RC Chalamila: Wanaomzungumzia Wanu na Abdul, hawajawahi kukutana nao

RC Chalamila: Wanaomzungumzia Wanu na Abdul, hawajawahi kukutana nao

Kinachowasumbua CHADEMA ni Wivu ,Chuki Binafsi,roho mbaya na roho za kimaskini na Kishetani zilizo tawala mioyo yao
 
Hivi hawa chawa huwa wanameza saa ngapi mistari ya kusifia? Mbona hatuwaoni wakienda msibani kwa mama Karume, au kwakuwa hiyo familia kwa sasa haina cha kuwapa?
Anything but uonekane umesifia

Inakera sana hii kitu
 
Ndio maana tuna kila sababu ya kupigania Katiba Mpya. Ni pamoja na kuondoa vyeo vya ambavyo anavyogawa raisi (anateua watendaji husika), ambavyo ndio zao la uchawa. RC, DC n.k. Raisi abaki na wateule wachache kama rasimu ya Warioba ilivyopendekeza.

Raisi kwa Katiba iliyopo anatengeneza machawa. Mfano Majaji, lazima waombe kazi, wapitishwe na chombo huru, hivyo hivyo kwa Spika, n.k
 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila amesema watu wengi wanaowazungumzia watoto wa Rais Samia Suluhu Hassan akiwemo Wanu Hafidh, Abdul na Ahmed hawajawahi kukutana nao ana kwa ana wakaujua uhalisia wao.

Akizungumza kwenye hitma ya marehemu Hafidh Ameir aliyekuwa mume wa Rais Samia, Chalamila amesema watoto wa marehemu Hafidh wanawapenda na kuwahurumia Watanzani na kwamba wamelelewa kwenye mazingira mazuri.

Uchawa ni tatizo la kitaifa!
 
Back
Top Bottom