amekuwa Mkuu wa Mkoa Mwenezi wa CCM?
 
 

Attachments

  • 1000020485.jpg
    12.1 KB · Views: 12
  • IMG_0830.jpeg
    184.2 KB · Views: 12
Mkitaka maridhiano ni kuunda katiba mpya ya kufutwa kwa wakuu wa wilaya na mikoa,ambao ni makada wa ccm kupitia ujumbe wa Kamati za siasa na mikoa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…