RC Chalamila: Waziri Mkuu, Majaliwa kuanza ziara ya siku mbili Mkoani Mbeya, namshukuru Rais Magufuli kwa ujenzi wa Hospitali ya Rungwe

RC Chalamila: Waziri Mkuu, Majaliwa kuanza ziara ya siku mbili Mkoani Mbeya, namshukuru Rais Magufuli kwa ujenzi wa Hospitali ya Rungwe

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Albert Chalamila amesema Waziri Mkuu, Majaliwa anaanza ziara ya siku mbili mkoani Mbeya.

Akiwa mkoani Mbeya Mhe. Majaliwa atafungua Jengo la Mama na Mtoto jijini Mbeya, atafungua hospitali iliyoahidiwa na Rais Magufuli wakati wa kampeni wilayani Rungwe na atafungua kituo cha pamoja cha forodha (One Stop Center) wilayani Kyela.

Aidha, Chalamila amemshukuru sana Rais Magufuli kwa kutimiza ahadi yake ya kujenga hospitali Wilayani Rungwe yenye thamani ya Tsh. 481 milioni.

Chanzo: Channel Ten

Maendeleo hayana vyama!
 
Hongereni watu mbea kutimiziwa mahitaji yenu let jmapili maombi maombi maombi yanahitajika japotunachokiombea hatujui tunamuombea nn?
 
Unakichaa we jamaa, mwanaume rijali unaanzaje kulike taarifa toka channel ten? The undecided man to have ever existed in Mbeya. By the way, don't shoot the messenger, the message umepata?

Rungwe tumejengewa hospital.
Mwanaume rijali unaanzaje kutazama TBC na Channel 10?
 
Nimepita huko miaka kadhaa kwenda Itete hospital.

Barabara ya Masoko iliyoahidiwa na Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Magufuli vipi?

Lakini hayanihusu ngoja nirudi kwetu Simiyu.
 
Ninesoma kwamakini sana hii taarifa nimegundua iko sahihi maana haina tarehe wala siku ya kuanza hiyo ziara.
Nimekuelewa sana John
😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂😂
 
Ratiba hii hapa ya tarehe 14 imeshayumba tusubiri ya leo
 

Attachments

  • IMG-20210314-WA0004.jpg
    IMG-20210314-WA0004.jpg
    144.4 KB · Views: 1
Kama nakuona roho inavyokuchachamaa. Kwani unataka nini yani. Unataka kusikia mtu kafa? Roho ya kishetani ikushinde na uleghee.
Usidhani huyo member roho huyo inaishia ngazi ya taifa, hapana anawaza hivyo hadi kwenye ukoo na familia yake....yeye anatamani kuona mazishi tu!
 
chalamila hajui kuwa imeahirishwa?
Akae kwa kutulia asuburi tamko
 
Back
Top Bottom