RC Chalamila: Tunaweza kuwa na ‘Magufuli Ruling Party’ na mambo yakaenda vizuri kabisa

RC Chalamila: Tunaweza kuwa na ‘Magufuli Ruling Party’ na mambo yakaenda vizuri kabisa

Ebu tuombe radhi wana Mbeya kwa kutulinganisha na huyo mjinga
Mwalimu wa kiswahili huyo, bingwa wa kuchomekea maneno. wanambeya wanamkubali sana huyo mwamba wa lugha, hapo kawaacha CHADEMA , ACT, na wengine kuitafakari kauli hiyo bila majibu
 
Bado sina imani kama anakanusha serious.

Kama mwenyekiti wa Chama na mkuu wa nchi angekuwa tayari amekemea haya mambo juu ya subordinates wake.

Mambo mengi tu anakemea na hayazungumzwi tena.

Ila hili la utawala wa milele analikanusha kwa Kibaji, Chalamila analileta. Kuna jinsi hapa.

Itaenda hivi mwisho wa siku utasikia anasema basi wananchi wameamua niendelee japo nilikuwa sitaki, kama anavyosemaga alisukumiwa urais ata hili atasema alisukumiwa.
Hiyo haijatokea bahati mbaya haya yanapangwa taratibu taratibu kuna siku agenda itafikishwa bungeni na spika Ndugai atasikika akisema "waliosema Magufuli atawale milele wameshinda" ndo mtalia na kusaga meno
 
Hili swala tunalichukulia kama hawa watu wanajikomba ila ukweli ni kuwa kuna kila dalili kauli hizi zinatoka juu!!!. Magufuli ruling party??? Mkuu wa mkoa anayatamka haya mbele ya umati wa watu??, Hakika WTz tumeuvaa mkenge na tutabatizwa kwa moto.
 
Nimeisikia hii kupitia ITV huko mkoani Mbeya wilayani Kyela.

Ngoja niitafakari kidogo hii kauli ya RC Chalamila....... Nijiridhishe alichomaanisha.

Maendeleo hayana vyama!

ALICHOJIBU RAIS:

Rais Magufuli amesema mkuu wa mkoa Albert Chalamila anatamani tuwe na mfumo wa chama kimoja lakini yeye (Dr Magufuli) matamanio yake ni kuwa na mfumo wa vyama vingi lakini CCM iendelee kupata ushindi.

Rais Magufuli Magufuli anasema katika hilo anatofautiana na Mkuu wa Mkoa na kwa maana hiyo kila mmoja wao abakie na msimamo wake.

Hongera Rais Magufuli kwa kulitolea ufafanuzi wa haraka sana swala hili!

====================

Habari zaidi kutoka kwa Mdau mwingine

Katika ziara ya Raisi inayofanyika leo hapa Kyela, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amesikika akisema "Natamani kuwe na Chama kimoja Magufuli Ruling Party".

Akifafanua kauli hiyo Mkuu wa mkoa amesema "Kila mwezi unatusaidia kuwalipa watumishi 2471 wanao lipwa zaidi ya bil.1, pesa ambazo wewe mh. raisi Magufuli unazileta katika mji wa Kyela.

Ninacho shangaa unapokuta tunaendeleza malumbano katika mazuri hayo unayoyafanya, ambayo hatuna mahali popote pakuyalinganisha. Sioni sababu ya kua na mfumo wa vyama vingi Kyela zaidi ya kua na chama kimoja kinachoitwa "Magufuli Ruling party katika mazuri"

Akijibu hoja hiyo mh: raisi amesema "Mkuu wa mkoa anatamani kuwa na chama kimoja, lakini mimi natamani kuwe na vyama vingi sana vitakavyoleta ushindani lakini siku zote Ccm ndio iwe inashinda kwasababu ni kwa mujibu wa katiba yetu".
Maendeleo hayana chama
 
Jamaa wanatamani chama kipya ila ndiyo hivyo tena
IMG-20190430-WA0016.jpeg
 
Ni huyu huyu aliyeingia madarakani akapiga marufuku mikutano ya kisiasa hasa ya upinzani na maandamano yamebaki ya ccm pekee akidai kazi tu.

