RC Chalamila: Wafanyabiashara Wadogo wa Simu2000 wafahamu kuwa eneo walilopo ni la Serikali, lazima liendelezwe

RC Chalamila: Wafanyabiashara Wadogo wa Simu2000 wafahamu kuwa eneo walilopo ni la Serikali, lazima liendelezwe

Chalamila amesema Yeye ni level nyingine

Level gani hiyo inayowazidi Viongozi Wote?!

Nimekaa pale 🐼
Huyu sio mtu wa mchezo mchezo, angalia alichomfanya kibaka mmoja...https://www.jamiiforums.com/threads/this-man-is-either-a-sadist-or-alimuua-kibaka-akanywa-bia-kusherehekea.1622901/
P
 
Shida anadhania kufoka ndio suluhisho.
Sahihi
Hajajibu madai ya daladala kuwa hawataendelea kupewa leseni na Latra njia ya simu 2000 na je na hao machinga watabaki au kuhama? . Shida nchi hii kuna ujajnja mwingi
Angejibu hayo mawili kwanza

Kufoka foka kufokea watu wazima sio sahihi
 
RC ana mamlaka makubwa, anachotakiwa ni kuwataka watendaji wasimamie Kwa mujibu wa sheria
Sahihi lakini wananchi wakichachamaa mamlaka yaweza ondoka

Refer case ya Kenya baraza zima la mawaziri limepigwa chini
 
Kwa kusema dharau viongozi wote ila siyo Mimi?
Hasira za kihehe zimempanda
Wahehe wakipanda hasira huwa wanapoteza network kati ya mdomo na mara wa mawasiliano na ubongo ndio maana wengi hujinyonga.Sababu network ya mnara wa ubongo huwa hamna.Hasira za wahehe zikipanda
 
Alidhani anatengeneza watu wazalendo kama akina Butibu, Warioba kumbe anatengeneza majangili ya mali za umma
Warioba mzalendo!?..unalijua sakata lake la vyama vya ushirika,mjombaake Nyerere akamwambia mpwae arudishe alichopewa huko kanda ya ziwa!?
 
RC CHALAMILA ATIMIZA AHADI YA KUKUTANA NA WAFANYABIASHARA WA SIM 2000

-Awakutanisha DART, Manispaa ya Ubungo na Wafanyabishara wadogo.
-Aeleza dhamira ya Serikali kutekeleza mradi huo
-Asisitiza bado serikali itaendelea kujali na kuweka mazingira rafiki kwa wafanyabiashara wadogo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila leo julai 13,2024 amekutana na wafanyabishara wa Simu 2000 ikiwa ni ahadi aliyoitoa wiki iliyopita baada ya wafanyabiashara hao kufanya mgomo katika eneo hilo.

RC Chalamila akiwa katika eneo la kituo cha Simu 2000 amewakutanisha wafanyabiashara hao na wakala wa mabasi yaendayo kasi DART, na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo ambapo mawasilisho ya utekelezaji wa mradi wa kujenga karakana kwa ajili ya mabasi ya mwendokasi na umuhimu wake kwa pande zote mbili Manispaa na DART yaliwasilishwa kwa uwazi mbele ya wafanyabiashara hao

Aidha RC Chalamila alitoa nafasi kwa wafanyabiashara hao kutoa maoni huku akiweka wazi dhamira ya serikali kutekeleza mradi huo ambao una masilahi mapana kwa umma na kuwahakikishia pamoja na kutekelezwa kwa mradi huo bado kuna sehemu ambayo wafanyabiashara hao watapatiwa ili kufanya biashara zao lakini pia katika kipindi chote cha kutekeleza mradi huo utaratibu utawekwa ili kutovuruga biashara zilizoko.

Vilevile RC Chalamila amesema hakuna serikali isiyojali wafanyabiashara bali inapotokea kuna mradi wenye masilahi mapana kwa umma lazima tupishe,pia sio vizuri kuwa na migomo ya mara kwa mara kama una maoni au ushauri wasilisha katika njia nzuri “wale wote waliotoa maoni leo yenye tija wakati wa kutekeleza mradi huo yatazingatiwa kwa umakini mkubwa”.Alisema Chalamila

Mwisho RC Chalamila ametoa rai kwa wakazi wa Mkoa huo kuilinda Dar es Salaam kwa nguvu zote Amani ikitoweka athari zake ni kubwa.

