RC Chalamila: Wafanyabiashara wa Kariakoo wajitafakari, migomo siyo suluhisho

Shithole min
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila ametoa tamko la kuwataka Wafanyabiashara wote wa Mkoa wa Dar es salaam kujiepusha na migomo na kila mmoja kujitafakari, hii ni baada ya kusambaa kwa taarifa jana kuhusu Wafanyabiashara wa Dar es Salaam na Mikoa mingine kupanga kugoma.

View attachment 3023878

Akiongea Jijini Dar es salaam leo June 23,2024, Chalamila amesema “Masuala ya mgomo kwa Wafanyabiashara yasichukuliwe kuwa ni jambo la pamoja kila mmoja awe na tafakari ya kutosha kabla hajafikia wazo hilo la kufunga biashara, Mtu yeyote ambaye anaweza kuleta ubabe kutokusikilizana maana yake Serikali nayo inaweza kuamua kufanya hivyohivyo jambo ambalo hiyo sio falsafa hata kidogo ya Mh. Rais wa Tanzania”

“Wote tuungane kuijenga Dar es salaam, migomo sio suluhisho hata kidogo wala tusishabikie, mwisho wa mgomo inaweza ikawa ni vita ndogo ambayo ikamuathiri hata asiyekuwa na hatia”

Nawatakia Dominica njema 😃

Pia soma
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila ameyasema hayo mapema leo Juni 23,2024 Kufuatia uwepo wa taarifa za uvumi wa mgomo wa wafanyabiashara wa kariakoo ambapo amewataka wafanyabiashara kuepuka kushiriki kwenye masuala yanayoweza kuleta uvunjifu wa amani na kurudisha nyuma uchumi ikiwemo mgomo huu kwani Serikali imeshashughulikia baadhi ya changamoto na inaendelea kushughulikia changamoto za wafanyabiashara hususani zile zinazohusu mabadiliko ya Kisheria

RC Chalamila amewataka wafanyabiashara kutambua kuwa mgomo sio suluhisho pekee la kutatua changamoto bali utaratibu bora wa kutatua changamoto ni kukaa mezani na mamlaka kujadili kwani mgomo huongeza chuki na wakati mwingine kusababisha uvunjifu wa amani

Aidha RC Chalamila amesema kuwa Serikali inatambua changamoto za wafanyabiashara na kada zingine za wafanyakazi na watumishi na inaendelea kuzifanyia kazi hivyo amewataka wafanyabiashara kushirikiana na Serikali kumaliza changamoto zao na kuepuka mihemko inayoanzishwa na watu wachache wasio kuwa na nia njema na Mkoa wa Dar es salaam na Taifa kwa ujumla

Sanjari na hilo RC Chalamila amesema ujenzi wa soko jipya la kariakoo na ukarabati wa soko liloloungua kuwa soko hilo linalojengwa kwa zaidi ya shilingi bilioni 28 lipo katika hatua za mwisho na kwamba Rais Dokta Samia atakuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa soko hilo na wafanyabiashara waliokuwepo zamani na wapya wataingia kwa utaratibu maalum utakaotolewa na uongozi wa soko hilo

Vilevile katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Albert Chalamila amezungumzia oparesheini ya kuwaondoa wafanyabiashara za ngono (Dada Poa) inayofanyika Wilayani Ubungo na kusema kuwa Mila,Desturi na Tamaduni za Tanzania hazikubaliani na biashara hiyo ya ngono pamoja na ndoa za jinsia moja hivyo Serikali mkoani humo itaendelea kupinga vitendo
D

Shithole country
 
Hivi Vyeo vya u RC ni vya Kikoloni kazi yake ilikuwa ni kumlaza Mwafrika na sisi baada ya Uhuru tukavirithi.
 
anaongelea ngono tu!Sijui anaakili gani aisee!Hivi anapokua anahamasisha pombe kila mara huwa hajui kwamba anahamasisha ngono indirectly?Vichwa vingine bana🫥
 
Hana hoja ni vitisho tu ambavyo sidhani ni njia sahihi, naona kabisa jamaa wataendelea na mgomo wao. Alipaswa kuwasihi katika lugha za kiungwana manake hela wanazo wale jamaa wa kkoo.
 
Tunatingisha ila ipo wazi Wafanyabiashara kugoma kwa zaidi ya wiki si rahisi sababu ili hilo litokee inabidi tuwe na reserve ya kutosha kulipa mikopo.

Unless, kama inawezekana kushawishi mabank yatoe grace period ya miezi kama mitatu ya kutopeleka marejesho ili kuwezesha hilo zoezi la kugoma mpaka kusikilizwa kukamilika.

Pia serikali ina mbinu nyingi sana za kutugawanya tusiwe kitu kimoja kwa matamko tu, mfano serikali ikisema:

"ATAKAYEFUNGA DUKA KWA SIKU ZAIDI YA TATU ATAFUTIWA LESENI NA KUTAKIWA KUOMBA UPYA, UTARATIBU HUU UTAAMBATANA NA KULIPA MADENI YOTE YA KIKODI KABLA YA KUPATIWA LESENI"

Wafanyabiashara tunagawanyika, unless lile la marejesho liwe limewezekana. La marejesho likiwezekana Serikali itaingiwa na hofu maana ikipita wiki tu bila biashara kutachafuka vibaya mno.
Hakuna benki kichaa kama mawazo yako, leseni ni mkataba hakuna namna ya kuufuta, wakifuta watarajie kulipa fidia.
 
  • Thanks
Reactions: I M
kesho ni muendelezo wa sakata la sukari lililoibuliwa na mbunge Luhag Mpina dhidi ya mkimbizi fisadi Bashe
 
Boss, si rahisi mwanasiasa kumuelewa mfanyabiashara, si rahisi mwajiriwa serikalini kumwelewa mfanyabiashara. Siku zote mfanyabiashara ni kama adui badala ya mshirika, anatungiwa sera za kudhibitiwa. Kabla hujaanza biashara Serikali imeshakudhibiti kupitia mifumo ya kifedha na kikodi na lazima ujae kwenye mfumo.
Ina maana unasema wafanyabiashara ndio waovu na hawaendani na mfumo wa serikali ndo unachomaanisha?

If that yes, unafikiri kwanini wanagoma wafanyabiashara kila inapobidi wao kufanya hivyo?

Mimi sio mfanyabiashara bana nataka kujua tu Bw. Tsh
 
Swala la kukagua sales, purchases, expenses na kufuta VAT returns hilo hapana aisee, hapo serikali inatuumiza
 
Hakuna benki kichaa kama mawazo yako, leseni ni mkataba hakuna namna ya kuufuta, wakifuta watarajie kulipa fidia.
Hoja ipo wazi, mgomo hauwezi kudumu sababu watu wana marejesho kwenye mabank, unless mabank nayo yaamue kushirikiana kwenye mgomo. Hayo mengine mbwembwe zako tu.
 
Ina maana unasema wafanyabiashara ndio waovu na hawaendani na mfumo wa serikali ndo unachomaanisha?

If that yes, unafikiri kwanini wanagoma wafanyabiashara kila inapobidi wao kufanya hivyo?

Mimi sio mfanyabiashara bana nataka kujua tu Bw. Tsh
Wafanyabiashara ndo wanailisha nchi kupitia kodi. Bila wao hata hajira hakuna. Yaani unavyomuona afisa wa TRA mshahara wake unatokana na jasho la wafanyabiashara.
 
Waache wagome maana selikari haitekelezi ahadi zake
 
  • Thanks
Reactions: I M
Back
Top Bottom