Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Swali la kijinga kabisa.Hivi ukivaa barakoa huwezi kufa au kuambukizwa uviko??
Why utunze, hata ukichukua tahadhari ka wengine hawachukui ni kazi bureNgoja niitunze hii comment. Nitakuja kukumbusha mbele ya safari!
Hili neno mjeledi linatumika sana mwambao wa pwani.Yani makala amepuuzwa asipotumia askari na na watu wa vyombo vya umma kupigwa fine watu hawatafata utaratibu, Yani hapo wakipigwa fine konda hatakubali kuruhusu abiria asiye na barakoa na mask kupanda. Punda haendi bila mjeledi
Matamko ni mengi kuliko data za kupima!!Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla amesema kuanzia sasa siyo hiari kuvaa barakoa bali ni lazima kwa watu wanaotumia usafiri wa umma au wanaokwenda au kuingia katika vituo vya mabasi.
Makalla ameeleza hayo, Jumatatu Agosti 2, 2021 wakati akizungumza na wanahabari kuhusu mwenendo wa uchukuaji wa tahadhari kwa wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam.
Amesema wamefanya tathimini na kubaini kuna baadhi ya maeneo ikiwemo vyombo vya usafiri kuna ulegevu wa uchukuaji wa tahadhari.
Makalla ametoa msimamo huo, akiwa ameambatana na kamati ya ulinzi na usalama wa Mkoa wa Dar es Salaam, akisisitiza kuwa ugonjwa wa corona upo na wagonjwa wapo katika hospitali za Serikali na binafsi , lazima wananchi waendelee kuchukua tahadhari za kujikinga.
"Ukiingia kwenye gari, kivuko lazima uvae barakoa, hili ni moja ya sharti. Nimefanya survey ukienda Kivukoni Feri mtu anaingia na barakoa kwa sababu ya usimamizi akiwa ndani anaivua, akitaka kutoka anaiva tena," amesema Makalla.
"Tumepokea taarifa ya utekelezaji wa mwongozo wa Wizara ya Afya kuhusu kujikinga na corona kutoka kila wilaya tumebaini kuna ulegevu wa utekelezaji wa jambo hili. Sasa utekelezaji wa hiari haupo tena bali ni lazima ili kukabaliana na changamoto hii," amesema Makalla.
Makalla amesema wamiliki wa vyombo vya usafiri wa umma, vivuko lazima kuzingatia jambo hilo, akisema suala la kuchukua tahadhari ikiwemo kuvaa barakoa siyo hatua ya kuiridhisha mamalaka husika bali usalama wa mwananchi.
Atabwabwaja mpaka siku anatumbuliwa asitegemee watu wote watavaa barakoa.huyu mkuu wa mkoa watu wanamdharau ama? kwa sababu hakuna anayevaa barako wala nini.
Hizo data za Kila wiki zitakusaidia Nini? Kama unazihitaji Sana nenda hospital watakupa.Matamko ni mengi kuliko data za kupima!!
Hii wizara ya afya na uongozi wake wote hawatufai! Misaada ya vifaa mmepokea lakini hatusikii vipimo vya kila wiki vinasemaje. Pia tume iliyoundwa kutathmini upokeaji wa chanjo haulioni hilo kuwa muhimu!
Hii ndio Tanzagiza kweli!
Huyu Makala hajapanda hata Bajaj halafu anatudanganya kuwa kafanya utafiti, alipanda daladala la kwenda Mbagara skaona hayo anayoyasema?Nimeona madalada yamejaza na watu kusimama with no barakoas at all
Makala ukuu wa mkoa wa Dar umemushinda full matamko ila utekelezaji sifuri ana kwama wapi aisee, na ana vyombo chini yake vingi yeye ni matamko tu hadi bashite mzee wa fa fa fa kamshinda mbaliHuyu Makala hajapanda hata Bajaj halafu anatudanganya kuwa kafanya utafiti, alipanda daladala la kwenda Mbagara skaona hayo anayoyasema?
Huyu jamaa ni pumba sana.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Hili neno mjeledi linatumika sana mwambao wa pwani.
Yaani afadhali hata Bashite alikuwa active sana, ila huyu Makala hafai kuwa RC popote.Makala ukuu wa mkoa wa Dar umemushinda full matamko ila utekelezaji sifuri ana kwama wapi aisee, na ana vyombo chini yake vingi yeye ni matamko tu hadi bashite mzee wa fa fa fa kamshinda mbali