View: https://www.youtube.com/watch?v=ParVZCgSBAI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Albert Chalamila amesema kuwa ni lazima wafanyabiashara wadogo (Wamachinga) waliopo Simu2000 waliodaiwa kugoma wakafahamu na kuelewa kuwa eneo walilopo ni la Serikali na ni lazima liendelezwe kwa manufaa ya Serikali na Wananchi.
"Wote lazima mfahamu kwamba hili eneo la Simu2000 ni eneo la serikali na ni lazima liendelezwe kwa manufaa ya serikali na wananchi, hii yote ni miradi ya serikali hata Kariakoo na Mwenge mnayoiona leo haikuwa hivo miaka ya nyuma lakini serikali imeendeleza maeneo hayo mpaka leo watu wanafurahia, mwanzo siku zote lazima utakuwa mgumu lakini serikali ina nia njema na wananchi wake" Albert Chalamila - Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam

Ameyasema hayo leo Jumamu Julai 13, 2024, siku ambayo aliwaahidi wafanyabiashara hao waliogoma siku ya Julai 8, 2024 na kufunga biashara zao na kuweka vizuizi vya kufunga barabara huku wakizuia magari kuingia na kutoka katika kituo cha daladala chanzo kikidaiwa ni kupinga uamuzi wa Manispaa ya Ubungo kukabidhi eneo wanalofanyia biashara kwa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa ajili ya kujenga karakana ya mabasi ya mwendokasi.

Itakumbukwa wafanyabiashara hao hawakuwa tayari kumsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Ubungo wakidai kuwa madai yao amshindwa kuyasikiliza kwa wakati, baada ya sintofahamu hiyo Chalamila alifika eneo hilo na kuwahasa wafungue biashara huku akiahidi kufanyia kazi madai hayo kwa kuketi na mamlaka nyingine na kuleta majawabu leo Julai 13, 2024,

"Wote lazima mfahamu kwamba hili eneo la Simu2000 ni eneo la serikali na ni lazima liendelezwe kwa manufaa ya serikali na wananchi, hii yote ni miradi ya serikali hata Kariakoo na Mwenge mnayoiona leo haikuwa hivo miaka ya nyuma lakini serikali imeendeleza maeneo hayo mpaka leo watu wanafurahia, mwanzo siku zote lazima utakuwa mgumu lakini serikali ina nia njema na wananchi wake" amesema Albert Chalamila

Hata hivyo Chalamila amewaonya wafanyabiashara hao kutorudia tena utaratibu wa kufunga barabara, ambapo amedai kwamba wakirudia kufanya hivyo hawatarudi kufanya biashara eneo hilo.

"Mkifanya tena mchezo kama mlioufanya juzi wa kufunga kituo cha mabasi cha Simu2000 nitawachukulia hatua wote kwasababu hiki kituo ni mali ya umma na sio yenu mngeweza kufunga maduka na biashara zenu mkaacha kituo kiendelee na shughuli zake lakini mkijaribu tena kufunga kituo mjue hamtorudi tena kwenye kituo cha simu 2000" amesema Albert Chalamila.

===============

CHALAMILA: ENEO LA SIMU2000 NI LA SERIKALI LAZIMA LIENDELEZWE
DAR ES SALAAM: Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila amesema lazima Wafanyabiashara Wadogo (Wamachinga) waliopo eneo la Simu2000 waliofanya mgoma na kuziba Barabara wafahamu kuwa eneo walilopo ni la Serikali na lazima liendelezwe kwa manufaa ya Nchi.

Akizungumzia mpango uliopo wa sehemu ya eneo hilo kukabidhiwa kwa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa ajili ya ujenzi wa karakana, jambo ambalo lilipingwa na baadhi ya Wamachinga waliofanya mgomo, Chalamila amesema “Hii yote ni miradi ya Serikali, hata Kariakoo na Mwenge mnayoiona leo haikuwa hivyo miaka ya nyuma.”

Amesema hayo leo Julai 13, 2024 baada ya baadhi ya Machinga kugoma na kufunga Stendi ya Daladala katika Kituo cha Simu2000, Julai 8, 2024.

CHALAMILA: HATUWEZI KUENDESHA MKOA UKIWA NA MIGOMO-MIKOMO
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewataka Wafanyabiashara kuheshimu mamlaka ya Serikali na ya Mkuu wa Mkoa wakati akizungumza nao kuhusu mipango iliyopo kuhusu uendelezaji wa eneo la Simu2000, akiwakanya walioonesha kumpinga na kupinga mkakati huo.

Pia, ameonya tabia ya kufanya mgomo mara kwa mara kutoka kwa Wafanyabiashara akisisitiza sio njia sahihi ya kuendesha Mkoa, amesema hayo leo Julai 13, 2024 wakati akizungumza na Wafanyabiashara waliogoma na kufunga Stendi ya Daladala katika Kituo cha Simu2000, Julai 8, 2024.

