Mwalimu wa kiswahili huyo, bingwa wa kuchomekea maneno. wanambeya wanamkubali sana huyo mwamba wa lugha, hapo kawaacha CHADEMA , ACT, na wengine kuitafakari kauli hiyo bila majibu
Kamuumbua na kumwachia aibuRais Magufuli kamtolea nje live!
Hiyo haijatokea bahati mbaya haya yanapangwa taratibu taratibu kuna siku agenda itafikishwa bungeni na spika Ndugai atasikika akisema "waliosema Magufuli atawale milele wameshinda" ndo mtalia na kusaga menoBado sina imani kama anakanusha serious.
Kama mwenyekiti wa Chama na mkuu wa nchi angekuwa tayari amekemea haya mambo juu ya subordinates wake.
Mambo mengi tu anakemea na hayazungumzwi tena.
Ila hili la utawala wa milele analikanusha kwa Kibaji, Chalamila analileta. Kuna jinsi hapa.
Itaenda hivi mwisho wa siku utasikia anasema basi wananchi wameamua niendelee japo nilikuwa sitaki, kama anavyosemaga alisukumiwa urais ata hili atasema alisukumiwa.
Maendeleo hayana chamaNimeisikia hii kupitia ITV huko mkoani Mbeya wilayani Kyela.
Ngoja niitafakari kidogo hii kauli ya RC Chalamila....... Nijiridhishe alichomaanisha.
Maendeleo hayana vyama!
ALICHOJIBU RAIS:
Rais Magufuli amesema mkuu wa mkoa Albert Chalamila anatamani tuwe na mfumo wa chama kimoja lakini yeye (Dr Magufuli) matamanio yake ni kuwa na mfumo wa vyama vingi lakini CCM iendelee kupata ushindi.
Rais Magufuli Magufuli anasema katika hilo anatofautiana na Mkuu wa Mkoa na kwa maana hiyo kila mmoja wao abakie na msimamo wake.
Hongera Rais Magufuli kwa kulitolea ufafanuzi wa haraka sana swala hili!
====================
Habari zaidi kutoka kwa Mdau mwingine
Katika ziara ya Raisi inayofanyika leo hapa Kyela, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amesikika akisema "Natamani kuwe na Chama kimoja Magufuli Ruling Party".
Akifafanua kauli hiyo Mkuu wa mkoa amesema "Kila mwezi unatusaidia kuwalipa watumishi 2471 wanao lipwa zaidi ya bil.1, pesa ambazo wewe mh. raisi Magufuli unazileta katika mji wa Kyela.
Ninacho shangaa unapokuta tunaendeleza malumbano katika mazuri hayo unayoyafanya, ambayo hatuna mahali popote pakuyalinganisha. Sioni sababu ya kua na mfumo wa vyama vingi Kyela zaidi ya kua na chama kimoja kinachoitwa "Magufuli Ruling party katika mazuri"
Akijibu hoja hiyo mh: raisi amesema "Mkuu wa mkoa anatamani kuwa na chama kimoja, lakini mimi natamani kuwe na vyama vingi sana vitakavyoleta ushindani lakini siku zote Ccm ndio iwe inashinda kwasababu ni kwa mujibu wa katiba yetu".
kwaio unataka kusema mkulu hajui katiba kiasi icho
Nyerere Alishawahi Kufuta Vyama Vya Siasa
Kwahiyo tufanye hilo tena kwa reference ya Nyerere?Nyerere Alishawahi Kufuta Vyama Vya Siasa
Ndiyo,itapendeza zaidiKwahiyo tufanye hilo tena kwa reference ya Nyerere?
Ili kuleta usawa kwa vyama vyote Tz, Wenyeviti wa vyama vyote vya Siasa wawe na ukomo sio Mkiti wa chama miaka nenda rudi ni yeye tu. Kamuchezo ka design hii kako sana kule Vyama vya upinzani ndo mana na wenzenu wanatamani wakacheze.Bado sina imani kama anakanusha serious.
Kama mwenyekiti wa Chama na mkuu wa nchi angekuwa tayari amekemea haya mambo juu ya subordinates wake.
Mambo mengi tu anakemea na hayazungumzwi tena.
Ila hili la utawala wa milele analikanusha kwa Kibaji, Chalamila analileta. Kuna jinsi hapa.
Itaenda hivi mwisho wa siku utasikia anasema basi wananchi wameamua niendelee japo nilikuwa sitaki, kama anavyosemaga alisukumiwa urais ata hili atasema alisukumiwa.