RC Dodoma tembelea Stendi ya Daladala Sabasaba ujionee jinsi Wamachinga wako hatarini

RC Dodoma tembelea Stendi ya Daladala Sabasaba ujionee jinsi Wamachinga wako hatarini

Kurunzi

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2009
Posts
9,753
Reaction score
10,747
Jana nilipita pate stendi ya Daladala ya saba saba Dodoma hali niliyoiona pale ni ya kutisha, nilijiuliza sana akiwa watu wanaakili sawa sawa.

Wamachinga kama wote wamepanga biashara ndani ya stendi chini, sehemu Daladala zinapita wao wamepanga biashara zao, Daladala inabidi wapige hone ili ahamishe mchicha wake na gari ipite

Sijui viongozi wa jiji kama walishafika hapo wakaona hali ya hapo.

Siku daladala ikipata hitilafu watakufa watu kama njugu, nafikiri hapo ndipo viongozi wetu watashituka, hii haiwezi kuwa sahihi.
 
Pole mkuu. Umeandika kwa hisia sana hadi umechapia balaa. Lakini umeeleweka na umefanya jambo jema kuipa jamii taarifa. Hakika umefanya kile unachoweza katika kujenga nchi.
 
Umeandika kwa hisia sababu ni mgeni eneo hilo,tangu enzi za JpM ndio walipata kiburi hao wafanyabiashara ukiwagusa sahv watasema Angekuepo Magu wasingeteswa hivo kila kiongozi anaogopa kuwatoa pale,pale ni familia kama 150 zinapata ulaji utazipeleka wapi???

Vipi mkuu una mishe gani mjini unipe hata dili la buku tu.
 
Taifa lenye wamachinga wengi kuliko hata watembea kwa miguu ni bomu linalokaribia kulipuka.
 
Machinga ni wapiga kura wa chama pendwa, hawaguswi hao, bila kusahau bodaboda.
 
Na ole wenu mtuguse...baba atafufuka huko kaburini
 
Suala la Machinga liende chuo cha Ardhi kwanza

waje na majibu meeengi afu zichaguliwe suluhu kadhaa...

viongozi msikurupuke
Serikali imelea hili tatizo ila ni fursa likitumiwa vizuri...
 
Back
Top Bottom