CHALAMILA: CHEZEENI VIONGOZI WOTE ILA MSIGUSE HII KICHWA, NIPO LEVO NYINGINE YA MAAMUZI
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amewaonya Wafanyabiashara waliofunga eneo la Stendi ya Daladala katika Kituo cha Simu2000, Julai 8, 2024, akisema bora wafunge biashara zao na sio kituo au Barabara.

Amesema “Kuna Watu mmepangana vilio, vimachozi, amekufinya mumeo unataka kuja kunililia mimi... chezeeni pote mnapoweza kuchezea, Viongozi wote chezeeni ila msiguse hii kichwa, nipo kwenye levo nyingine sana ya maamuzi.

Ameyasema hayo leo Jumamosi Julai 13, 2024 wakati wa kikao kati yake na Wafanyabiashara wa Simu2000.
View attachment 3041442
View attachment 3041443

Hilo eneo lingine analotaka kuwapa wafanyabiashara awape DART. Viongozi wetu hawafikirii, pale Simu 2000 kwa sasa ni mjini sana, hiyo gereji ya DART wangepeleka Mbezi huko. Pale Simu 2000 ni eneo la makazi na ni mjini sana kuweka karakana. Kutoka hapo Simu 2000 ni chini ya kilometa moja kutoka soko la biashara la Afrika mashariki [terminal ya zamani]; najiuliza kulikuwa na sababu gani kuiondoa Ubungo Terminal na kuipeleka Mbezi? Kwa nini hiyo karakana isipelekwe Mbezi pia?

Vv
 
CHALAMILA: ENEO LA SIMU2000 NI LA SERIKALI LAZIMA LIENDELEZWE
DAR ES SALAAM: Mkuu wa Mkoa, Albert Chalamila amesema lazima Wafanyabiashara Wadogo (Wamachinga) waliopo eneo la Simu2000 waliofanya mgoma na kuziba Barabara wafahamu kuwa eneo walilopo ni la Serikali na lazima liendelezwe kwa manufaa ya Nchi.

Akizungumzia mpango uliopo wa sehemu ya eneo hilo kukabidhiwa kwa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka (DART) kwa ajili ya ujenzi wa karakana, jambo ambalo lilipingwa na baadhi ya Wamachinga waliofanya mgomo, Chalamila amesema “Hii yote ni miradi ya Serikali, hata Kariakoo na Mwenge mnayoiona leo haikuwa hivyo miaka ya nyuma.”

Amesema hayo leo Julai 13, 2024 baada ya baadhi ya Machinga kugoma na kufunga Stendi ya Daladala katika Kituo cha Simu2000, Julai 8, 2024.
Leo amewageuka
Huyu si alisema majuzi anahisi DC alikula rushwa!?
 
Anasikika Chalamila RC wa Dar akitoa mkwara mbuzi kwa wafanyabiashara wa Simu 2000. Anasema yeye ni level nyingine, wachezee viongozi wote isipokuwa yeye. Anasema usicheze na kichwa chake.

MyTake:
RC Chalamila bado yuko kwenye siasa za Mwendazake, halafu hajui kuwa Gen Z wako moto sana. Mkwara wake ni wa mbuzi tu kwa vile anajivunia Polisi alionao hapo. Otherwise hana lolote na ni mwepesi sana
 
View attachment 3041550

Mtikise sasa ujue mkwara wake ni wa mbuzi au simba wa yuda
 
Napenda sana viongozi wenye kujiamini ila wasisahau kuna haki za watu sio kila siku serikali ipo sawa. Haki za watu ni muhimu saba kuzizingatia sababu hata maandiko yanasisitiza hivyo. Ila watu nao wasitumike kisiasa.
 
View attachment 3041550

Anasikika Chalamila RC wa Dar akitoa mkwara mbuzi kwa wafanyabiashara wa Simu 2000. Anasema yeye ni level nyingine, wachezee viongozi wote isipokuwa yeye. Anasema usicheze na kichwa chake.

MyTake:
RC Chalamila bado yuko kwenye siasa za Mwendazake, halafu hajui kuwa Gen Z wako moto sana. Mkwara wake ni wa mbuzi tu kwa vile anajivunia Polisi alionao hapo. Otherwise hana lolote na ni mwepesi sana
Hivi kabla ya teuzi wanapimwa akili wapi
 
Tumezoea kubembeleza Wavunja Sheria za mipango mini Nchi hii. Wacha waambiiwe ukweli
 
Back
Top Bottom