Miss Zomboko
JF-Expert Member
- May 18, 2014
- 4,599
- 9,532
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema kuanzia sasa siyo hiari kuvaa barakoa bali ni lazima kwa watu wanaotumia usafiri wa umma au wanaokwenda au kuingia katika vituo vya mabasi.
Makalla ameeleza hayo, Jumatatu Agosti 2, 2021 wakati akizungumza na wanahabari kuhusu mwenendo wa uchukuaji wa tahadhari kwa wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam.
Amesema wamefanya tathimini na kubaini kuna baadhi ya maeneo ikiwemo vyombo vya usafiri kuna ulegevu wa uchukuaji wa tahadhari.
Makalla ametoa msimamo huo, akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama wa Mkoa wa Dar es Salaam, akisisitiza kuwa ugonjwa wa corona upo na wagonjwa wapo katika hospitali za Serikali na binafsi , lazima wananchi waendelee kuchukua tahadhari za kujikinga.
"Ukiingia kwenye gari, kivuko lazima uvae barakoa, hili ni moja ya sharti. Nimefanya survey ukienda Kivukoni Feri mtu anaingia na barakoa kwa sababu ya usimamizi akiwa ndani anaivua, akitaka kutoka anaiva tena," amesema Makalla.
"Tumepokea taarifa ya utekelezaji wa mwongozo wa Wizara ya Afya kuhusu kujikinga na corona kutoka kila wilaya tumebaini kuna ulegevu wa utekelezaji wa jambo hili. Sasa utekelezaji wa hiari haupo tena bali ni lazima ili kukabaliana na changamoto hii," amesema Makalla.
Makalla amesema wamiliki wa vyombo vya usafiri wa umma, vivuko lazima kuzingatia jambo hilo, akisema suala la kuchukua tahadhari ikiwemo kuvaa barakoa siyo hatua ya kuiridhisha mamalaka husika bali usalama wa mwananchi.