2. Ni huyu huyu alisema kabla ya 2020 atahakikisha kauwa upinzani wote.

3. Huyu huyu alisema shughuri za kisiasa mpaka uchaguzi lakini yeye kila siku anazifanya kwa mgongo wa rais na utekelezaji wa ilani ya chama.

ANATEKELEZAJE HAYO MAAZIMIO YA KUUWA VYAMA VYA UPINZANI

1. Kama sio ccm hakuna uteuzi wala nafasi ndani ya serikali iliyopewa jina la serikali ya Magufuli then serikali ya ccm ikiwa wewe sio mwana ccm huna sifa. Lakini kisheria serikali na chama ni vitu viwili tofauti serikali ni watu wote kwa sababu kodi inalipwa na wote.

2. Mikutano ya kiserikali imekuwa ya kichama inakuwa uccm zaidi kuliko ya kiserikali

3. Polisi na jesbi hawatoi vibari kwa vyama vya upinzani kufanya mikutano na maandamano zaidi ya ccm pekee hata jimboni kwa mbunge.

4. Kuwatumia watendaji wa serikali kuimarisha chama. Mfano Ded, RC, Dc kama Chalamila kalisema lile sio kwa bahati mbaya imepangwa ile na ndio wanatekeleza maazimio.

5. Vyombo vya habari vinaogopa kutoa habari kwa vyama vya upinzani. Kumbuka habari ya Zitto na barua ya msemaji wa rais kama msemaji wa chama sio serikali.

6. Bungeni hotuba kuhaririwa na kuhakikisha hakuna bunge live bali ikulu live sijui wanaomwangalia mwenyekiti wa ccm hawana kazi za kufanya?
 
wanajua ccm sio makazii yao ni 2020,watatafuta kazi za kufanya so wanajaribu kutaka kutuonesha Boss wao anawaza nini juu ya ccm anayoiharibu kila kukichaa na matukio ya kutengeneza.
 
Huyu boya anajipendekeza hadi anashtukiwa?
Ifike kipindi magufuli aachane na sifa za kishamba kama hizi
 
Anataka kuwepo na vyama vya upinzani kama CUF ya Lipumba ili kuhadaa wafadhili kuwa kuna mfumo wa vyama vingi, lakini visifikie kiwango cha kuitoa madarakani ccm.

Hili Magufuli kalisema kwakuwa hana siri, lakini hii ndio sera ya ccm dola inayotamba utawala milele. Jambo hili limekuwa likitekelezwa na marais wote kwa kushirikiana na vyombo vya dola na tume ya uchaguzi.

Kwahiyo box la kura ni kupoteza muda, machafuko tu ndio yatabadili hiki kinachoendelea hapa nchini.
 
hao ndio viongozi walioteuliwa na mkulu baada ya kuridhishwa na cv zao au tusubiri wengine?
 
Bado sina imani kama anakanusha serious.

Kama mwenyekiti wa Chama na mkuu wa nchi angekuwa tayari amekemea haya mambo juu ya subordinates wake.

Mambo mengi tu anakemea na hayazungumzwi tena.

Ila hili la utawala wa milele analikanusha kwa Kibaji, Chalamila analileta. Kuna jinsi hapa.

Itaenda hivi mwisho wa siku utasikia anasema basi wananchi wameamua niendelee japo nilikuwa sitaki, kama anavyosemaga alisukumiwa urais ata hili atasema alisukumiwa.
Ili kuleta usawa kwa vyama vyote Tz, Wenyeviti wa vyama vyote vya Siasa wawe na ukomo sio Mkiti wa chama miaka nenda rudi ni yeye tu. Kamuchezo ka design hii kako sana kule Vyama vya upinzani ndo mana na wenzenu wanatamani wakacheze.
 
Back
Top Bottom