Asprin
JF-Expert Member
- Mar 8, 2008
- 68,223
- 96,083
Amekufundisha nini huyo kilaza?Hakuna alikoonesha ujuzi wa kutumia lugha hapo.Anajipendekeza mpaka Bosi anaona aibu kwa upuuzi anaoongea!
Ameniangusha sana Mwl wangu!!!!
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Amekufundisha nini huyo kilaza?Hakuna alikoonesha ujuzi wa kutumia lugha hapo.Anajipendekeza mpaka Bosi anaona aibu kwa upuuzi anaoongea!
Ameniangusha sana Mwl wangu!!!!
Kiswahili.in one of universities!Amekufundisha nini huyo kilaza?
. Kujikomba kukizidi fahamu huondoka. Mishahara ya watumishi ni baki zao, hulipwa na hazina, si kwa upendeleo wa rais. Kwa mtazamo wake (wa kichonganishi)marais awali watumishi hawakulipwa.
Kuna watu wanajua kujikomba jamani.😂
Doh pole sana kwa kufundishwa na mtu wa hovyohovyoKiswahili.in one of universities!
Alikuwa wa hovyo hivyo hivyo, u RC haujambadilisha chochote!!!
Kwenye harambee ya kuchangia ujenzi wa msikiti mbunge wa jimbo jirani kachangia millioni moja, yeye Rc mzima linalia kwa Rais eti Mheshimiwa Rais si unajuwa hatuna hela mimi nitachanga laki mbili, huu ndio unafki unaowakabili maccm wengi, Rc kachoka kama sisi tu halafu jukwaani unajaza ujinga watu wasiojitambuwa, too bad.Tangu aseme anapenda michepuko,huyu mkuu wa mkoa nikajua ni mropokaji
Taifa limejaa wajinga sanaRais Magufuli kamtolea nje live!
Watu wana utindio wa ubongoKwasasa akili itamkaa sawa maana kashushuliwa Kyela tena na Mpuguso akiendelea kutambulisha uongozi mkulu akasimama na kwenda kwenye mic na kumwambia ukitaka kuwatambulisha andaa mkutano wako uje utatue kero zao yamemshuka Mzee wa michepuko
Mbumbumbu FcMwalimu wa kiswahili huyo, bingwa wa kuchomekea maneno. wanambeya wanamkubali sana huyo mwamba wa lugha, hapo kawaacha CHADEMA , ACT, na wengine kuitafakari kauli hiyo bila majibu
kwaio unataka kusema mkulu hajui katiba kiasi ichoHajamtolea nje wala nini bali anawazuga mabwege. Rais katunga sheria ya vyama vya siasa ili hayo matamshi ya mkuu wa mkoa yatimie vizuri.
Huyo ni sawa na kina Nkamia akitegemea uwepo wa magufuli waendelee kuneemekaNimeisikia hii kupitia ITV huko mkoani Mbeya wilayani Kyela.
Ngoja niitafakari kidogo hii kauli ya RC Chalamila....... Nijiridhishe alichomaanisha.
Maendeleo hayana vyama!
ALICHOJIBU RAIS:
Rais Magufuli amesema mkuu wa mkoa Albert Chalamila anatamani tuwe na mfumo wa chama kimoja lakini yeye (Dr Magufuli) matamanio yake ni kuwa na mfumo wa vyama vingi lakini CCM iendelee kupata ushindi.
Rais Magufuli Magufuli anasema katika hilo anatofautiana na Mkuu wa Mkoa na kwa maana hiyo kila mmoja wao abakie na msimamo wake.
Hongera Rais Magufuli kwa kulitolea ufafanuzi wa haraka sana swala hili!
====================
Habari zaidi kutoka kwa Mdau mwingine
Katika ziara ya Raisi inayofanyika leo hapa Kyela, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amesikika akisema "Natamani kuwe na Chama kimoja Magufuli Ruling Party".
Akifafanua kauli hiyo Mkuu wa mkoa amesema "Kila mwezi unatusaidia kuwalipa watumishi 2471 wanao lipwa zaidi ya bil.1, pesa ambazo wewe mh. raisi Magufuli unazileta katika mji wa Kyela.
Ninacho shangaa unapokuta tunaendeleza malumbano katika mazuri hayo unayoyafanya, ambayo hatuna mahali popote pakuyalinganisha. Sioni sababu ya kua na mfumo wa vyama vingi Kyela zaidi ya kua na chama kimoja kinachoitwa "Magufuli Ruling party katika mazuri"
Akijibu hoja hiyo mh: raisi amesema "Mkuu wa mkoa anatamani kuwa na chama kimoja, lakini mimi natamani kuwe na vyama vingi sana vitakavyoleta ushindani lakini siku zote Ccm ndio iwe inashinda kwasababu ni kwa mujibu wa katiba yetu".