2019
JF-Expert Member
- Dec 31, 2018
- 3,130
- 4,735
Kwa sasa nyumba nyingi za ibada zinakimbiwa na waumini, hii unatokana waumini kuchoshwa na mienendo ya kanisa ambayo ni tofauti na lilichoachwa na mitume.
Jumuia inabaki na wabibi tena wachache sana hata kupita mtaani kupeleka msalaba nyumba nyingine wanaona aibu.
MAMBO YANAYOCHOSHA
Nipokuwa katoliki sikuweza kufungua Biblia wala kuielewa mpaka nilipochukua hatua mwenyewe.
Mafundisho mengi ya uongo, hii imefanya waumini kuanza kuichunguza Biblia ili kupatanisha na mafundisho yanapoonekana ni tofauti wengi wanakata tamaa na kuhamia sehemu nyingine au kuchana na kanisa kabisa.
ULAFI WA VIONGOZI WA KIROHO
Kiongozi wa dini anafundisha upendo lakini yeye akiwa mbinafsi na Asiyejali.
UBAGUZI
Waliopewa dhamana wanaangalia zaidi maslahi kuliko kondoo, mwenye pesa ndio huzikwa na Padri hata kama hakuwa muumini, asiye na pesa atazikwa na jumuiya tu.
MICHANGO MINGI.
Hii toa toa tu ya ulichonacho kimekatisha wengi tamaa, kutoa sadaka kwa mstari kunapunguza waumini sababu kuna mengine weenda kusikiliza neno lakini hawana chochote, anapobaki kwenye benchi anaaibika na siku nyingine haji.
USIRI NA KULINDANA
Kuna vitendo vingi sana vya unyanyasaji kingono vinavyofanywa na mapandri dhidi ya vijana wadogo, mapadri kuzaa na masista kisiri, mapadri kuwa na watoto mitaani na hakuna hatuwa wanayochukuliwa.
Kilichobaki kwenye hizi dini kubwa ni kurithishana dini tu wala si mafundisho tena,ukizaliwa romani basi na ww ni mroma, ukizaliwa uislamu na ww utakuwa muislamu lakini mafundisho halisi ya dini yako unakuwa hujui hata kidogo,hata kuitetea imani inakupa tabu.
Ombeni nanyi mtapewa,Tafuteni nanyi mtapata, TAFUTENI KWELI MTAKUWA HURU.